Pages

Thursday, May 15, 2014

MWANDISHI WA HABARI AUWAWA HUKO AFRICA YA KATI

Mwandishi huyu wa habari ameuwawa huko Africa ya kati na watu ambao hadi sasa hawajulikani ila Ufarasa imenza Uchunguzi wa makini,
huyu ni muandishi wa 3 kuuliwa africa ya kati muandishi wa kwanza wa kigeni kuuliwa .

MTOTO WA MIAKA MIWILI AFARIKI BAADA YA KUUNGUA NA MOTO AKIWA NDANI YA NYUMBA YAO



Na Mercy Mwalusamba 

Iringa



MTOTO Christian Kipeto (2)  Mkazi wa Mafuruto kata ya Mlandege manispaa ya Iringa amefariki dunia baada ya kuungua na moto uliosababishwa na mshumaa

Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa moja na  nusu jioni ambapo moto wa mshumaa uliokua ukiwaka ndani ya nyumba hiyo 

ulindondokea kwenye mito ya makochi na hivyo kuanza kusambaa taratibu na kumuunguza mtoto huyo kwenye mguu wake wa kushoto na kuepelekea kifo chake.
 
Katika tukio lingine wafanyabiashara wawili wilayani  Mufindi katika kijiji cha Sawala  tarafa ya Ifwagi mkoani Iringa  wameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuiba msumeno wa kupasulia mbao pamoja na puli yake uliokuwa unamilikiwa na Joseph Kandege .

Kamanda wa polisi Mkoani Iringa Ramadhani Mungi amethibitisha kuawa kwa wafanyabiasha hao  jana majira ya saa moja usiku ambapo mmoja alifahamika kwa jina moja la George na mwingine kwa jina Edwin Lyavule wote wakiwa ni wafabiashara wa Mafinga

Mungi alisema katika tukio hilo watuhumiwa wengine watano ambao majina yao yamehifadhiwa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano Zaidi


Mwisho………………….

Monday, May 12, 2014

MAAJABU!!! Je ulijua kama Kondo la Nyuma au 'Placenta' huliwa?


 Hugeuka kuwa uchafu pindi mama anapojifungua , sasa kwa nini baadhi ya wanawake wanaamua kula Kondo la nyuma au Placenta ikiwa mbichi ?
Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa kutoka kwa mama akiwa tumboni.
Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa , lakini sio kila mtu ana mtazamo huu.
Baadhi ya wanawake wanaamini kuwa madini yanayopitia kwa mkondo wa Nyuma hadi kwa mtoto ili kumuwezesha mtoto kukuwa huwa bado yanaweza kutumika na kwamba sio vizuri kuitupa.

Njia za kula Kondo la Nyuma

  • Husagwa na kuwa majimaji kama Sharbati vile
  • Inaweza kukaushwa na kutengezwa kama tembe
  • Kupikwa kwa kukaangwa kama vile nyama
Wanasema kuwa mama bado anaweza kupata madini muhimu wakati anapoendelea kupata nafuu baada ya kujifungua na pia anapoanza kuonyonyesha kwa kula Kondo la nyuma.
'Mama ale Kondo la Nyuma?'
Baadhi ya wanawake husaga kondo hilo na kunywa maji yake saa chache tu baada ya kujifungua, baadhi wanaihifadhi na kutengeza tembe ambazo wanameza na wengine wanaikata vipande vipande kwa kuweka chini ya ndimi zao.
Wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa tembe hizo zinaweza kuwapa nguvu na pia kusaidia maziwa ya mama kuongezeka.
Kampuni moja nchini Uingereza inayotengeza biadhaa mbali mbali kutoka kwa Kondo la Nyuma, hulipisha watu kati ya pauni 150 au dola elfu kumi na saba kwa kila tembe na chini ya dola hamsini kwa maji ya kondo hilo linaposagwa.




 Baadhi hutengeza maji ya sharubati kwa kuichanganya na matunda
Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa na madini mengi ambayo hayapaswi kutupwa tu.
Lakini kampuni hiyo inakumbwa na kesi mahakamani ambayo huenda ikaisababisha kufungwa.
Kampuni hiyo ilishitakiwa na wataalamu wanaohofia kuwa bidhaa hizo zinaweza kuwa na Bakteria ambayo inaweza kusababisha athari za kiafya kwa wanaotumia bidhaa zinazotokana na kondo la nyuma.
Charlie Poulter, kutoka mtaa wa Reading, anaamini kuwa alipokunywa maji ya kondo la Nyuma pindi baada ya kujifungua ilimwezesha kupata nguvu.
"nilikunywa harakaharaka, kwa sababu sikutaka kutafakari kuhusu harufu na ladha yake, alisema Charlie''
"nilikuwa nimejifungua na nilihisi kuishiwa na nguvu sana na pia kwa kiasi kidogo nilijidharamau. Kwa hivyo nilihisi kuwa ikiwa nitakunywa maji hayo ingenisaidia kupata nguvu na kupona haraka,'' alisema mama Charlie.
'Kondo la Nyuma ni nini?'


Baadhi ya wanawake huikausha na kuikaanga kama nyama
Hii huwa ni kiongo cha mwili ambacho huwa kimeshikana na nyumba ya mtoto pamoja na kitovu.
Kiungo hicho hubeba hewa ya Oxygen na madini kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Pia husafirisha uchafu kutoka kwa mtoto hupitia kwa kiungo hicho hadi kwa mama.
Baada ya mtoto kuzaliwa kiungo hicho hutoka mwilini mwa mama anaposukuma mtoto au hutolewa na madaktari mama anapofanyiwa upasuaji.
Binadamu kwa kawaida hajulikani kwa kula sehemu hiyo ya uzazi. Ni kawaida kwa baadhi ya wanyama wa baharini na wanyama wengine wa kufugwa. Lakini kwa mwanmadamu , bila shaka ni jambo geni.
Nchini China baadhi ya madaktari wa kienyeji hutumia sehemu hiyo ya mwili kutengeza dawa za kienyeji lakini utamaduni huu wa watu kula Kondo la Nyuma umeanza tu kusikika katika mataifa ya magharibi.
'Je wanasayansi wanasemaje?'
Hadi leo hakuna utafiti wowote kisayansi kuhusu wanawake wanaokula Kondo la Nyuma.



CHRIS BROWN AENDELEA KUBAKI JELA


 
Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown ataendelea kutumikia kifungo chake kwa siku nyingine 131 baada ya kukiri kukiuka amri ya mahakama kuhusu kifungo cha nje alichokuwa amepewa na mahakama.

Muimbaji huyo maarufu wa muziki wa  R&B alikiri mahakamani mjini Los Angeles mnamo siku ya Ijumaa kuwa alitenda uhalifu mjini Washington Oktoba mwaka jana.
Jaji alimuhukumu kifungo cha siku 365 jela ingawa alimpongeza kwa kuhudumia siku 234 katika kituo cha kupata ushauri nasaha.
Brown amekuwa chini ya aungalizi wa mahakama tangu mwaka 2009 alipokiri kumpiga mwanamuziki mwenzake na ambaye alikuwa mpenzi wake wakati huo, Rihanna.

Mshindi huyo wa tuzo la Grammy amekuwa kizuizini tangu mwezi Machi alipokamatwa kwa kukiuka amri ya mahakama iliyomweka ndani ya kituo cha ushauri nasaha pamoja na jela.
Kifungo alichopata kuongezewa siku kinahusiana na kisa cha ugomvi kilichotokea mjini DC mwaka jana.

Brown anakabiliwa na mashitaka ya kumchapa mwanamume mmoja nje ya hoteli moja mjini Washington

Tuesday, March 18, 2014

WACHIMBAJI WADOGO WANANE WANADHANIWA KUFA KATIKA MACHIMBO YA NYANGALATA NA KALOLE WILAYANI KAHAMA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI.

  Baadhi ya Wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Kalole wakihangaika kuwatoa wenzao wanane wanao daiwa kufariki dunia kwa kufukiwa na kifusi ndani ya shimo hilo.
 Wachimbaji wakiaangalia sehemu walipofukiwa wenzao wakati wakichimba Dhahabu katika machimbo hayo madogo ya Kalole Wilayani Kahama.

Mjiolojia kutoa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Wilyani Kahama Bw. Amir Chande akitoa maelekezo juu ya kufungwa kwa machimbo hayo baada ya maafa hayo kutokea

 Mmoja wa Wachimbaiji katika Mgodi wa Kalole akiwa katika jitihada za kuwafukuwa wenzao wanaodaiwa kufukiwa katika machimbo hayo juzi

Majeruhi ambaye alisalimika katika tukio hilo akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama akipatiwa Matibabu


via WANG BLOG

BABU SEYA, PAPII MENO NJE WAKILI WAO ANASA USHAHIDI WA KUWATOA GEREZANI




MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ anayetumikia kifungo cha maisha jela na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa kuwanajisi watoto tisa, wana furaha upya baada ya mwanga wa kuweza kurudi uraiani kuchomoza tena, wakili wao, Mabere Nyaucho Marando amezungumza na Uwazi.

KASORO HUKUMU YA MWANZO Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Marando alisema kwamba katika kesi ya Babu Seya na mwanaye iliyosikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar aligundua kuna vielelezo muhimu ambavyo havikuambatanishwa hivyo kuwa vigumu kwake kuviingiza na kuvitetea katika ngazi ya mahakama ya rufaa iliyoshindilia adhabu dhidi ya wawili hao.

Marando alisema mwanga mwingine wa kupitiwa upya wa mashitaka yao umekuja baada ya kuwepo kwa kesi mpya inayofanana na ya akina Babu Seya kwa asilimia mia moja. Alisema kesi hiyo ipo kwenye hatua ya mwisho ambapo ushindi wake utamfanya apate nguvu ya kurudi mahakamani kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa mwaka 2004.

DIRA KWENYE KESI HIYO “Kuna kesi mahakama kuu kanda moja nchini inayotetewa na wakili maarufu (jina tunalo). Hii kesi inafanana sana na ya akina Babu Seya. Uzuri wake ina dalili zote za washtakiwa kuibuka na ushindi wa kishindo. MAHOJIANO Mazungumzo kati ya Marando na Uwazi yalikuwa hivi:

Uwazi: Lakini mheshimiwa kesi ya Babu Seya si ilifika katika rufaa mara tatu na wakashindwa na ulisema hakuna namna tena, sasa itakuwaje kurejeshwa tena huko? Marando: Ni kweli, lakini ni jambo linalowezekana.

Nimesema kama hiyo kesi ninayoitaja watashinda na wanaweza kushinda, basi mimi nitaenda kwa Nguza na kumwambia wazo langu, akikubali nitaiandikia barua mahakama ya rufaa kuomba kupitiwa tena kwa yale mashitaka, nitajenga hoja.

Uwazi: Hiyo kesi unayoingoja hukumu yake inahusu nini? Marando: Inahusu kubaka na kulawiti, ni kama hii ya Babu Seya na wanawe. Hakuna tofauti. Sasa washitakiwa wale wakishinda ndipo hoja inapokuja, kwa nini vipengele vilevile viwatie hatiani akina Babu Seya wengine viwaweke huru, ndivyo inavyokuwa katika kesi. Uwazi: Ukiwaandikia mahakama ya rufaa wakakubali, majaji walewale watasikiliza ombi lako?

Marando: Hilo ni la mahakama lakini idadi inaweza kuongezwa na kufikia majaji sita au saba.Uwazi: Una hakika utashinda na kukubaliwa? Marando: Kama nilivyokueleza, ikipita ile kesi halafu mahakama ya rufaa wakakubali kupitia tena jalada, nina uhakika wa kushinda.

ANALIPWA NA NANI? Wakili huyo maarufu alisema yeye aliwatetea wanamuziki hao bure kwenye kesi yao ikiwa katika ngazi ya mahakama ya rufaa baada ya kusoma jalada lenye kurasa 1,362 ambapo aligundua kuwa kuna nyaraka kadhaa ambazo hazikuambatanishwa katika Mahakama ya Kisutu ambazo zingeweza kuwaokoa na kifungo wateja wake.

“Unajua kesi inapokuwa mahakama ya rufaa, majaji wanachofanya ni kupitia jalada si kusikiliza, hivyo haiwezekani kuambatanisha vielelezo vipya,” alisema Marando ambaye anajipambanua kuwa awali alishinda nusu kwa kuwatoa nje watoto wa Babu Seya, Mbangu na Francis Nguza ambao nao walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa moja na wafungwa hao.

HUKO NYUMA Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Addy Lyamuya aliwatia hatiani kwa ubakaji na ulawiti Babu Seya na wanawe Papii Kocha, Mbangu na Francis. Januari 27, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu hiyo.

Wakili Marando akapeleka suala hilo Mahakama ya Rufaa Tanzania ambako Mbangu na Francis waliachiwa huru na yeye kutangaza kwamba ameshinda nusu. Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka na kulawiti watoto hao kati ya Aprili na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza ya Kwaremmy, Dar es Salaam.
GPL