Pages

Friday, May 10, 2013

WAENDESHA DALADALA WAGOMA KUSAFIRISHA ABIRIA LEO MJINI IRINGA



 mmoja wa madereva wa daladala akiwatuliza madeveva wenzie
Ofisa  wa  Sumatra  mkoa  wa Iringa Rahim Kondo





usafiri uliotumika leo kubeba abiria

Mgomo  wa  daladala katika Manispaa ya Iringa umeanza asubuhi hii katika eneo la Mwang'ingo mjini Iringa kwa  madereva na   wamiliki   wa  daladala mjini hapa kudai  kuchoshwa na manyanyaso ya afisa mpya  wa SUMATRA mkoa  wa  Iringa.
Habari  ambazo  mtandao huu umezipata zinadai  kuwa hatua ya  mgomo huo  imekuja   kutokana na kuchukizwa  uamuzi  wa Sumatra  mkoa  wa Iringa  kufuta  stendi ya  posta pamoja na  kuzuia daladala  kukaa kwa muda  eneo la stendi ya  daladala  ya Miyomboni maeneo ambayo  kimsingi  walikuwa  wakikaa siku zote. 
Madereva  hao  wamesema  kuwa leo  hawapo   tayari  kufanya kazi hadi  hapo afisa  huyo  wa Sumatra  mkoa  wa Iringa atakapofuta maagizo yake ya  kuzuia stendi hiyo ya  posta na kuruhusu daladala  kukaa muda zaidi  eneo la Miyomboni.

Hali  hiyo  imeanza  kutikisha  na kufanya  polisi  kuingilia kati  kuwatuliza  madereva  wasigome jitihada  zinazoendelea  hadi  sasa.

Hata  hivyo usafiri  unaofanya kazi ni bajaji  ,pikipiki na Taxi ambapo nauli  kwa kichwa katika bajaji  Tsh. 3000 wakati Taxi kwa kila kichwa Tsh 1000

No comments:

Post a Comment