JESHI la polisi jijini Arusha limesema linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la ulipuaji lililofanyika katika kanisa la Arusha.
Tukio hilo ambalo limetokea majira ya saa tano asubuhi ya leo tarehe 5 mwezi huu Mei katika Parokia ya Mpya ya Joseph Mfanyakazi iliyokuwa inafunguliwa rasmi kumetokea mlipuko uliojeruhi watu zaidi ya 25.
Parokia hiyo teule ya orasiti- ya mtakatifu Joseph mfanyakazi Arusha ilikuwa ikifanya uzinduzi mpya, ambapo Kwa mujibu wa taarifa zinazosikika moja kwa moja kupitia Radio Maria, Tanzania, mlipuko huo umetokana na kitu kinasadikika kuwa ni bomu.
Hata hivyo haijafahamika ikiwa mlipuko huo ulikuwa niwa bomu la kutegwa ama la kurushwa kwa mkono kutokana na jeshi la polisi kuendelea na uchunguzi wake juu ya mlipuko huo.
Inaripotiwa kuwa wengi wamejeruhiwa miguuni na kulazimika kuwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Hakuna taarifa zozote za kifo zilizoripotiwa katika tukio hilo.
Aidha viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo mwakilishi wa Papa aliyekuwa anatabaruku Kigango hicho kilichozaliwa mwaka 2008 kuwa Parokia, Padre Francisco Padilla na viongozi wa jeshi la polisi na usalama, wanaendelea na kikao ili kuamua hatima ya misa iliyokatizwa.
Hata hivyo kutokana na usalama wa waumini waliokuwemo katika kanisa hilo, wametakiwa kuondoka na hivyo kukatishwa kwa misa na matukio hayo ya uzinduzi.

Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha, akiwemo mkuu wa mkoa, Mbunge wamefika katika eneo hilo, huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi
No comments:
Post a Comment