Pages

Monday, June 24, 2013

SIO WANAUME TU WANAOWEZA KUOA WANAWAKE 2 HATA WANAWAKE WANAWEZA KUOLEWA NA WANAUME 2;HUYU NI MWANAMKE ALIYEOLEWA NA WANAUME 2 NA ANAISHI NAO BILA MATATIZO

Veronika akiwa na waume zake

MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.

Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.

Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji iitwayo kayoga.

Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.

Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.

“Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi.

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.

Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.

Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.

Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.

Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.

“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulia nguo.

“Ndivyo wanavyoishi, nasi sasa tumewazoea ila yule mama ni mkali na ana sauti pale kwake kwa wanaume wale ila tunaona kama ana wivu sana kwa huyu mdogo ambaye naye pia ana wivu kwa mkewe huyo, labda anahofia kuwa mama huyo anaweza kuongeza mwanamume mwingine,” anasema mmoja wa majirani hao.

Hakuna mazuri yasiyokuwa na machungu, japo familia hiyo inaelezwa kuwa na amani, mtoto wao mdogo nusura avuruge uhusiano wa wanandoa hao, baada ya kuibuka mzozo wakati wa maandalizi ya ubatizo wake.

Kwa sababu anazojua mama, ingawa inafahamika kuwa wote ni watoto wa mume mkubwa, mke huyo katika hati za ubatizo aliandikisha ubini wa mtoto huyo kuwa ni Mlele (akimaanisha kuwa mtoto wa mume mdogo), lakini mume mkubwa aliweka pingamizi kanisani akidai yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, yeye na Arcado ni waumini wa madhehebu ya Katoliki wakati Paulo ni Mpentekoste. Madai ya mzozo wa uhalali wa `ubaba’ wa mtoto huyo, yalithibitishwa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, akiwamo mwalimu wa dini wa Kigango cha Kanisa Katoliki Uruira, Mashaka Abel. Walisema miaka sita iliyopita, mtoto huyo akiwa na umri wa mwaka mmoja, alifanyiwa taratibu za ubatizo, lakini ilishindikana, kutokana na wanaume hao, kila mmoja kudai ndiye baba mzazi wa mtoto.

“Lilikuwa jambo la kustaajabisha sana, kwani familia hiyo ilifanya maandalizi yote ya sherehe ya ubatizo wa mtoto huyo, lakini siku hiyo kanisani wakati huo ilikuwa ni kigango cha Katumba ambacho sasa ni Uruira, sakata lilianzia pale Padri alipomwuliza mama wa mtoto huyo ubini wa mtoto naye akasema ni Mlele.

“Hapo ndipo mume mkubwa alipopinga na kudai kuwa mtoto yule si wa Arcado bali wake na yeye ndiye baba halali. Padri hakuamini, aliuliza tena na tena na majibu yakawa ni yale yale, ndipo ubatizo ukashindikana,” alisema Katekista Abel.

Kazi ya kutafuta undani wa ndoa hiyo haikuwa rahisi kutokana na mazingira ya woga na usiri uliokusudiwa kubaki, ambapo awali mama alisema kwamba mume wake ni Paulo pekee japo siku ambayo mwandishi wa habari hizi alifika kijijini hapo na baadaye nyumbani kwa wanandoa hao na kumkuta mume mdogo (Arcado akimsaidia mkewe kukoroga pombe. Awali katika utambulisho, walidai kuwa ni mtu na mdogo wake na kusita kuzungumzia maisha yao ya kifamilia.

Mke wao ambaye alionekana wazi kuwa ni msemaji mkuu alifoka na kuja juu, akidai kuwa hayuko tayari kuzungumzia uhusiano wake na wanaume hao wawili, ingawa alikiri kuwa wanaishi pamoja.

"Kwa hiyo umefunga safari yote hii kutoka huko ulikotoka ili uje kwangu mie Veronica … nasema sitaki kabisa mtu kuja hapa na kutaka kunivurugia mpangilio wa maisha yangu, kwanza nani alikueleza hayo, wambea wakubwa hao yanawahusu nini watu hao?” alihoji.

“Mie mume wangu ni huyu Paulo basi … sasa leo umeniachia vurugu ndani ya nyumba nitapigwa na huyo mume wangu Paulo, kwani mmenishikisha ugoni?” alifoka Mama Kaela. Hata hivyo, mume mkubwa alidai kuwa hatamwadhibu mkewe huyo na kwamba wataendelea kuishi pamoja na mdogo wake Arcado kwa amani. Hata hivyo, akina mama wengi kijijini hapo wanalaani kitendo cha mama huyo kuishi na wanaume wawili ambapo waliomba uongozi wa Kanisa uingilie kati, ili mama huyo aweze kufunga ndoa na mume mmoja.

Lakini kwa upande mwingine, baadhi walimpongeza mwanamke huyo wakidai kuwa kitendo hicho ni cha kijasiri kwa mwanamke, kumudu kuishi na wanaume wawili na kuwa na mamlaka juu yao.

via Hi5 

ASKARI WA JESHI LA POLISI AFANYA KITENDO CHA UNYAMA KWA MKEWE NA KISHA KUTOWEKA ....




 Hapa akionyesha majeraha ambayo aliyapata shingoni kutokana na kukabwa shingo na askari huyo

 Hapa akiwa hoi kwa kipigo

 

WAKATI jeshi la polisi nchini likiendelea kujiweka karibu na Raia hata kuamua kuanzisha dawati la jinsia katika vituo vya polisi ,kwa mkoa wa Iringa baadhi ya askari wanadaiwa kupiganga na jitihada hizo za polisi kwa kushindwa kuheshimu dawati hilo na badala yake kushiriki kulivunjia heshima jeshi hilo kutokana na kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na mkakati wa jeshi hilo katika kuanzisha dawa.ti la jinsia.

Uchunguzi wa mtandao huu wa www.matukiodaima.com na www.francisgodwin.blogspot.com umeonyesha kuwa dawati hilo kwa askari limekosa kuheshimika kutokana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ambavyo baadhi ya askari (30) wamekuwa wakifanya kwa watoto wao na wake zao.

Rehema Shauri Madongo ni mmoja kati ya mwanamke ambaye amebahatika kuolewa na askari polisi kitendo cha upelelezi ambaye anaeleza jinsi alivyotendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuteswa na kupigwa kikatili na pindi anapofika polisi hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni askari .

" Mimi niliolewa kwa ndoa na Stephen Kanyala ambae ni askari kitengo cha upelelezi ila baada ya kuolewa ukiwa umepita mwezi mmoja tuo nilianza kushuhudia mateso ya ndoa kutokana na kipigo na mateso makali niliyokuwa nikiyapata"

Anasema kuwa kila wakati pindi anapotaka kujua jambo kutokana kwa mume wake huyo hasa pale anapoona jumbe zenye utata katika simu yake ambazo zimetoka kwa wanawake anaiowatambua vizuri amekuwa akijibiwa kwa kipigo kikali.

Rehema alisema kuwa ni rahisi kwake kuweza kuhesabia siku ambazo hajapigwa kuliko kuhesabi siku ambazo amepigwa ambazo ni nyigi zaidi .

Kwa alisema toka ameolewa kila mara amekuwa akipokea kipigo na mbaya zaidi kabla ya kupigwa amekuwa akifungwa mikono kwa pingu zinazotumika kuwafunga watuhumiwa pingu ambazo mume wake huyo amekuwa akizihifadhi ndani ya nyumba .

" Kweli inasikitisha sana kusimulia kwani kabla ya kupigwa nimekuwa nikifungwa pingu mikono kama mharifu sugu na baada ya hapo kipigo kikali kimekuwa kikinikuta ....hadi sasa nimepigwa zaidi ya mara 20 na polisi nimekwenda kuripoti mara tatu na Hospital nimelazwa mara moja ila siku nyingine nimekuwa nikiugulia nyumbani ila nyumbani kwa wazazi nimerudi mara tatu sasa"

Alisema kuwa mbali ya kupigwa na kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi kuelezwa hapa kutokana na jinsi ambavyo askari huyo anavyomtenda ukatili wa kinyama.

Hata hivyo alisema kuwa akiwa na mimba ya mwezi mmoja hali ya kipigo ilizidi zaidi na wakati mwingine alipata kumfunga shingo na kanga kwa kutaka kunyonga shingo huku akitishi kumuua .

Alisema kuwa baada ya kujifungua mtoto wa njia ya Oparesheni mwanaume huyo alimpiga kiasi cha kumjeruhi mtoto wa mwezi mmoja kwa kumpiga kofi ambalo lilielekezwa kwake na bahati mbaya likaishia kwa mtoto.

Aidha alisema kuwa kila akifika polisi kufungua kesi hakuna utekelezaji unaofanyika kutokana na polisi kulindana na kuwa suala hilo la askari polisi kulindani lilianza toka wakati kamanda wa polisi akiwa Evarist Mangala ,pia alipofika kamanda Michael Kamuhanda ambaye kwa sasa amehamishwa baada ya cheo kupanda pia amepata kufikisha malalamiko yake ila hakuna jipya ila sasa amefikisha tena suala hilo kwa kamanda mpya RPC Ramadhan Mungi ambae amedai kuwa na imani nae zaidi katika kulishughulikia suala lake

Pia alisema mbali ya kupigwa akiwa nyumbani kwake ila bado anapoamua kukimbia nyumba hiyo na kukimbilia kwa wazazi wake bado askari huyo amekuwa akimfuata na kumpa kipigo mbele ya wazazi wake .

Hivyo alisema katika kunusuru uhai wake kwa sasa ameamua kurudi kwa wazazi wake na suala la ndoa hataki tena .

Kwa upande wake Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri alisema kuwa amechoka kuuguza binti yake kwa kipigo na kuwa kuna wakati mwanaume huyo amekuwa akitishia kumpiga hata yeye.

Hivyo alisema kwa sasa mbali ya kumtoa binti yake Hospital ila wamekuwa wakiishi ndani wamejifungia milango kuogopa askari huyo kuja kuwafanyia ukatili ikiwa ni pamoja na kuwaua kwa risasi kama ambavyo amekuwa akiwatisha mara kwa mara kuwa dawa yao inachemka na ipo siku wataonja mauti.

Bi Shauri alisema mbali ya kuwa yeye ni mmoja wa wacha Mungu kwa maana na Mlokole mzuri ambae kila wakati asubuhi lazima aende kusali ila kwa sasa anaogopa kutoka asubuhi kwa kuhofia kuvamiwa na askari huyo .

Hivyo aliomba jeshi la polisi kuweza kumpa ulinzi yeye na familia yake ama kumkamata mtuhumiwa huyo ambae inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa Iringa ila askari wenzake wanamlinda.

Kuhusu uamuzi wa binti yake wa kuomba ndoa hiyo kuvunjwa alisema anaungana na binti yake kuikataa ndoa hiyo na kuwa kwa sasa wapo tayari kurudisha mahali yake ya Tsh 200,000 ambazo alizitoa kama mahali ili kunusuru uhai wao na uhai wa mtoto wake huyo.

..................Itaendelea ..........
via Demasho