Na Mercy Mwalusamba
Iringa
Kutokana na sakata la mapadre wa Parokia ya Isimani Jimbo Katoliki la
Iringa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, watu
wanne wametiwa mbaroni wakituhumiwa kuhusika na tukiohilo .
Hii inakuja siku moja baada ya mapare wawili wa Parokia hiyo kuvamiwa
nyumbani kwao na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimba za mwili kwa
silaha.
Siku moja kabla ya kuvamiwa mapadre hao watu wasiojulikana walivamia
mlinzi wa Kanisa katika Parokia ya Kihesa na kumjeruhi vibaya na kitu
kizito kichwani ndipo walipovunja milango ya Kanisa na kuiba pesa
kadhaa, baadhi ya vyombo vya ibada na kuharibu vibaya mavazi ya ibada,
vitabu na nyaraka mbalimbali kiasi cha kutotamanika tena.
Miongoni mwa vyombo vya ibada vilivyoharibiwa na watu hao ni pamoja na
Kuvunjwa Msalaba, Monstranti, Taberenakulo ndogo pamoja na kumwagwa
ovyo Hostia Takatifu.
Usiku wa kuamkia juzi watu wanaokadiriwa kufikia saba wakiwa na
bunduki, rungu na mapanga walivamia makazi ya mapadri hao majira ya
saa nne za usiku, ambapo walimpiga nne Padre Angelo Burgio ambaye ni
Paroko wa Parokia hiyo na kumjeruhi vibaya msaidizi wake Pd. Helman
Myala fedha zaidi ya shilingi 3.9 milioni na Euro 100.
Watuhumiwa waliokamatwa kuhisiana na tukiohilo wametajwa kuwa ni
Joseph Ngwale (30), Erasto Ngwale (38), Gaitan Kitwange na Anita
Mwinuka wote wakazi wa Isimani.
Taarifa kutoka kwa wananchi mmoja wa kijiji hicho mshiriki wa msako
huo ambaye alitoa taarifa hizi wa masharti ya kutataka jina lake
liandikwe alisema kuwa ,walianza kupata watuhumiwa baada ya kufanya
upekuzi katika nyumba ya Josepha Ngwale na kupata goroli 37 na gram
100 huku ikipatikana silaha gobore iliyotumika katika ujambazi huo
ambayo kwa usiku huo ililetwa na mwanye Joseph Ngwale ili aifiche.
Tarifa hizo zilithibitishwa na Diwani wa Kata ya Kihorogota
Costantino Kihwele ambaye alisema watuhumiwa wote wamekwisha
kufikishwa polisi ili hatua za kisheria zifuate.
Hata hivyo watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na tukio la uvamizi wa
Kanisa Kuu la kiaskofu Parokia ya Kihesa.
Kaimu wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Gwanchele Faustine alisema baada ya
kumfanyia upasuaji Pd. Angelo waliweza kutoa risasi 3 sehemu ya
kifuani ambazo zilikuwa zimekwama na kueleza kuwa hali zao zinaendelea
kuimarika.
“Jana tulimfanyia upasuaji Pd. Angelo tukaweza kutoa risasi 3 sehemu
ya kifuani ambazo zilikuwa zimekwama. Hali zao zinaendelea kuimarika
huku tukifanya jitihada za kuwahudumia” alisema Dk. Faustine.
Katika hatua nyingine Dk. Faustine alisema kuwa Mlinzi wa Kanisa la
Kihesa Bathlomeo Nzigilwa aliyejeruhiwa na watu hao bado hali yake ni
mbaya japo kuwa kuna dalili za kuweza hata kufumbua macho.
“Mlinzi wa Kanisa la Kihesa aliyejeruhiwa na kuletwa hapa hospitalini
bado hali yake ni mbaya na tumegundua kuwa alivunjika mfupa wa
kichwani kwa hiyo tunaendelea kufanya utaratibu wa kuutoa. Ila kwa leo
amekuwa na dalili za kufumbua macho kwa hiyo tunafanya jitihada za
kumpa huduma zaidi” alisema Dk. Faustine.
…………………………………….. Mwisho ……………………………
Iringa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, watu
wanne wametiwa mbaroni wakituhumiwa kuhusika na tukio
Hii inakuja siku moja baada ya mapare wawili wa Parokia hiyo kuvamiwa
nyumbani kwao na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimba za mwili kwa
silaha.
Siku moja kabla ya kuvamiwa mapadre hao watu wasiojulikana walivamia
mlinzi wa Kanisa katika Parokia ya Kihesa na kumjeruhi vibaya na kitu
kizito kichwani ndipo walipovunja milango ya Kanisa na kuiba pesa
kadhaa, baadhi ya vyombo vya ibada na kuharibu vibaya mavazi ya ibada,
vitabu na nyaraka mbalimbali kiasi cha kutotamanika tena.
Miongoni mwa vyombo vya ibada vilivyoharibiwa na watu hao ni pamoja na
Kuvunjwa Msalaba, Monstranti, Taberenakulo ndogo pamoja na kumwagwa
ovyo Hostia Takatifu.
Usiku wa kuamkia juzi watu wanaokadiriwa kufikia saba wakiwa na
bunduki, rungu na mapanga walivamia makazi ya mapadri hao majira ya
saa nne za usiku, ambapo walimpiga nne Padre Angelo Burgio ambaye ni
Paroko wa Parokia hiyo na kumjeruhi vibaya msaidizi wake Pd. Helman
Myala fedha zaidi ya shilingi 3.9 milioni na Euro 100.
Watuhumiwa waliokamatwa kuhisiana na tukio