Pages

Monday, July 15, 2013

MAMA AMCHOMA MWANAE MCHANGA MARA 90 KWA MKASI KISA ALIMG'ATA ZIWA WAKATI WA KUNYONYA

Ni kama miujiza kwa mtoto wa kichina kuwa hai mpaka sasa licha ya kuchomwa chomwa mara 90 na mama yake mzazi huko China kwa madai kuwa alimng’ata ziwa mama yake wakati akinyonyeshwa.
Kwa mujibu wa Daily Mail mtoto huyo Xiao Bao mwenye miezi 8 tu ameshonwa zaidi ya nyuzi 100 ili kuurudisha uso wake katika hali nzuri baada ya shambulizi hilo lililotokea katika jiji la Xuzhou mashariki mwa China.


 Bao anaishi na mama yake pamoja na wajomba zake wawili ambao wanajishughulisha na ukusanyaji wa taka kwaajili ya kipato. Mmoja wa wajomba hao ndiye aliyegundua kuwa Bao ameumizwa baada ya kumkuta akiwa amelala kwenye damu iliyotapakaa nyumbani hapo kabla hajamkimbiza hospitali
 Mama wa mtoto huyo baadaye alikiri kumchoma choma mwanae na mkasi mara 90 hususan eneo la usoni baada ya mtoto huyo kumng’ata ziwa wakati akimnyonyesha.
Baada ya tukio hilo majirani wa familia hiyo wameiomba serikali imnyang’anye mama huyo wa kichina mtoto kwa sababu za kiusalama, lakini ombi hilo limekataliwa kwa madai kuwa hakuna uthibitisho wowote mpaka sasa kama mwanamke huyo anamatatizo ya akili, lakini wameongeza kuwa hata hivyo mtoto huyo bado ana walezi wengine wawili anaoishi nao (wajomba zake)
Mtoto huyo anaendelea kupata nafuu akiwa hospitali




USIOMBE VITA! ANGALIA PICHA MBALI ZA ATHARI KWA RAIA KATI YA MAPIGANO YA SERIKALI YA CONGO NA WAASI WA M23

 mama huyu kaka yake ameuliwa na watoto ye 5hajui sehemu walipo ila yeye amekimbilia Uganga na mtoto mmoja akihufia maisha



wa moja wa wakimbizi wakubali kuingia kambini na wengine wakataa kuingia kwa gari za polisi ya Uganfa.
 
wakimbizi kutoka Drc wahamishwa kutoka kwenyi mpaka hadi kilometa 8
 
 wakimbizi wa Drc walio kimbilia Uganda wafanya siku nne bila kupata chakula hadi asubui hii ya leo
 wakimbizi wa Drc wanao patikana Bubandi hapa mpakani mwa Congo na Uganda wakataa kuingia katika kambi ambayo imeandaliwa dhidi yao kilometa 8 na Bundibujo magharibi mwa Uganda





 wakimbizi walio kubali kuingia kambini tayari wameingia kayika kambi ya BUBUKWANGA kilometa 8 kaskazini mwa Bundibujo magharibi mwa Uganda
 gari za polisi ya Uganda wakikimbia na mbuzi zao kutoka mashariki mwa Drc Nobili na kuingia Uganga