Pages

Monday, May 6, 2013

MWANAMKE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI




AMEUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR'

'Majambazi yamempora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi na kutokomea nazo kusikojulikana....
Tukio hilo limetokea jana saa 5:16 jioni na


Inavyosemekana ni kuwa mwanamke huyo alikuwa akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia..
Alipotoka ,majambazi hayo yalimfuata na kuligonga gari lake makusudi na ndipo dada huyo aliposimama ili kuangalia nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa. ..

MILIPUKO KANISANI JIJINI ARUSHA





JESHI  la polisi jijini Arusha limesema linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la ulipuaji lililofanyika katika kanisa la Arusha.

Tukio hilo ambalo limetokea majira ya saa tano asubuhi ya leo tarehe 5 mwezi huu Mei  katika Parokia ya Mpya ya Joseph Mfanyakazi iliyokuwa inafunguliwa rasmi kumetokea mlipuko uliojeruhi watu zaidi ya 25.

Parokia hiyo teule ya orasiti- ya mtakatifu Joseph mfanyakazi Arusha ilikuwa ikifanya uzinduzi mpya, ambapo Kwa mujibu wa taarifa zinazosikika moja kwa moja kupitia Radio Maria, Tanzania, mlipuko huo umetokana na kitu kinasadikika kuwa ni bomu.

Hata  hivyo haijafahamika ikiwa mlipuko huo ulikuwa niwa  bomu la kutegwa ama la kurushwa kwa mkono kutokana na jeshi la polisi kuendelea na uchunguzi wake juu ya mlipuko huo.

Inaripotiwa kuwa wengi wamejeruhiwa miguuni na kulazimika kuwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Hakuna taarifa zozote za kifo zilizoripotiwa katika tukio hilo.

Aidha viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo mwakilishi wa Papa aliyekuwa anatabaruku Kigango hicho kilichozaliwa mwaka 2008 kuwa Parokia, Padre Francisco Padilla na viongozi wa jeshi la polisi na usalama, wanaendelea na kikao ili kuamua hatima ya misa iliyokatizwa.

Hata hivyo kutokana na usalama wa waumini waliokuwemo katika kanisa hilo, wametakiwa kuondoka na hivyo kukatishwa kwa misa na matukio hayo ya uzinduzi.

Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha, akiwemo mkuu wa mkoa, Mbunge wamefika katika eneo hilo, huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi

Monday, April 1, 2013

JENGO LILILOANGUKA DAR WALIOKUFA SASA NI 29!!




Maghorofa matatu watu wahamishwa
  Mkandarasi diwani wa CCM mbaroni

Wakati miili ya watu waliokufa katika jengo la ghorofa 16 lililoporomoka Ijumaa ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam iliyopatikana ikiwa imefikia 29, serikali imeamuru watu waliopo katika maghorofa mengine matatu yaliyopo jirani na ghorofa hilo kuhama mara moja kwa sababu hayapo katika hali ya usalama.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema majengo hayo yanayomikiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wapangaji wake wanatakiwa kuondoka ili uchunguzi ufanyike kubaini kama yana uimara unaotakiwa.


Sadiki alisema majengo hayo yanaweza yakawa yamepata mtikisiko mkubwa kutokana na kuwa karibu na ghorofa lililoanguka na ghorofa moja kati ya hayo matatu tayari limeonyesha dalili za kuwa na nyufa.

“Nimewaagiza Shirika la Nyumba la Taifa kuwaondoa wapangaji wake wote waliopo karibu na ghorofa lililoporomoka ili uchunguzi wa majengo hayo ufanyike,” alisema Sadiki.
Alisema NHC watagharamia gharama zote za mazishi kwa maana ya jeneza, sanda na kusafirisha miili ya waliokufa kupelekwa katika maeneo mbalimbali ya nchi.

WALIOKUFA WAFIKIA 29
Awali akizungumza na NIPASHE jana mchana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema kuwa idadi ya watu waliokufa imefikia 28.

Hata hivyo, baadaye jioni Sadiki aliiambia gazeti hili kuwa idadi hiyo imeongezeka na kufikia watu 29 na kwamba hadi saa 1:10 usiku zoezi la kutafuta miili zaidi lilikuwa linaendelea.

Sadiki alisema zoezi hilo litaendelea ili kuhakikisha kwamba linakamilika kwa siku ya jana.

WALIOKAMATWA WAONGEZEKA
Katika tukio lingine; Kamanda Kova alisema kuwa idadi ya watu wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo imeongezeka na kufikia wanane.

 Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni mmiliki wa ghorofa hilo, Raza Husein Damji (69) na mtoto wake, Ally Raza Damji (31) ambaye alikuwa akishirikiana naye.

Wengine  ni wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,  Mhandisi Ogare Salu, Mhandisi wa Majengo , Goodluck Mbagaga, na Mkaguzi wa Majengo, Wilbroad Mugyabusu.

Mkandarasi wa Kampuni ya Lucky Construction iliyokuwa ikijenga jengo hilo na ni Diwani wa Goba (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Ibrahim Mohamed Kisoki.

Pia wamo  Zonazea Anage Oushadada (53), ambaye ni Mhandisi Mshauri na Mohamed Abdulkarim (61), mshauri wa kujitegemea aliyekuwa akitumiwa na mmiliki wa jengo.
Alisema watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo kama wangekuwa makini, janga hilo lisingetokea na kwamba wakati wakiendelea kuhojiwa, Jeshi la Polisi nalo litaendelea kuchunguza.

Kova alisema wakati wa zoezi la kuokoa watu waliofukiwa na kifusi cha jengo hilo likiendelea, walikuta nondo na mifuko kadhaa ya saruji ambayo ilikuwa imefukiwa kabla ya kutumika.

 Alisema kutokana na tukio hilo, serikali imemua kuchukua majina ya watu ambao ni wataalam wa masuala ya majanga ili kunapotokea janga wanaitwa haraka kusaidia.
 Kamanda huyo alitoa onyo kwa watu wanaochukua nondo zinazotupwa pamoja na kifusi kutoka katika jengo lililoporomoka na kwenda kuziuza na kwamba wakikamatwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

‘MAGHOROFA YOTE DAR ES SALAAM SIYO SALAMA’
Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia, akizungumza jana na waandishi wa habari, alisema majengo mengi hususani maghorofa katika Jiji la Dar es Salaam siyo salama kwa kuishi.

Mbatia alisema majengo hayo siyo salama kutokana na kujengwa chini ya kiwango na kwamba kama kukitokea tetemeko la ardhi, majanga yanaweza kutokea kila wakati.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema kutokana na hali hiyo, serikali inatakiwa kuchukua maamuzi magumu kuwaondoa wananchi wanaoishi katika maghorofa na kufanya utafiti wa majengo hayo kubaini kama yana uimara unaotakiwa.

“Vifaa vya ujenzi TBS (Shirika la Viwango la Taifa) linapitisha tu, pia wapo watu wanaotoa vibali nao wanatoa vibali tu bila kufanya utafiti na kufuatilia ujenzi wa maghorofa, hii ni hatari katika nchi yetu,” alisema Mbatia.

Mbatia ambaye ana taaluma ya uhandisi alisema: “Yametokea matukio mengi ya maghorofa kuporomoka, lakini bado  hatujajifunza na  tukio hili lililotokea mfano likijitokeza jingine hili lililotokea litasahaulika.”

Alisema kuna haja ya kuwa na kitengo maalum cha kushughulikia majanga na wabunge katika mkutano ujao wa Bunge wanatakiwa kushinikiza suala hilo.

Naye Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, alisema ghorofa pacha na lililoporomoka lililokuwa likijengwa na mkandarasi mmoja linatakiwa kubomolewa haraka ili lisije likasababisha janga jingine.

“Serikali ilibomoe haraka jengo hili na kama haitatekeleza tutajua kuna mkono wa rushwa, tunahitaji kuona nguvu ya John Magufuli (Waziri wa Ujenzi) kama masuala ya ujenzi wa majengo siyo kwenye ujenzi wa barabara tu,” alisema Machali.
Machali alisema kama jengo hilo halitaangushwa, watatangaza mgogoro na serikali.

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI KUTOA TAMKO

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye, alisema wizara yake itatoa tamko la serikali baada ya kazi ya kufukua kifusi cha ghorofa hilo lililoporomoka kukamilika.

Medeye alisema utata kuhusu kibali kilichotolewa kama kilikuwa cha kujenga ghorofa tisa au 16 litatolewa ufafanuzi.

KIKWETE ATEMBELEA WAJERUHI MUHIMBILI

Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete jana waliwatembelea majeruhi wa ajali ya  jengo lililoporomoka hivi karibuni waliolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Rais Kikwete aliyeambatana na mkewe, Salma na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadiki, alifika MNH majira ya asubuhi kwa ajili ya kuwajulia hali majeruhi hao.

Alitembelea wodi ya Sewahaji namba 17 walikolazwa majeruhi wawili, pamoja na Taasisi ya Mifupa (Moi) katika wodi binafsi ya  wagonjwa walikolazwa wengine wawili.

Akizungumzia tukio hilo juzi, Kova alisema zoezi ya uokoaji liliendelea usiku kucha na miili hiyo imehifadhiwa MNH ilikowekwa kambi itakayosaidia watu kugundua miili ya ndugu zao.

Friday, March 29, 2013

HABARI MPASUKO!! JENGO LA GHOROFA 16 LILILOKUWA LIKIJENGWA KATIKA MAKUTANO YA INDIRA GANDHI NA MOROGORO JIJINI DAR LAANGUKA WATU KADHAA WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA!!!!!

Kwa maelezo ya shuhuda, inasemekana limeanguka saa moja asubuhi ambapo kwa muda huo kulikua na watoto wa kihindi wanacheza mpira, kulikua na vibarua ambao wanataka kumwaga zege kuendelea na ujenzi na ndio walikua wanabadilisha nguo kuanza kazi.Ni posta mtaa wa Indira Gandhi pembeni ya msikiti mkubwa wa Itnasheri, lilikua ni gorofa la floor 12 ambapo mpaka sasa hakuna hesabu kamili ya vifo lakini shuhuda anasema kwa muda mfupi baada ya kuanguka alishuhusia maiti 12.




Thursday, March 21, 2013

ALIYEPIGWA RISASI JANA KINONDONI SOMA ZAIDI HAPA




Mpaka sasa hivi sijapata maelezo yoyote kutoka kwa Polisi Kinondoni kuhusu kijana alieuwawa kwa risasi akiwa anaendesha gari dogo kwenye foleni Kinondoni Dar es salaam march 20 2013.

Nafasi hii naitumia kumkariri mmoja wa mashuhuda wa hilo tukio akisema “ni kwenye barabara ya kutoka Magomeni kwenda Mkwajuni hii gari ilikua inashuka, kwa sababu sasa hivi kuna foleni upande wa kulia kuna magari upande wa kushoto kuna magari, pikipiki kama kawaida zikawa zinatanua katikati”

“Wakati pikipiki ya muhusika ilipotanua ghafla ilibidi dereva huyu aliyeuwawa amkwepe hivyo akagonga gari lake kwenye kingo za barabara na kupasua tairi, marehemu akatoka kwenye gari na kukutana na jamaa wa pikipiki wenye asili ya kiarabu wakaanza kubishana na kuwaambia amepasua tairi kwa sababu alikua anawakwepa wao kwa hiyo wamlipe tairi lake tu” – Shuhuda

“Wale waarabu walikua na waya flani kama za shoti, yani zinapiga shoti ndio wakawa wanawapiga kama shoti mwilini.. zikatokea purukushani Mwarabu mmoja akamwambia Marehemu nitakuua,

yule Marehemu akasema huna uwezo wa kuniua wewe… ndio mwarabu akampiga risasi ya shingo na kudondoka palepale na kufariki,  majirani ndio wakachukua kanga na kumfunika, mpaka naondoka pale Polisi walikua wamefika kwenye eneo la tukio”  – Shuhuda

Bado naendelea kuisubiri kauli ya polisi kuhusu hili tukio, pia nina ahadi ya kukutana na mmoja kati ya vijana waliokua pamoja na marehemu kwenye gari wakitokea gereji… nikiipata wakati wowote nitairipoti hivyo kuwa tu karibu na mimi kwenye

ALIYEUA TRAFFIC DSM AZIDI KUBANWA






Elikiza Nko 
Kwa ufupi


‘’Juzi usiku tuliwahoji na mmoja wao alitudanganya, tulipomuuliza dereva wa gari hili ni nani akajibu siyo mimi nimeachiwa na mwenyewe amekimbia” alisema Kamanda Mpinga na kuongeza kuwa baada ya kumbana alikiri kuwa ndiye.

Dar es Salaam. Dereva wa gari lililomgonga na kumuua askari wa usalama barabarani, Elikiza Nko (pichani)  atafikishwa kortini wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika, ilielezwa jana.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini(trafiki), Mohammed Mpinga alisema hayo jana alipozungumzia tukio hilo ambalo lilisababisha simanzi kwa watu wengi.
Mpinga alisema polisi walifanikiwa kumkamata mhusika kwa mbinu za kipolisi na kwamba kwa jana alikuwa akihojiwa ili kupata ushahidi utakaowezesha kumpeleka kortini.
Alisema dereva huyo ni kati ya wale wawili waliowakamata   awali na  hatimaye mmoja walimbaini kuwa ni mhusika .

‘’Juzi usiku tuliwahoji na mmoja wao alitudanganya, tulipomuuliza dereva wa gari hili ni nani akajibu siyo mimi nimeachiwa na mwenyewe amekimbia” alisema Kamanda Mpinga na kuongeza kuwa baada ya kumbana alikiri kuwa ndiye.

Kwa mujibu wa Kamanda Mpinga marehemu ameacha mume na watoto watatu. Maziko yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya Mbweni yaliyopo Manispaa ya Kinondoni na yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.

Marehemu alifariki dunia baada ya kugongwa na gari lililokurupuka kuufuata msafara wa Rais Jakaya Kikwete eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita alipokuwa katika ziara ya kutembelea mkoa huo.
mwananchi