Thursday, March 21, 2013
ALIYEPIGWA RISASI JANA KINONDONI SOMA ZAIDI HAPA
Mpaka sasa hivi sijapata maelezo yoyote kutoka kwa Polisi Kinondoni kuhusu kijana alieuwawa kwa risasi akiwa anaendesha gari dogo kwenye foleni Kinondoni Dar es salaam march 20 2013.
Nafasi hii naitumia kumkariri mmoja wa mashuhuda wa hilo tukio akisema “ni kwenye barabara ya kutoka Magomeni kwenda Mkwajuni hii gari ilikua inashuka, kwa sababu sasa hivi kuna foleni upande wa kulia kuna magari upande wa kushoto kuna magari, pikipiki kama kawaida zikawa zinatanua katikati”
“Wakati pikipiki ya muhusika ilipotanua ghafla ilibidi dereva huyu aliyeuwawa amkwepe hivyo akagonga gari lake kwenye kingo za barabara na kupasua tairi, marehemu akatoka kwenye gari na kukutana na jamaa wa pikipiki wenye asili ya kiarabu wakaanza kubishana na kuwaambia amepasua tairi kwa sababu alikua anawakwepa wao kwa hiyo wamlipe tairi lake tu” – Shuhuda
“Wale waarabu walikua na waya flani kama za shoti, yani zinapiga shoti ndio wakawa wanawapiga kama shoti mwilini.. zikatokea purukushani Mwarabu mmoja akamwambia Marehemu nitakuua,
yule Marehemu akasema huna uwezo wa kuniua wewe… ndio mwarabu akampiga risasi ya shingo na kudondoka palepale na kufariki, majirani ndio wakachukua kanga na kumfunika, mpaka naondoka pale Polisi walikua wamefika kwenye eneo la tukio” – Shuhuda
Bado naendelea kuisubiri kauli ya polisi kuhusu hili tukio, pia nina ahadi ya kukutana na mmoja kati ya vijana waliokua pamoja na marehemu kwenye gari wakitokea gereji… nikiipata wakati wowote nitairipoti hivyo kuwa tu karibu na mimi kwenye
ALIYEUA TRAFFIC DSM AZIDI KUBANWA
Elikiza Nko
Kwa ufupi
‘’Juzi usiku tuliwahoji na mmoja wao alitudanganya, tulipomuuliza dereva wa gari hili ni nani akajibu siyo mimi nimeachiwa na mwenyewe amekimbia” alisema Kamanda Mpinga na kuongeza kuwa baada ya kumbana alikiri kuwa ndiye.
Dar es Salaam. Dereva wa gari lililomgonga na kumuua askari wa usalama barabarani, Elikiza Nko (pichani) atafikishwa kortini wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika, ilielezwa jana.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini(trafiki), Mohammed Mpinga alisema hayo jana alipozungumzia tukio hilo ambalo lilisababisha simanzi kwa watu wengi.
Mpinga alisema polisi walifanikiwa kumkamata mhusika kwa mbinu za kipolisi na kwamba kwa jana alikuwa akihojiwa ili kupata ushahidi utakaowezesha kumpeleka kortini.
Alisema dereva huyo ni kati ya wale wawili waliowakamata awali na hatimaye mmoja walimbaini kuwa ni mhusika .
‘’Juzi usiku tuliwahoji na mmoja wao alitudanganya, tulipomuuliza dereva wa gari hili ni nani akajibu siyo mimi nimeachiwa na mwenyewe amekimbia” alisema Kamanda Mpinga na kuongeza kuwa baada ya kumbana alikiri kuwa ndiye.
Kwa mujibu wa Kamanda Mpinga marehemu ameacha mume na watoto watatu. Maziko yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya Mbweni yaliyopo Manispaa ya Kinondoni na yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.
Marehemu alifariki dunia baada ya kugongwa na gari lililokurupuka kuufuata msafara wa Rais Jakaya Kikwete eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita alipokuwa katika ziara ya kutembelea mkoa huo.
mwananchi
Subscribe to:
Posts (Atom)