Pages

Tuesday, June 4, 2013

MAJAMBAZI YAUA NA KUJERUHI NA KUIBA PESA ZAIDI YA MILIONI 2. IRINGA

Wakazi wa Zizi la Ng'ombe mjini Iringa  wakiwa kando ya gari ambalo marehemu  alijificha  chini ya uvungu baada ya  kupigwa risasi na majambazi hao 


Hapa penye damu ndipo alipopigwa  risasi 


Mwili  wa marehemu huyo aliyetambulika kwa jina la baba  Daudi  ukiwa katika  gari la polisi

 Askari  polisi  wakiushusha mwili  huo tayari kuuhifadhi  chumba cha maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa  wa Iringa

Jeraha  ambalo kijana Patrick Vatung'a alilokwanguliwa kwa  risasi 



 
WAKATI  kikao  cha  wadau  wa ulinzi kinataraji  kufanyika kesho jumanne mkoani Iringa katika  ukumbi wa Siasa ni kilimo kikao  kinacholenga  kupambana na mtandao  wa uharifu  mkoa ya  kusini mwa Tanzania ,

Watu  wanaosadikika  kuwa ni majambazi   wakiwa na  silaha  wamevamia maduka  eneo la Zizi la Ng'ombe jirani na msikini mjini Iringa na kuua mtu mmoja na  kujeruhi wengine  wawili kwa  risasi kabla ya  kupora  fedha  kiasi cha  zaidi ya shilingi milioni 2 .

Mashuhuda wa  tukio  hilo  wameueleza mtandao huu  kua baada ya kufika  eneo la tukio kuwa  majambazi hao  wakiwa zaidi ya  wawili   walivamia eneo hilo muda wa saa 1.30  usiku wa  leo .

Mashuhuda hao walisema  kuwa  majambazi hao  baada ya  kufika katika  eneo hilo la kibanda cha M-Pesa  kinachomilikiwa na Zamoyoni na  kufanikiwa  kumpora  kiasi hicho cha  fedha kabla ya  kuelekea katika  duka moja  wapo maarufu  eneo hilo kwa lengo la  kuvamia na kupora.

Alisema Kevin Kalinga  kuwa chanzo cha  kuuwawa kwa  mwananchi huyo aliyetambuliwa kwa jina la baba Daudi ni kutokana na kugoma  kutii amri ya  majambazi hao  ambao walimkuta akitoka  dukani  kununu sigara na  kumtaka  kukaa chini na baada ya marehemu huyo kugoma  kukaa chini ndipo walipomfyatulia risasi mwili  jirani na pega na kupelekea  kutimua  mbio na kujificha chini ya gari  lililokuwa limeegeshwa   nje ya duka hilo gari aina ya Toyota Hilux lenye namba  T 258 .

Hata  hivyo  baada ya  kupigwa  risasi kwa  mwananchi huyo wananchi  waliokuwa karibu na eneo hilo  walianza kujikusanya kwa  lengo la  kuwavaa majambazi hao hali  iliyopelekea  majambazi hao  kuanza  kufyatua  risasi  ovyo na  kujeruhi  wananchi  waliokuwa karibu na eneo hilo.

Kwa  upande  wao majeruhi  wa tukio hilo ambao  wamelazwa  wodi namba  5 katika  Hospitali ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa Dismas Nyaulingo ( 20) na Patrick Vatung'a(19)  walisema  kuwa wao  walikuwa wakiendelea  kucheza  Pool  eneo hilo na baada ya  kusikia mlio kama  wa baruti walianza  kujihami kwa kukimbia na ndipo  walipokutwa na mkasa  huo .


Nyaulingo  alisema chanzo cha majambazi hao  kuanza  kufyatua  risasi onyo ovyo ni baada ya  wananchi  kuanza  kujikusanya kwa  lengo la kupambana na  majambazi  hao .

"Sisi  tulikuwa tukicheza mchezo  wa  Pool eneo hilo na baada ya hapo tulisikia mlio wa risasi  hewani na tukajua ni baruti na baada ya kusikia mlio wa  pili ndipo  tulipoanza  kutimua mbio kabla ya  kupigwa  risasi "

Nyaulingo  yeye amedai kujeruhiwa  eneo la paja  lake la mguu  wa  kushoto huku mwenzake Vatung'a akijeruhiwa  eneo la paja  la mguu wa  kulia.

Madaktari  waliowatibu majeruhi hao  wamedai kuwa hali  zao  zinaendelea  vizuri na uwezekano wa kupona ni mkubwa  zaidi.

Tukio  hili  limetokea ikiwa ni  siku chache  baada ya Rais Jakaya  Kikwete  kumpandisha  cheo aliyekuwa kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa (RPC) Michael Kamuhanda ambae  kutokana na kupanda  kwake kwa cheo wakati  wowote  kuanzia wiki  hii atauaga rasmi  mkoa wa Iringa na kwenda kuanza maisha mapya  katika kiti  cha enzi mpya. 
 

No comments:

Post a Comment