Na Mercy Mwalusamba
Iringa
Wanawake waendelea kutupa au kutelekeza watoto Nchini
Utupaji wa watoto hivi sasa umekua kama fasheni kila mahali kumekuwa na kasumba hii ya kutupa watoto mara tu wazaliwapo kana kwamba ni taka ambazo ni kawaida kuzikuta jalalani
Ukatili huo hufanywa mara nyingi na wazazi ambao ama hawana mipango ya kuchukua jukumu la kuwalea watoto hao au kutokana na sababu moja au nyingine, huku wengi wakiokotwa barabarani, kwenye majalala ya taka, vyooni na wengine wakiwa wametelekezwa mahospitalini
Kila binadamu ana haki ya kuishi awe amezaliwa katika hali ya ulemavu wa aina yoyote au awe amezaliwa katika familia duni hivyo ndivyo Mungu alivyopanga hivyo yeye kama binadamu ana haki ya kuishi kama binadamu wengine
Wanawake wanaotupa watoto wamekuwa na visingizio lukuki pindi wanapobainika na makosa hayo na kuhojiwa kusingizia maisha magumu au kusingizia kuzaa mtoto mlemavu kukataliwa na wazazi wenzao wanaowapa mimba japo sababu hii inahusiana sana na suala lenyewe lakini si sawa na si haki kutupa kiumbe kilichoumbwa kwa makusudi ya Mungu
Suala la kutupa watoto kila mtu linamuhusu awe mwanamke ambae ndie muhusika mkuu lakini pia linamuhusu mwanaume kwasababu mtoto hutengenezwa na watu hawa wawili hivyo ushirikiano katika hili unapaswa kuwepo kuanzia kipindi cha ujauzito hadi mtoto anapozaliwa
Japo suala la kukataa kwa mwanaume kua sie muhusika wa mimba ndio limekua limechukua nafasi kubwa lakini sitaki kuamini kwamba ndio sababu kuu ya kumpelekea mwanamke kutupa mtoto
Mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe huna haki kisheria huna haki ki imani wala hakuna utamaduni wa kutupa mtoto kwa kabila lolote unapaswa ujue kwamba Mungu anakushangaa na bina damu wanakushangaa kwa ukatili huo
Wanawake wanaosingizia ugumu wa maisha kwamba maisha yake magumu hana uwezo wa kulea mtoto uamuzi wa mwisho unaoufikia wakuamua kwenda kutupa mtoto jalalani bado hutendi haki wewe una dhambi tu tena kubwa sana
Kuna baadhi ya wanawake wanazeeka hajawahi kubeba hata ujauzito ni stori kwake anatamani hata Mungu amjaalie kupata mtoto taahila ili mradi tu asionekane mgumba wengine wamekula hata vinyesi lakini ameshindwa mwingine lakini wewe unabeba Rambo iliyowekwa mtoto kama taka taka unaenda kutupa jalalani huna tofauti na muuaji
Serikali iangalie adhabu nyingine katika hili ikiwezekana adhabu ibadilishwe na iwe kali zaidi adhabu iliyopo haiogopwi hata kidogo
kuna njia nyingi za uzazi wa mpango na asilimia kubwa ya wanawake wana elimu hii ya uzazi wa mpango kwanini wasichukue hatua ya kuzitumia ukizingatia hazina gharama yoyote kuzipata serikali imetoa bure
Ingekua ni vyema kuzuia mapema kama haupo tayari kwa wakati huo kupata mtoto lakini cha ajabu unalea mimba kwa miezi tisa au chini ya hapo ambapo tayari Mungu kafanya uumbaji wake mtoto anazaliwa unatupa
mapema wiki hii mtoto amekutwa ametupwa maeneo ya M.R amekutwa akiwa amekufa ndani ya mfuko wa kusafiria kabla ya tukio hilo mtoto mwingine aliokotwa karibu na Chuo cha Tumaini University mkoani Iringa wanawake wanaosifika kwa huruma na kuwa walezi wazuri wa familia wenye mapenzi amebadilika na kua kama mnyama
wengine wamekua wakizaa watoto wazima na kuwanyonga kisha kuwatupa hata hofu ya Mungu haipo kabisa kwao hakuna imani ya dini yoyote inayoruhusu ukatili wa namna hii labda dini ya mashetani
Na hili limekua ni chanzo cha watoto wa mitaani kwasababu baadhi yao akija kugundua ukweli wa maisha yake anashindwa kujikubali na kuadhirika kisaikolojia na huishia mitaani
imefika wakati sasa wanawake watambue umuhimu na haki ya mtoto ya kuishi kwani wanawake wamekuwa wakibeba ujauzito na kisha kutoa mimba huku wanawake wengine wakitupa watoto wachanga pindi wanapojifungua
Wanawake waepukane na mimba zisizotarajiwa hii itasaidia kupunguza tatizo la watoto wachanga kutupwa au kunyongwa pindi wazaliwapo
Ikishindikana wafuate uzazi wa mpango hospitali inatoa huduma bure na siyo kutupa mtoto ambaye umemlea kwa miezi 9 tumboni leo hii mama anajifungua na kutupa mtoto huo ni ukatili wa hali ya juu kwa mtoto asiye na hata chembe ya hatia
..........................................MWISHO...............................................................
KICHANGA KILICHOTUPWA PEMBENI MWA MTO KARIBU NA CHUO KIKUU TUMAINI IRINGA