mmoja wa madereva wa daladala akiwatuliza madeveva wenzie
Ofisa wa Sumatra mkoa wa Iringa Rahim Kondo
usafiri uliotumika leo kubeba abiria
Mgomo wa daladala katika Manispaa ya Iringa umeanza asubuhi hii katika eneo la Mwang'ingo mjini Iringa kwa madereva na wamiliki wa daladala mjini hapa kudai kuchoshwa na manyanyaso ya afisa mpya wa SUMATRA mkoa wa Iringa.
Habari ambazo mtandao huu umezipata zinadai kuwa hatua ya mgomo huo imekuja kutokana na kuchukizwa uamuzi wa Sumatra mkoa wa Iringa kufuta stendi ya posta pamoja na kuzuia daladala kukaa kwa muda eneo la stendi ya daladala ya Miyomboni maeneo ambayo kimsingi walikuwa wakikaa siku zote.
Madereva hao wamesema kuwa leo hawapo tayari kufanya kazi hadi hapo afisa huyo wa Sumatra mkoa wa Iringa atakapofuta maagizo yake ya kuzuia stendi hiyo ya posta na kuruhusu daladala kukaa muda zaidi eneo la Miyomboni.

Hali hiyo imeanza kutikisha na kufanya polisi kuingilia kati kuwatuliza madereva wasigome jitihada zinazoendelea hadi sasa.
Hata hivyo usafiri unaofanya kazi ni bajaji ,pikipiki na Taxi ambapo nauli kwa kichwa katika bajaji Tsh. 3000 wakati Taxi kwa kila kichwa Tsh 1000