Pages

Thursday, January 23, 2014

MAHABUSU AJIPAKA KINYESI KWA LENGO LA KUWATOROKA POLISI MKOANI MWANZA

 




 Mahabusu mmoja aliyekuwa mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la jirani na Mamlaka ya maji safi na Hifadhi ya Mazingira (MWAUWASA) jijini Mwanza alitoa kioja cha mwaka kwa kujaribu kutoroka kwa kujipaka kinyesi ili asiguswe wala kukamatwa.

Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikufahamika alijimwagia kinyesi kilichokuwa kwenye ndoo iliyokuwa ndani ya sero ya Mahakamani hapo na askari alipokwenda kufungua ili kuwapeleka watuhumiwa kwenye chumba cha Mahakama kusomewa kesi yake baada ya kutajwa na karani wa Mahakama ya mwanzo, baada ya kutajwa ndipo mahabusu huyo alipopata mwanya wa kukimbia na kutoa tahadhari kwa atakaye mgusa au kumshika atakumbana na kadhia ya kuchafuliwa kwa kupakwa kinyesi.

Askari mwingine mwenye cheo cha sajenti, ambaye alikuwa akihushughulika na huduma nyingine mahakamani hapo, kwa kuwa alikuwa na uzoefu wa kupambana na mikasa na vioja kama hivyo vya mahabusu wanao kula njama za kutaka kutoroka aliamua kula naye sahani moja kwa kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata.


Baada ya kumkamata na kumrejesha katika chumba cha mahabusu mahakamani hapo, kwanza mtuhumiwa huyo aliamriwa kuzoa mtondoro wa kinyesi cha binadamu alichokuwa amejimwagia na kutapakaa chini na mara baada ya kumaliza kuzoa uchafu huo, alipelekwa kwa hakimu ambapo alisomewa kosa la kula njama za kutoroka na kukumbana na adhabu nyingine ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita (6) jela, huku kesi yake iliyokuwa ikimkabili awali ikiahirishwa.
Via Mzee wa matukio