Pages

Monday, May 6, 2013

MWANAMKE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI




AMEUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR'

'Majambazi yamempora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi na kutokomea nazo kusikojulikana....
Tukio hilo limetokea jana saa 5:16 jioni na


Inavyosemekana ni kuwa mwanamke huyo alikuwa akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia..
Alipotoka ,majambazi hayo yalimfuata na kuligonga gari lake makusudi na ndipo dada huyo aliposimama ili kuangalia nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa. ..

MILIPUKO KANISANI JIJINI ARUSHA





JESHI  la polisi jijini Arusha limesema linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la ulipuaji lililofanyika katika kanisa la Arusha.

Tukio hilo ambalo limetokea majira ya saa tano asubuhi ya leo tarehe 5 mwezi huu Mei  katika Parokia ya Mpya ya Joseph Mfanyakazi iliyokuwa inafunguliwa rasmi kumetokea mlipuko uliojeruhi watu zaidi ya 25.

Parokia hiyo teule ya orasiti- ya mtakatifu Joseph mfanyakazi Arusha ilikuwa ikifanya uzinduzi mpya, ambapo Kwa mujibu wa taarifa zinazosikika moja kwa moja kupitia Radio Maria, Tanzania, mlipuko huo umetokana na kitu kinasadikika kuwa ni bomu.

Hata  hivyo haijafahamika ikiwa mlipuko huo ulikuwa niwa  bomu la kutegwa ama la kurushwa kwa mkono kutokana na jeshi la polisi kuendelea na uchunguzi wake juu ya mlipuko huo.

Inaripotiwa kuwa wengi wamejeruhiwa miguuni na kulazimika kuwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Hakuna taarifa zozote za kifo zilizoripotiwa katika tukio hilo.

Aidha viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo mwakilishi wa Papa aliyekuwa anatabaruku Kigango hicho kilichozaliwa mwaka 2008 kuwa Parokia, Padre Francisco Padilla na viongozi wa jeshi la polisi na usalama, wanaendelea na kikao ili kuamua hatima ya misa iliyokatizwa.

Hata hivyo kutokana na usalama wa waumini waliokuwemo katika kanisa hilo, wametakiwa kuondoka na hivyo kukatishwa kwa misa na matukio hayo ya uzinduzi.

Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha, akiwemo mkuu wa mkoa, Mbunge wamefika katika eneo hilo, huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi