Pages

Tuesday, December 10, 2013

WOSIA WA MANDELA WAZUA MJADALA MZITO....!!


Marehemu Nelson Mandela enzi za uhai wake.
Mwandishi Wetu na Mitandao
WOSIA aliowahi kuuandika hayati Nelson Rolihlahla Mandela ‘Mzee Madiba’ au ‘Tata’ (95) enzi za uhai wake akielezea anavyotaka azikwe, ndiyo tishio kubwa lenye utata kuelekea siku ya mazishi yake, Jumapili ijayo, Ijumaa Wikienda limebaini.
Mtandao mmoja nchini humo umeukumbushia wosia huo huku familia ikianza kuonesha misimamo tofautitofauti, hali inayoashiria kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana.

Gari lililobeba mwili wa Nelson Mandela.
FAMILIA INAVYOTAKA
Habari za ndani zilisema kuwa familia inataka mazishi ya kiongozi huyo maarufu duniani yawe makubwa na ya kisasa kwa vile viongozi wa nchi mbalimbali duniani watahudhuria.
“Mandela ni kingozi mkubwa sana duniani, mazishi yake lazima yawe makubwa pia ya kisasa. Hawezi kuzikwa kama mwananchi wa kawaida,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo. 

Mmoja wa waombolezaji akigusa picha na Mandela.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa wakati familia hasa wajukuu na watoto wake wakishikilia msimamo huo, wapo wanandugu wanaotaka azikwe kama alivyoandika katika wosia wake huo.
SERIKALI YAPANGA MAMBO BILA KUFUATA WOSIA
Habari zaidi zilisema kuwa Serikali ya Afrika Kusini inajitahidi kuupangua wosia huo kwa kuendelea na maandalizi ya mazishi kama haukuwahi kuwepo licha ya kwamba jamii ya watu nchini humo inaheshimu wosia wa marehemu.
WOSIA UNAVYOSEMA
Mzee Madiba alishauandika wosia huo kwenye karatasi moja tu ambapo aliagiza anavyotaka azikwe. Alisema kuwa akifa azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake katika Kijiji cha Qunu, Eastern Cape huko ‘Sauzi’.


Waombolezaji wakiweka maua katika sanamu la Mandela.
ALITAKA MAZISHI YA KAWAIDA SANA
Inadaiwa wosia huo aliuandika Januari, 1996 wakati bado akiwa rais ambao ulijaa maelekezo yote juu ya mazishi yake. Aliagiza kufanyiwa mazishi ya kawaida sana yenye hadhi ya raia wa kawaida nchini humo hivyo kuyafanya kuwa makubwa na ya kifahari ni kukiuka wosia wa mzee.
KABURI ALILOLITAKA MANDELA
Katika wosia wake huo uliotolewa na rafiki yake wa karibu, Mzee Madiba aliandika kuwa akifa azikwe katika eneo la familia lenye makaburi ya ukoo wa Mandela kijijini hapo.
Pia aliagiza kuwa kaburi lake liwekewe jiwe la kawaida kama alama ya mahali lilipo ili lisije kupotea kwa mvua au mabadiliko ya tabia nchi.


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
KABURI LISISAKAFIWE
Katika tafsiri ya maneno hayo, Mzee Madiba alitaka kaburi lake liwe la kawaida sana, akimaanisha lisijengewe kama ilivyokuwa kwa makaburi ya viongozi wengine wa mfano wake barani Afrika kama, Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Kamuzu Banda (aliyekuwa Rais wa Malawi).
WOSIA WAKE ULIKUWA WA UPANDE MMOJA WA KARATASI
Magazeti ya nchini humo, South African Mail na Guardian miezi ya karibuni yaliripoti kumnukuu rafiki huyo wa siku nyingi wa familia ya Mandela akisema: “Madiba hakuwahi kukifanya kifo kuwa jambo kubwa la kufikiriwa, pia hakuwahi kutaka chochote cha fahari wakati wa kumzika.” 
Cha ajabu, wosia huo wa Mandela ulitosha kwenye upande mmoja wa karatasi ya kawaida ya kuandikia licha ya kwamba mauzo ya kitabu chake cha Long Walk to Freedom na michoro yenye jina lake vilimpatia mamilioni ya fedha.


elson Mandela (kulia) akiwa na Mwalimu Julius Nyerere enzi za uhai wao.
FAMILIA YACHUKIZWA NA WOSIA
Wosia huo ulielezwa kuwashangaza watu wengi duniani kwani waliamini angekuwa na vitu vingi vya kuandika kulingana na uwezo wake.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, SABC, suala hilo la sehemu atakayozikwa Mzee Madiba liliiudhi mno familia yake akiwemo yule mjukuu wake ambaye ni chifu, Mandla Mandela aliyewahi kufikishwa kortini kwa kuhamisha makaburi hayo ya ukoo na kuyapeleka sehemu nyingine. Pia ndiye msemaji wa familia ya Mandela.
DUNIA YAMKATALIA
Baadhi ya wanaharakati ulimwenguni kote walisema wosia huo unapingana na matakwa ya dunia nzima, ambapo walitaka maziko ya mzee huyo yawe  makubwa na ya kihistoria ambayo hayajawahi kutokea.Ilifahamika kwamba dunia inataka mazishi hayo yavunje ile rekodi iliyoshikiliwa na mazishi ya Papa John Paul II aliyefariki dunia Aprili 2, 2005.


Mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla Mandela.
SAFARI HII HAKUKIMBIZWA HOSPITALI
Mzee Madiba ambaye alitimiza umri wa miaka 95 Julai 18, mwaka huu, alikuwa hospitalini kwa karibu miezi  mitatu nyuma akitibiwa maambukizi kwenye mapafu huku akipumulia mashine. Baadaye alipata nafuu na kurudishwa nyumbani ambako usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita aliugua ghafla na kufariki dunia.




Thursday, November 28, 2013

WARAKA HALISI WA MKAKATI WA MADILIKO 2013 CHADEMA UTATA 

Utata mkubwa umeibuka kuhusu waraka halisi wa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ uliosababisha Zitto Kabwe kuvuliwa wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika Novemba 20 - 22, mwaka huu.

Baada ya juzi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika kuwaeleza wanahabari kuwa waraka uliochapishwa katika magazeti na mitandao ya kijamii, siyo halisi, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba amejitokeza na kuutetea huku akidai kwamba huo unaodaiwa na uongozi kuwa ndiyo halisi umeghushiwa.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alivuliwa uongozi pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na Mwigamba kutokana na madai ya kuandaa waraka huo ambao Chadema kimesema ulikuwa unaeleza mbinu za uasi za viongozi hao ambazo zingetumika wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho jambo ambalo ni kinyume na katiba, sheria na itifaki zake.

Katika tamko alilotoa jana, Mwigamba alidai kwamba

kuna njama zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa Chadema ili kuubadili waraka halisi wa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ kwa lengo la kupoteza maana yake, huku akisisitiza kuwa waraka halisi hauna tatizo lolote.

Katika madai yake, Mnyika alisema waraka huo unaosambazwa na kuchapishwa, si ule uliowasilishwa na kujadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu na kuahidi kuutoa waraka halisi ambao una mambo makubwa na mengi zaidi.

“Waraka utakaotumika katika mashtaka yao siyo huo. Sisi tutautumia ule ambao uliwasilishwa katika Kamati Kuu ambao una mambo makubwa na mengi zaidi kuliko huo unaochapishwa sehemu mbalimbali, ikibidi tutautoa huo waraka halisi,” alisema.

Hata hivyo, jana Mwigamba alisema waraka halisi ni ule ambao upo katika kompyuta mpakato (Laptop) aliyonyang’anywa na wanachama wa Chadema, Oktoba 25, mwaka huu, katika mkutano mjini Arusha.

“Waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ni sahihi neno kwa neno kama nilivyousoma katika magazeti ya jana (juzi), pamoja na nakala iliyopo katika mtandao wa kijamii wa Jamii Forums.”

Aliongeza: “Ili kuthibitisha kwamba waraka ule ndiyo wenyewe, nawatumieni ‘soft copy’ kutoka kwenye kompyuta yangu kwani waraka huo uliibwa kutoka katika kompyuta hiyo ambayo nilirudishiwa baada ya wao kuikagua na kukuta waraka huo halisi.”

Mwigamba alisema waraka wake unatofautiana kwa kiasi kikubwa na ule ambao Chadema kinasema kuwa ndiyo halisi: “Lissu na wenzake wana mpango wa kuuchakachua waraka huu, lakini wamekwama.”

Alisema kuandaa waraka huo siyo uhaini kama ambavyo imekuwa ikielezwa na viongozi wa Chadema na kusisitiza kuwa ni waraka wa kusaka ushindi katika uchaguzi halali ndani ya chama hicho uliopangwa kufanyika Desemba mwaka huu na baadaye kusogezwa hadi Juni mwakani.

“Wakati wa uchaguzi si ajabu kuwepo kwa wanachama wanaounga mkono wagombea tofauti. Nimekuwa karibu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa miaka mingi, najua hata yeye ana mikakati na wanaoshiriki mkakati wake ni Lissu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema,” alisema.

Alisema anashangazwa kwa kitendo cha Chadema kuusambaza waraka huo, wakati ulikuwa ni mpango wa siri kati yake, Dk Kitila pamoja na mtu mwingine anayetajwa kwa jina la M2.

“Baada ya kugundua madhara ya kusambaza ovyo waraka huo, sasa wameamua kuukana, waraka wangu ni sahihi na unaeleza ukweli. Binafsi nimefanya kazi ofisi ya makao makuu ya chama kama Mhasibu Mkuu ningeweza kuanika mengi lakini sijafanya hivyo kwa masilahi ya chama,” alisema na kuongeza:

“Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia Zitto na tangu siku nyingi walipanga kumfukuza. Nawashauri watafute sababu nzuri za kumfukuza uongozi na hata uanachama. Zitto hahusiki na mkakati huu pamoja na kwamba alikuwa ndiye mhusika mkuu, alikuwa hajui lolote.”

Jumamosi iliyopita, mama yake mzazi Zitto, Shida Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema waraka huo ulikuwa umeongezwa maneno.

“Hata ule waraka uliongezwa maneno baada ya baadhi ya wanachama kumpora Mwigamba `laptop’ yake alipokuwa mkoani Arusha katika kikao cha Chadema,” alisema bila kutaka kufafanua ulibadilishwa vipi, licha ya kuwataja kwa majina waliohusika kuubadili wakiwamo wabunge wawili wa chama hicho na viongozi wa ngazi za juu.

Sitoki Chadema

Kuhusu hatima yake ndani ya Chadema, Mwigamba alisema hana mpango wa kuondoka hata baada ya kuvuliwa uongozi, huku akisisitiza kuwa hakusudii kuomba radhi kutokana na kuandaa waraka huo.

Alisema hakusudii kuhama kwa kuwa ana historia ndefu na Chadema na anaamini kuwa ndicho mkombozi wa Watanzania.

“Nimekuwa kiongozi wa kata, wilaya, mkoa hadi taifa. Nimetumia muda wangu mwingi na hata kuhatarisha maisha yangu kwa ajili ya chama hiki, siwezi kuondoka kutokana na tofauti za kimitazamo na viongozi wangu,” alisema.

Mwigamba, ambaye alikuwa mfanyakazi katika Mahakama ya Kimataifa inayosikiliza Kesi za Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (ICTR) na baadaye kujiondoa ili ajikite kwenye siasa, alisema ana imani yanayotokea sasa katika chama hicho yatapita salama.
Mwananchi 

VIA UDAKU SPECIALLY

BABA KANUMBA ATOA MPYA>>>>>>>>>>>>

KAMA KUNA WANAWAKE WANAO TAKA KUZAA NA MIMI WAJITOKEZE"BABA KANUMBA"

ABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa amefunguka kuwa baada ya kutangaza kuwa wanawake wanaotaka uzao wake wajitokeze azae nao, wamejitokeza kumi lakini akawapa masharti, yakawashinda.

Akizungumza na mwandishi wetu, baba Kanumba aliweka bayana kuwa warembo hao waliojitokeza aliwapa sharti la kwenda kupima Ukimwi lakini ajabu wote waliingia mitini.
“Wamejitokeza vizuri lakini nashangaa wote wamekuwa wazito katika suala la kupima Ukimwi wameingia mitini, kama wapo wengine watakaolimudu sharti hilo, nawakaribisha,” alisema baba Kanumba 



VIA UDAKU SPECIALLY

Thursday, July 25, 2013

MGONI AKATWA MIGUU BAADA YA KUFUMANIWA AKIVUNJA AMRI YA 6 NA MKE WA MTU

 Miguu ya Said Iddi ikivuja damu baada ya kukatwa
 KilosaALI Omar, mkazi wa Kijiji cha Mabana, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumkata miguu Said  Iddi kwa kumtuhumu kumfumania na mkewe aliyejulikana kwa jina la mama Ali, mkanda mzima upo mikononi mwa Amani.
Said  Iddi akiwa chini baada ya kukatwa miguu na Ali Omar.Tukio hilo la kikatili lilijiri Julai 15, mwaka huu wakati Said na mama Ali walipokuwa ndani ya nyumba ya Ali iliyopo kijijini Hapo

 

MANENO YA SHUHUDA
Akizungumza na mwandishi wetu, shuhuda mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alisema Said alifumaniwa ndani ya nyumba asubuhi akiwa na mke wa Ali baada ya kuwekewa mtego ambao ulimnasa vizuri.
“Ali alipewa habari na kijana mmoja aitwaye God kwamba mkewe si mwaminifu katika ndoa, akamwongezea kuwa anatoka kimapenzi na Said. Ndipo Ali na mnyetishaji wake huyo walipopanga kumfumania jamaa,” alisema shuhuda.


 Said akipelekwa kwenye difenda.
MWENYE MKE AKIMBIA, ANASWA
Ali, God na baunsa walikimbia eneo hilo. Baadhi ya wanawake walitumia khanga zao kuifunga miguu ya Said kwa lengo la kujaribu kuzuia damu isiendelee kumwagika. Said alikuwa akilia sana.
“Wanakijiji walichukizwa sana na ukatili uliofanywa na Ali, hivyo wakaanza kumsaka na kumkamata kichakani akiwa amejificha pamoja na God. Alipewa mkong’oto kwa lengo la kutaka kumuua, lakini viongozi wa kijiji walisihi asiuawe bali afikishwe kwenye kituo cha polisi,” alisema shuhuda

 
 MKE, MUME, MMBEYA WAFIKISHWA POLISI
Polisi wa Kituo cha Dumila waliitwa na kumchukua Said, Ali na God kwa kutumia gari aina ya Land Rover lenye namba za usajili T 750 AAJ. Mke wa Ali yeye alipelekwa polisi kwa pikipiki.
Walipofika kituoni, Said alipewa fomu ya matibabu ya polisi (PF 3) na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa matibabu.
“Pale hospitali Said alishonwa miguu yote lakini madaktari wakaamua ahamishiwe katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi,” alisema shuhuda huyo.
ANAWEZA ASITEMBEE TENA
Akaongeza: Daktari mmoja alisema haamini kama jamaa (Said) atatembea tena kwa sababu zana iliyotumika kumkata ilifika hadi kwenye mishipa ya nyuma ambayo ndiyo humfanya binadamu aweze kusimama na kutembea.

 .Said akishonwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.BAUNSA ASAKWA
Afisa mmoja wa polisi kituoni hapo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji, alisema wanaendelea kumsaka baunsa aliyeshirikiana na Ali kumkata miguu Said.
 .Kijana aitwaye God (kulia) aliyetoa taarifa kwa Ali naye akiwa chini ya ulinzi.Katika kufanikisha mtego huo, mmbeya huyo alipewa jukumu la kuhakikisha nyendo za Said na mama Ali siku hiyo zinarekodiwa mpaka kuingia ndani ya nyumba hiyo na kumtaarifu Ali ambaye siku hiyo alimuaga mkewe kwamba amesafiri.

SAID ATINGA NYUMBANI KWA ALI
Habari zinasema mtoboa siri huyo alimwambia Said kuwa Ali amesafiri na ndipo jamaa akafunga safari kwenda kwa mama Ali kwa nia ya kujivinjari licha ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukifikia katikati
 Mwenye mali, Ali Omar (kati) akiwa chini ya ulinzi baada ya kumkata Said.Aliongeza kudai kuwa, Said ni msimamizi wa mashamba ya Ali kijijini hapo na kwamba God ni mtoto wa mwenye nyumba ambayo Ali amepanga kijijini hapo.
MPANGO WA FUMANIZI
Habari zinapasha kuwa mara baada ya mnyetishaji kutoa taarifa za usaliti huo, Ali alimtafuta  ‘baunsa’ ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja na wakaweka mtego kwa kujificha karibu na nyumba hiyo ambayo Said angeingia ili kuivunja amri ya sita ya Mungu
Mke wa Ali Omar naye akipelekwa polisi baada ya tukio hilo.Habari zinadai mara baada ya kufika kwa Ali, Said aliingia ndani ya nyumba bila kujua kwamba mwenye mke alikuwa amejificha jirani akisubiri mtego unase.
Inasemekana Said akiwa ndani, Ali na baunsa wake waliibuka kwa kutaarifiwa na God na kumnasa jamaa huyo huku akidai ni mgoni wake. Alimuuliza maswali kadhaa, yakiwemo haya:
“Umekuja kufanya nini ndani ya nyumba yangu? Kwa nini umekaa na mke wangu?”
Habari zinasema Said alijibu hakuona ubaya kwa kuwa yeye ni mwangalizi wa mashamba ya mwanaume huyo hivyo anaweza kuingia ndani kwake wakati wowote.