Pages

Thursday, October 18, 2012

WAKAZI WA MBEYA WAINGIWA NA HOFU BAADA YA NDEGE ZA KIVITA KUPITA KATIKA ANGA LA JIJI LA MBEYA


Ndege kama hii zikiwa mbili zimeonekana kwenye anga la jiji la Mbeya huku zikipita kwa kasi wakazi wa jiji la Mbeya waingiwa na hofu kubwa wakidhani ndio mambo ya Malawi yameivaaaaa............!kutokana na mvutano uliopo wa nchi hizi mbili kuingia kwenye vita ya mpaka wa ziwa nyasa

Meneja wa viwanja vya Ndege Mbeya EZEKIEL MWALUTENDE ameuambia mtandao huu kuwa kinachofanyika sasa ni mazoezi ya ndege kwenye uwanja huo na kusema kuwa pamoja na ndege za kivita pia zipo ndege za abiria 5 ambapo zoezi hilo linatarajia kukamilika Jumanne wiki ijayo.

Ndege ya kwanza kutua katika Uwanja Wa Ndege Wa Kimataifa Wa Songwe mkoani Mbeya Jumapili Julai 22 2012, ilikuwa ndege aina ya Forker 28 ambayo alikuwemo Rais Jakaya Kikwete na msafara wa watu wengine 31.
Uwanja huo ambao aujakamilika na kudaiwa kuwa matengenezo yake yamefikia asilimia 95 tu bado aujaanza kutumika rasmi.
Baada ya kutua kwenye uwanja huo majira ya saa tano na dk 15 , rubani wa ndege hiyo, Kapteni Dominick Boman, akiongozwa na Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mbeya ilipotua, Valentine Kadeha, aliusifia kuwa una sifa zote za kurusha ndege kubwa zinazobeba abiria na kuhoji kwa nini haujaanza kutumika.
“Uwanja ni mzuri sana, sehemu ya kurukia ndege ni pana na uwanja ni mrefu hakika wananchi wana kila sababu ya kuufurahia, sijui kipi kinakwamisha kuanza kutumika kwa abiria labda vituo vya mafuta havijajengwa, suala la sehemu ya kushukia abiria si tatizo; marubani tunahitaji uwanja mzuri,” alisema Bomani.