Na
Iringa
RAISI wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete jana amefanya uzinduzi wa barabara mpya ya Iringa Dodoma yenye urefu wa kilomita 260 na kuweka jiwe la msingi katika ya kata ya Migori jimbo la Isimani Mkoani Iringa
Alisema kutokana na kuwa na mahusiano mazuri na wafadhili kutoka nchi za nje ujenzi wa barabara hiyo umewezeshwa na mikopo kutoka benki ya serikali ya Japan na benki ya maendeleo ya Afrika pamoja na serikali ya Tanzania.
Kikwete alisema lengo la serikali ni kuunganisha barabara zote zinazounganisha mikoa zenye kiwango cha chini kua na kiwango cha lami na kwamba barabara hiyo ni moja ya barabara kuu za Afrika hivyo kuwepo kwa barabara hiyo kutainua utalii na kukuza uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla
‘’bila shaka serikali imejitahidi kujenga barabara na lengo la serikali ni kuunganisha barabara zote japokua ujenzi wake ni ghali sana lakini pia kuna manufaa makubwa na barabara hii tunatarajia kuimaliza mwaka 2015’’
Alisema barabara ya Iringa Dodoma itawasaidia wananchi wa kusini kwenda mikoa ya kaskazini kwa urahisi ukitofautisha na usumbufu ulikuwepo awali ambapo wananchi walilazimika kipita Chalinze kwenda mikoa ya Arusha
Pia raisi Kikwete alieleza kuwa barabara ya Iringa Dodoma itagharimu kiasi cha Tsh Bilioni 232.2 na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni 1.9 kilitumika kuwalipa fidia baadhi ya wananchi waliokuwa na makazi ndani ya hifadhi ya barabara hiyo.
Hata hivyo Jakaya amewaasa wananchi wanaoizunguka barabara hiyo kuacha kurudisha nyuma shughuri za maendeleo kwa kuiba baadhi vitendea kazi vikiwemo vipuli pamoja na mafuta kwani kwa kufanya hivyo wanarudisha nyuma maendeleo yao wenyewe.
Mbali na hayo raisi Kikwete amewaasa wananchi kuwa makini na gonjwa hatari la Ukimwi kwani uwepo wa barabara hiyo utaongeza idadi kubwa ya watu hivyo kuchukua tahadhari mapema.
‘’Uwepo wa barabara hii utaongeza wingi wa watu na wingi wa magari hivyo nawaasa kua makini kwa kupalamia wageni hovyo kwasababu barabara hii itatumika na watu tofauti kutoka nchi mbali mbali’’Alisema
Nae waziri wa ujenzi Dk John Magufuli alisema wakandalasi watakaozembea katika shughuri nzima ya kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo serikali haitawavumilia na badala yake watafukuzwa
Magufuli amempongeza Mbunge Wa Isimani William Lukuvi kwa uchapa kazi wake na kwamba endapo mbuge huyo angeamua kugombea jimboni kwake basi asingeweza kusimama nae bali angemuachia.
No comments:
Post a Comment