Pages

Wednesday, June 5, 2013

NIGERIA WAGOMA KUNYWA MAJI YA WAKENYA


 MCHEZO wa soka umetawaliwa na fitna pamoja na mbini chafu ambazo hulenga kumdhoofisha mpinzani hasa kwenye mechi za ugenini ili kutoa faida kwa timu ya  nyumbani kupata ushindi kiwepesi .

Hali hii imedhihirika kwenye maandalizi ya mchezo wa kufuzu kwa kombe la dunia kwa kanda ya Afrika kati ya Nigeria na Kenya ambapo timu ya taifa ya Nigeria imegoma kutumia maji ya kunywa ambayo wamepewa na viongozi wa shirikisho la soka la Kenya ambao kimsingi ni wenyeji wa timu hiyo ya Nigeria .

Kocha wa Mabingwa hao wa Afrika Stephen Keshi alikataa kupokea maboksi 25 ya maji ambayo yaliletwa na kiongozi wa shirikisho la soka la Kenya ambapo alisemakuwa hawahitaji maji hayo na kama wangelazimishwa kuyapokea angewaagiza wachezaji wake wayamwage .

Kitendo hicho kiliwashangaza viongozi wa Fifa waliofika kwenye uwanja wa Kasarani jijini Nairobi ambao walishindwa kuelewa sababu za msingi za kocha huyo kugoma kupokea maji ya kunywa .

Timu ya taifa ya Nigeria inacheza na timu yataifa ya Kenya huko Nairobi baadae hii leo kwenye mchezo muhimu wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2014.

MBATIA AANIKA UOZO WIZARA YA ELIMU:MAKINDA AMTAKA AFUTE KAULI




  • Asema kauli ya vitabu vilivyopo ni sumu kwa taifa inatisha.
  •  Amtaka afute kauli.
Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia, jana aliingia matatani baada ya kutakiwa kutoa maelezo ya kauli yake kuwa vitabu vilivyopo nchini ni sumu kwa Taifa.

Agizo hilo lilitolewa na Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye alisema kuwa maneno yaliyotolewa na Mbatia ni mazito na kama hayatatolewa ufafanuzi yanaweza kuleta madhara makubwa.
Mbatia alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza kufuatia swali lake na msingi ambalo alitaka kujua vitabu vya hisabati kwa shule za sekondari, ambavyo havikuandikwa kwa ubora unaokubalika.

Mbunge huyo pia alihoji wataalamu ambao walipewa kazi ya kupitia vitabu hivyo hawakuweza kubaini udhaifu huo na kama waliuona licha ya kuwa walitumia zaidi ya Sh24.4 bilioni huku Wizara ikidanganya kuwa vitabu hivyo, vilipewa ithibati mwaka 2011 wakati ithibati ilitolewa Oktoba 2010.

“Huu ni uongo tena uongozi mbaya, na ninataka Waziri atuambie hawa waliotoa majibu ya uongo wanachukulia hatua gani pamoja na kutumia Sh24 bilioni, kwa nini wasifukuzwe kazi, hii ni sumu kali kwa Taifa,” alihoji Mbatia.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo alisema kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ilikubaliana na Chuo Kikuu Cha Jimbo la Carolina na Shirika la Usaid kutumia vitabu vilivyoandikwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar.

Alisema kuwa mpango huo ulifuatia ombi la Rais Jakaya Kikwete la mwaka 2009 ambapo aliomba vitabu vya sayansi na Hisabati kutoka Serikali ya Marekani. Alikanusha kuwa hakuna sumu yoyote ambayo wataalamu waliiweka katika mitalaa hiyo kwani waliweza kupitia vizuri na kwamba makosa yaliyobainika hayakuwa makubwa.
hisani ya Brogu ya wananchi

AJALI MBAYA TENA KIWIRA WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA.

 HAPA NDIPO ENEO LINALOTAMBULIKA KAMA UWANJA WA NDEGE AMBAPO KILA MARA AJALI HUTOKEA KWA MAGARI KUFELI BREKI NA KUSHINDWA KUKATA KONA HIVYO KUPITILIZA BONDENI

 MABAKI YA GALI AINA YA SCANIA T669ACU MALI YA KAMPUNI YA LAKE OIL ILIYOKUWA IKITOKEA DSM KUELEKEA KYELA

 HAPA NDIPO WALIPOKUTWA TINGO  ALIYENUSURIKA KIFO AMBAPO DEREVA WAKE NA MWANAE WALIFARIKI PAPO HAPO

 ENEO AMBALO GARI HILO LILISHINDWA KUKUNJA KONA KISHA KUTUMBUKIA KORONGONI

 NASIBU RAMADHANI AMBAYE NI TINGO WA GALI HILO

 MAJERUHI NASIBU RAMADHANI AKIPATA HUDUMA KATIKA HOSPITALI YA TUKUYU KABLA YA KUKIMBIZWA KWENDA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA





POLISI WAKIWA ENEO LA TUKIO



kwa hisani ya mbeya yetu