Pages

Thursday, May 16, 2013




 Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.

 JESHI la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru mwenye umri wa miaka 44 aliyevalia mavazi ya kitawa wa masister wa kanisa Kathoriki, ambapo baada ya kupekuliwa amekutwa na baadhi ya vielelezo vilivyobaini kuwa ni tapeli.

Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi baada ya masister wenzie kubaini kama si mmoja wao, kutokana na kushindwa kufanya baadhi ya masuala  ambayo ni msingi wa utawa wao.

Akizungumzia mkasa huo, kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema mwanamke huyo kabila laKe ni Muwembu wa nchini Kenya amekamatwa katika nyumba  za masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.

Aidha Kamuhanda amesema mwanamke huyo ambaye awali aligoma kutoa maelezo ya kina juu ya ujio wake nchini Tanzania, katika upekuzi walimkuta na baadhi ya chip (Line) za makampuni mbalimbali ya simu ya ndani na nje ya nchi.

Kamuhanda amesema Sister huyo bandia alikutwa pia akiwa na hati za kusafiria (Passport) mbili, moja ikiwa niya Africa Mashariki yenye namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa na jumuiya ya Kenya namba A. 1790366.

Amesema Sister huyo feki katika hati hizo ilionyesha kuwa alitembelea nchi ya Rwanda, Uganda pamoja na nchini Tanzania ambapo siku za hivi karibuni alikuwa Mkoani Mara Tarime.

Sister huyo FEKI amekuwa akitumia mbinu ya kujiangusha kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa pindi anapofanyiwa mahojiano, jambo linalowawia vigumu jeshi hilo kupata maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya kuingia humu nchini.

Kamuhanda ameitaka jamii kuwa makini na wageni mbalimbali, huku akiwaasa kuacha tabia ya kuwaamini watu kwa muonekano wao, kutokana na mwanamke huyo kutumia njia hiyo ambayo inamfanya kila mtu kumuamini.

Wema: “Ni kweli picha ni romantic lakini yule kijana (Raheem) si mpenzi wangu. Naomba nieleweke hivyo.”





WEMA ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006, huku akifurukuta kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, ametokelezea na mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Raheem katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

GUMZO MITANDAONI
Picha hiyo ambayo pozi lake ni ‘very romantic’ imezua gumzo katika mitandao mbalimbali ilipotundikwa na wadau wengi walionekana kuamini kuwa Wema alikuwa akimnadi mpenzi wake mpya.
Mtoa maoni mmoja aliandika: “Naona Wema ameamua kutuonesha shem wetu mpya, sasa hapo kazi kwa wenye vijicho.”

Mwingine aliandika: “Mmh! Mbona (Raheem) haonekani uso? Kama lengo lake lilikuwa kumwanika angemuacha tu aonekane ila dah! Ana kifua kizuri sana. Huyu jamaa anaonekana anafanya sana mazoezi.”
DIAMOND ATAJWA

Katika gumzo hilo, wengine walikwenda mbali zaidi, wakisema kwamba inawezekana Wema alikuwa na Raheem kwa siri muda mrefu lakini sasa ameamua kuvunja ukimya ili kumringishia x – boyfriend wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
INTERVIEW NA RAHEEM
Ni jadi ya magazeti ya Global Publishers likiwemo hili la Risasi Mchanganyiko kutafuta mzani wa habari kabla ya kwenda hewani hivyo lilimtafuta Raheem ambaye alitoa ushirikiano wa kutosha.
Raheem alikiri kuitambua picha yake na Wema lakini alisema imemshtua na kumcha-nganya maana hakutegemea kama ingefika mitandaoni na hatimaye kwenye vyombo vya habari.

Alisema: “Ni kweli nilipiga hiyo picha na Wema lakini ni ya kawaida tu, haina maana nyingine tofauti. Wema ni rafiki yangu na dada yangu. Tunaheshimiana, hakuna cha zaidi.

“Wema ni maarufu na watu wanaweza kujaji wanavyotaka, hilo litanisababishia matatizo kwa sababu mimi nina mpenzi wangu na Wema si mtu wangu kabisa…she is just my sister (ni dada yangu tu).”
Risasi: Hiyo picha mlipiga lini, wapi na kwa matumizi gani?Raheem: Ilikuwa kwenye function (tukio) fulani ambayo siwezi kuizungumzia. Kama wiki sita au miezi miwili hivi iliyopita na tulipiga kama marafiki tu, hakuna cha zaidi.
Risasi: Kwa hiyo Wema akithibitisha wewe ni mpenzi wake itakuwaje?Raheem: Nitamshangaa sana! Wema ni dada yangu tu.Risasi: Inasemekana Wema ameamua kuianika hiyo picha kwa lengo la kumrusha roho Diamond, unasemaje hapo?

Raheem: Sijui na kwa kweli siwezi kuzungumzia mambo ya mtu binafsi. Sijui chochote.
Wema alipatikana na kusomewa mashitaka yake ambapo alikiri kupiga picha na Raheem, akafafanua kuwa aliipiga muda mfupi baada ya kutoka kufanya interview na kituo kimoja cha redio (jina kapuni) lakini akasema haina uhusiano wowote na suala la mapenzi.
“Ni kweli nilipiga hiyo picha, yeye aliniomba tu kama fan (shabiki) wangu, akataka ku-show love (kuonesha upendo), sikuona sababu ya kumkatalia. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na Martin (Kadinda – meneja wake) na baada ya siku hiyo sijawahi kuonana naye tena mahali popote…sioni tatizo kabisa, ni kawaida kwa sisi mastaa,” alisema Wema.
Risasi: Lakini Wema wadau wanasema eti ni mpenzi wako na umefanya hivyo kwa lengo la kumrusha roho Diamond.
Wema: Umeshasema wadau, waache na mambo yao lakini maelezo yangu ni hayo na naamini yamejitosheleza.
Risasi: Kuna kitu nahitaji ufafanue zaidi…lile pozi lipo romantic sana, hufikiri kuwa inaweza kuwa sababu ya watu kuwa na hisia kwamba ni mpenzi wako?
Wema: Ni kweli picha ni romantic lakini yule kijana (Raheem) si mpenzi wangu. Naomba nieleweke hivyo. Ahsante

Tuesday, May 14, 2013

MASKINI ANGELINA JOLIE AKATWA MATITI YAKE NA KUONDOA MFUKO WAKE WA UZAZI







 MCHEZAJI wa filamu mashuhuri sana duniani,Angelina Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi.

Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New York Times, Bi Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari kubwa sana ya kupata saratani ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.

Angelina mwenye umri wa miaka 37 na mama na watoto sita, alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.

Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena.

Kulingana na Jolie madaktari walisema kuwa uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi.

''Niliamua kuchukua hatua mwenyewe ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua Saratani hiyo,'' alisema Jolie.

Alisema kuwa shughuli hii ilianza mwezi Februari na kukamilika mwishoni mwa mwezi April.
Katika taarifa iliyoandikwa na Bi Jolie na yenye kichwa, 'Uamuzi wangu wa kimatibabu', Bi Jolie alieleza kuwa mamake alipambana na Saratani kwa miaka kumi na kufariki akiwa na umri wa miaka 56.


Alisema kuwa alielewa fika kuwa siku moja atawahi kuugua Saratani na ndio maana akachukua uamuzi wa kufanyiwa upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji kukatwa matiti.

Uwezekano wake wa kuugua saratani sasa umeshuka kutoka 87% hadi 5%.
Alimsifu mumewe Brad Pitt, kwa kumuunga mkono na kumfariji kwa kila aliyopitia, na kusema kuwa ametulizwa na kuwa wanawe hawakupata lolote katika matokeo ya uchunguzi wa madaktari tangu kufanyiwa upasuaji.


"ninahisi kuwa na nguvu kwa uamuzi niliofanya, na kwa kuwa ninasalia kuwa mwanamke hata baada ya kuondoa viungo hivyo,'' alisema Bi Jolie.

"kwa mwanamke yeyote anayesoma maneno haya, natumai ataweza kujua kuwa wanaweza kufanya uamuzi.''

Muigizaji huyo, ambaye ameshinda tuzo nyingi kwa uigizaji wake, pia ni mtunzi wa filamu na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na harakati za kibinadamu.

Wakati alipokuwa anafanyiwa upasuaji, Bi Jolie alizuru Jamuhuri ya Kidremokrasia ya Congo pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague.

Friday, May 10, 2013

WAENDESHA DALADALA WAGOMA KUSAFIRISHA ABIRIA LEO MJINI IRINGA



 mmoja wa madereva wa daladala akiwatuliza madeveva wenzie
Ofisa  wa  Sumatra  mkoa  wa Iringa Rahim Kondo





usafiri uliotumika leo kubeba abiria

Mgomo  wa  daladala katika Manispaa ya Iringa umeanza asubuhi hii katika eneo la Mwang'ingo mjini Iringa kwa  madereva na   wamiliki   wa  daladala mjini hapa kudai  kuchoshwa na manyanyaso ya afisa mpya  wa SUMATRA mkoa  wa  Iringa.
Habari  ambazo  mtandao huu umezipata zinadai  kuwa hatua ya  mgomo huo  imekuja   kutokana na kuchukizwa  uamuzi  wa Sumatra  mkoa  wa Iringa  kufuta  stendi ya  posta pamoja na  kuzuia daladala  kukaa kwa muda  eneo la stendi ya  daladala  ya Miyomboni maeneo ambayo  kimsingi  walikuwa  wakikaa siku zote. 
Madereva  hao  wamesema  kuwa leo  hawapo   tayari  kufanya kazi hadi  hapo afisa  huyo  wa Sumatra  mkoa  wa Iringa atakapofuta maagizo yake ya  kuzuia stendi hiyo ya  posta na kuruhusu daladala  kukaa muda zaidi  eneo la Miyomboni.

Hali  hiyo  imeanza  kutikisha  na kufanya  polisi  kuingilia kati  kuwatuliza  madereva  wasigome jitihada  zinazoendelea  hadi  sasa.

Hata  hivyo usafiri  unaofanya kazi ni bajaji  ,pikipiki na Taxi ambapo nauli  kwa kichwa katika bajaji  Tsh. 3000 wakati Taxi kwa kila kichwa Tsh 1000

Wednesday, May 8, 2013

Hatimaye Lwakatare afutiwa kesi ya ugaidi!




BREAKING NEWS!
 
 Lwakatare afutiwa Kesi ya Ugaidi!
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

...
Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando, Tundu Lissu, Professor Abdallah Safari, Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

Chanzo Kutoka Mahakamani.

Monday, May 6, 2013

MWANAMKE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI




AMEUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR'

'Majambazi yamempora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi na kutokomea nazo kusikojulikana....
Tukio hilo limetokea jana saa 5:16 jioni na


Inavyosemekana ni kuwa mwanamke huyo alikuwa akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia..
Alipotoka ,majambazi hayo yalimfuata na kuligonga gari lake makusudi na ndipo dada huyo aliposimama ili kuangalia nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa. ..

MILIPUKO KANISANI JIJINI ARUSHA





JESHI  la polisi jijini Arusha limesema linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la ulipuaji lililofanyika katika kanisa la Arusha.

Tukio hilo ambalo limetokea majira ya saa tano asubuhi ya leo tarehe 5 mwezi huu Mei  katika Parokia ya Mpya ya Joseph Mfanyakazi iliyokuwa inafunguliwa rasmi kumetokea mlipuko uliojeruhi watu zaidi ya 25.

Parokia hiyo teule ya orasiti- ya mtakatifu Joseph mfanyakazi Arusha ilikuwa ikifanya uzinduzi mpya, ambapo Kwa mujibu wa taarifa zinazosikika moja kwa moja kupitia Radio Maria, Tanzania, mlipuko huo umetokana na kitu kinasadikika kuwa ni bomu.

Hata  hivyo haijafahamika ikiwa mlipuko huo ulikuwa niwa  bomu la kutegwa ama la kurushwa kwa mkono kutokana na jeshi la polisi kuendelea na uchunguzi wake juu ya mlipuko huo.

Inaripotiwa kuwa wengi wamejeruhiwa miguuni na kulazimika kuwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Hakuna taarifa zozote za kifo zilizoripotiwa katika tukio hilo.

Aidha viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo mwakilishi wa Papa aliyekuwa anatabaruku Kigango hicho kilichozaliwa mwaka 2008 kuwa Parokia, Padre Francisco Padilla na viongozi wa jeshi la polisi na usalama, wanaendelea na kikao ili kuamua hatima ya misa iliyokatizwa.

Hata hivyo kutokana na usalama wa waumini waliokuwemo katika kanisa hilo, wametakiwa kuondoka na hivyo kukatishwa kwa misa na matukio hayo ya uzinduzi.

Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha, akiwemo mkuu wa mkoa, Mbunge wamefika katika eneo hilo, huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi