Pages

Thursday, November 1, 2012

RIHANA NA KARRUECHE WAONA POA KUSHARE PENZI LA CHRISS BROWN!



 
Mkasa wa mapenzi yenye pembe tatu zinazowahusisha warembo wawili Rihanna na Karrueche Tran kwa 'Don’t wake me up' hit maker Chris Brown unazidi kunoga siku hadi siku na imesemekana kuwa warembo hao wako poa tu na maisha yao na ‘baby boy’ wao Chris Breezy.

Mtu mmoja ameiambia Hollywood Life, “he got them both twisted up. He is trying to get as much p-y as he can before he leaves next month.”

Chanzo hicho kiliendelea kufunguka, “Chris anawapenda kweli wote na wanajua hilo na wao wanampenda pia”, akaendelea, “it’s crazy situation. Na inafanya kazi kwao, na ni kama RiRi na K.T wako poa tu na hili, hivo ndivyo ilivyo.”

Lakini stori za mtaa kwa upande mwingine zilisema Rihanna aliogopa pale alihisi kuwa labda Chris angeenda na Karrueche T kwenye party yake kubwa ya Halloween iliyowakutanisha mastaa kibao jumatano ya wiki hii.

Mtu mmoja alisema, “ingawa the 'umbrella' hit maker RiRi alikuwa poa tu kwa kile kinachoendelea kati ya Chris B na K.T lakini hakuwa na uhakika kama Chris ataamua kwenda kwenye party yake na K.T na hii ni kutokanana tetesi ambazo zilikuwa zimetapakaa mitaani na kwenye mitandao kuwa huenda Chris akatokea pale akiwa na K.T kama kawaida. Hapo ndo utaona kweli mapenzi ya watatu hayawezekani hasa inapoonekana kuwa itabidi kukutana kwenye eneo moja.

Chis Brezzy alitangaza kuachana na Karrueche October 4, na kauli yake ilikuwa ,” nimeamua kuwa single ili nifocus kwenye kazi yangu. Nampenda sana Karrueche lakini sitaki kumuona anaoumia kwa sababu ya urafiki wangu na Rihanna. Badala yake inabidi niwe single ili Kurusu kila mmoja wetu kuwa na furaha.”

Siku chache zilizofuata Chris B alitoa video ikiwa na kauli nyingine inayoonesha kweli anawapenda wote Rihanna na Karueche na hajui afanye nini na hajui kama kweli inawezekana kuwapenda watu wawili lakini ndivyo yeye anavyojisikia, lakini mwisho wa siku ikaonekana kabisa ameamua kuhamia rasmi kwa Rihanna wake wa zamani na kumtangaza rasmi japo ndo hivyo tena hawaachani na Karrueche pia. 

Haya ndiyo yanayoitwa Triangular Love, “mapenzi ya pembe tatu”.

ABOOD YAPATA AJALI MBEYA

 
 
GARI LA ABOOD LENYE USAJILI WA NAMBA T 545 AZE LIMEPATA AJALI MAENEO YA SAE SEHEMU MAARUFU  KWA JINA LA KWA MBILINYI LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA TUNDUMA. AJALI HIYO IMETOKEA BAADA YA LORI LA MIZIGO AINA YA SCANIA LIKIWA LIMETOKEA ZAMBIA KUELEKEA DAR WAKATI WA KUTAKA KUPISHANA NA BASI HILO, NA NDIPO GARI AINA YA KENTA IKAJITOKEZA NA KUJICHOMEKA BARABARANI NA KUSABABISHA AJALI HIYO.

Tuesday, October 30, 2012

Professor Jay: Tanzania’s Hip Hop Legend



Tanzanian music has always impressed and lived up to the praise it earns from across the divide of Africa’s entertainment sector.

From the very traditional cord-based Taarab to the modern day American hip hop adaptation; it continues to be a useful source of entertainment to millions of people in and around the East African region.

Joseph Haule, otherwise known as Professor Jay, is one of the Tanzania’s biggest hip hop acts, if not the most popular in East and Central Africa.

In the last decade, Jay, widely referred to as “East and Central Africa’s finest”, has grown to become a force most hip hop acts in Tanzania look up to and respect.

Friday, October 26, 2012

MWALIMU WA CHUO CHA UFUNDI VETA MOROGORO AJINYONGA


Mwalimu wa chuo cha veta marogoro akutwa amejinyonga kataka mwambao wa mto kilakala mjini morogoro asubuhi ya leo,Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mwalimu huyo amejinyonga asubuhi ya leo kwa kutumia mkanda wa suruali.Inasemekana ameonekana subuhi ya leo mtaa wa madizini kilakala kabla tukio hilo halijatokea mchana huu..picha zaidi tembelea

Thursday, October 25, 2012

KATIBU WA BAKWATA MKOA WA ARUSHA ANUSURIKA KIFO BAADA YA YA BOMU LA MKUONO KURUSHWA NYUMBANI KWAKE NA WATU WASIOJULIKANA USIKU WA KUAMKIA LEO




Katibu wa bakwata Mkoa wa Arusha Bw. Abdulkarimu Jonjo akiugulia maumivu katika wodi ya majeruhi ,katika hospitali ya mkoa mount Meru baada ya kulipuliwa na bomu la kutupwa na mkono akiwa amelala usingizini nyumbani kwake na watu wasiofahamika majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo. Picha na Josefu Ngilisho.


KATIBU mkuu wa Bakwata mkoani Arusha,Abdulkarim Jonjo (52) mkazi wa Esso jijini Arusha,amenusulika kufa baada ya kujeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospital ya Mkoa Mount Meru baada ya watu wasiojulikana kumlipua kwa bomu la kurushwa kwa mkono akiwa amelala usingizini nyumbani kwake. 

Akiongea kwa taabu katika wodi ya majeruhi hospitalini hapo,Jonjo alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 6.30 usiku akiwa amelala baada ya kuona mwanga wa cheche dirishani kwake na kufuatiwa na kishindo cha mlipuko. 

Alisema kuwa hali hiyo ilimlazimu kuinuka kitandani

KITUKO MAHAKAMANI: JUSTINE BIEBER ASHTAKIWA NA MTU ANAEDAI KUWA BABA WA GF WAKE, ETI ALIMUIBIA CREDIT CARD ILI AKUZE PEN*S YAKE”.



Katika hali ambayo inaonesha kuwa ni kituko cha mwaka, ama kichekesho flani tu ambacho obvious kinaonesha kutokuwa na ukweli, mtu mmoja ambae anadai kuwa ni baba mzazi wa girlfriend wa Justine Bieber mrembo Selena Gomez amefungua kesi mahakamani pande za Michgan.

Mtu huyo alifungua kesi yenye mambo mengi ya kushangaza, na pamoja na malalamiko yake pia yamewahusisha mastaa wengine wakubwa, haya ni kati ya malalamiko ya mtu huyo.

…“Bieber alinikopa $ 426.78 na hajawahi kunirudishia. Hizi pesa zilitumika kwa ajili ya kufanya abortion kwa sababu Justine Bieber alimpa binti yangu ujauzito kwenye chumba changu.”

…“Usher Raymond alikuja nyumbani kwangu tarehe 4, july 2012 na akaniingilia kinyume na maumbile na firework na akaiwasha in my anal area wakati huo anapiga makelele na wimbo wa Kate Perry Firework kwenye ngoma ya masikio yangu.”

…“Bieber aliiba credit card kwa ajili ya kununua cocaine kwa ajili yake na Sean P-ditty Combs.” Duh hapa alimaanisha P-Diddy, it’s funny heh!!!

….“Bieber pia alifanya pen*s enlargement kwa credit card yangu aina ya  ‘American express’.”

Lakini pia eti Bieber alimcheat binti yake na kutoka na Rihanna, Kisha na Penelope Cruz.

Hata hivyo mwisho wa malalamiko hayo akamaliza kuwa… “I’m an emotional mess…marekani inabidi isimamishe biashara ya muziki wa Bieber.”

Document ya kesi hii imenaswa na mtandao wa TMZ na hii ni document ambayo ni ya ajabu na ina malalamiko yasiyo ya kweli hata kwa kuyasikia tu, na inawezekana hayajawahi kutokea mahakamani hapo.

Kwa hiyo TMZ iliona hakukuwa na haja ya kumtafuta Bieber kumuuliza haya kwa sababu ni obvious ni uongo mtupu.

 




Wazazi tuwe makini na wasichana wa kazi

JUKUMU la malezi kwa watoto katika familia linawahusu wazazi wote wawili. Tofauti na ilivyokuwa huko nyuma siku hizi wazazi wote wawili wanapaswa kutafuta kwa ajili ya kusaidia familia. Mabadiliko hayo yamekuja baada ya hali ya maisha kuwa ngumu na kila mtu kuona hakuna sababu ya mmoja kubaki nyumbani.

Kila mzazi ana taratibu zake katika suala zima la malezi katika familia. Ingawa sote tunafahamu kuwa hakuna mzazi anayetegemea kumpotosha mtoto wake hata siku moja.

Wazazi wamekua wakiishi kwa imani na wasichana wa kazi na kweli baadhi ya wasichana wamekuwa wazuri katika jukumu la kulea watoto pamoja na familia kwa ujumla. Wamekuwa ni msaada mkubwa katika familia husika na pengine kubeba majukukumu makubwa kuliko ilivyotegemewa.

Baadhi ya wasichana wa kazi wamekuwa wakijitolea kulea familia iliyoachwa pengine na wazazi wote wawili na kubaki kwa upendo tu kulea familia isiyo yake.

Katika msafara wa mamba na kenge hawakosi, baadhi ya wasichana wa kazi wamekuwa hawako kama ambavyo mtu yeyote angetegemea, wamekuwa si walezi wazuri wawapo na watoto majumbani.

Hasa muda ambao wazazi wanakuwa wako katika kazi zao hawajui nini kinaendelea nyuma yao.

Kutikana na hali hii, kama mzazi unapaswa kuwa mwangalifu unapotaka kuishi na msichana wa kazi. Wanawake wengi wamekuwa wakihofia ndoa zao tu wawapo na wasichana wa kazi na kusahau suala la watoto kwamba wanalelewa namna gani wao wawapo katika shughuli zao.

Husahau kabisa kuhusu jukumu la wao kuchunguza mienendo ya watoto kwa sababu wanafika jioni wamechoka kutokana na majukumu waliyonayo. Wanachojali ni watoto wamekula, wamevaa na ni wazima kiafya. Wanasahau kuwa karibu na watoto wao ili kujua nini kina wasibu.

Je, watoto wanampenda dada yao au wana mchukia? Au dada anawachukia watoto? Hivi ni vitu vidogo vidogo ninavyovizungumzia hapa lakini vinaweza kugharimu maisha ya watoto wetu huko mbeleni na usijue tatizo lilianzia wapi.

Mabinti watokapo vjijini kuja kufanya kazi mijini, huiga aina ya maisha ya mjini kwa sababu baadhi wanaamini kila kinachofanyika mjini ni kizuri wakati wowote. Nina mfano hai na ndio ulionivuta niandike kuhusu wasichana wa kazi.

Nilikuwa mgeni mahali fulani ambapo mimi niliongozana na bosi wa dada wa kazi, baada ya kufika kwake akamwambia msichana wake atafute mkanda mzuri wa kuangalia (CD).

Yule binti kwa kuwa alikuwa na shughuli nyingine anafanya akamtuma mtoto wa huyo bosi wake ambaye hushinda naye nyumbani akatafute. Lakini badala yake mtoto akaongoza kule kwenye CD inayomfurahisha zaidi bila dada kujua.

Nilishangazwa kuona mtoto analeta picha za ngono. Alifanya hivyo kwa kuwa picha hiyo ndio inayomvutia.

Alipoleta ile picha akasema; “hii ndio CD nzuri mama tuangalie hii ni nzuri sana mama.” Mama akabaki amepigwa na butwaa asijue la kufanya. Fikiria huyu mtoto ana miaka minne wewe kama mzazi unategemea msipokuwapo mchana kitu gani kinaendelea nyuma yenu?

Alipohojiwa binti akasema; “nimeazima kibandani ili niangalie.” Lakini kwanini aangalie na mtoto asiangalie mwenyewe hana la kujibu anabaki kuuma uma meno.

Wazazi uliyempa jukumu la kukulelea watoto hivi unadhani ni sahihi hali ya ugumu wa maisha ndio inayotufanya tushindwe kuwa karibu na watoto wetu mara turudipo nyumbani?

Mtoto anayengalia picha za iana hiyo ni mdogo sana, hivyo chochote anachokiona yeye kwake ni sahihi, hajui baya wala zuri.

Hili jambo unalibebaje kifuani kama mzazi na ni namna gani ulitatue ili mtoto akili yake ikae sawa kwa sababu msichana wa kazi hakuona kama ni tatizo kuangalia ile picha na mtoto. Licha ya kwamba umri wa dada huyu haukustahili kuangalia picha za aina hiyo.

Wazazi wapaswa sasa kutenga muda wa kufuatilia kwa ukaribu mambo yanayofanywa na wasichana wao wa kazi.

Kisa hiki kilinisikitisha sana na kujikuta nikitamanio kuwaasa wazazi kuwa karibu na binti zao ili kufahamu wanafanya nini pindi wanapokuwa kazini.

Kama hatutakuwa karibu na watoto wetu ni dhahiri kwamba tutawafanya wakose na maadili mema, kwani tumeshuhudia wazazi wengi ambao watoto wao wamekuwa wakipoteza mwilekeo kwa kukosa malezi bora ya mama na baba.

Toa Maoni yako kwa habari hii