MERCY MWALUSAMBA
Wednesday, October 22, 2014
NDEGE AGEUKA MTU NCHINI NIGERIA
Mwanamke huyo inasemekana alikuwa Ndege iliyokuwa inaruka mtini kabla ya kugeuka na kuwa binadamu.
Umati wa watu ulikusanyika eneo alilokuwa mwanamke huyo baadhi wakinasa matukio kwenye simu zao za mkononi. Polisi wawili walilazimika kurusha mabomu ya petroli kuwatawanya watu hao na kuwazuia kunasa
picha za mwanamke huyo aliyekuwa anachapwa sana.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, mmoja alisema kuwa mwanamke huyo dakika chache zilizopita alikuwa Ndege mtini kabla ya kugeuka na kuwa mwanamke.
Ndege huyo alikuwa anazunguka mti mjini Oshodi , kisha akagonga mlingoti wa stima kabla ya kuanguka ardhini ambapo aligeuka na kuwa mwanamke.
Hii ni kwa mujibu wa wakazi wa mjini Oshodi wanaodai kuwa mwanamke huyo alikuwa mchawi.
'Kitu cha kushangaza'
''Ni kitu cha kushangaza lakini ni cha kweli,'' alisema bwana Sobowale.
"tulipozungumza na mwanamke huyo alidai kuwa na nguvu za kiganga, na kwamba alikuwa amewaua watu kadhaa. Aliongeza kuwa alikuwa anarejea kwa mumewe anayeishi katika eneo la Mushin kabla ya tukio hilo. Baadhi ya watu walianza kumpiga picha. ''
Video ya umati huo ukimtandika mwanamke huyo imeenea kama moto msituni na kutazamwa na maelfu ya watu kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube.
Mwanamke huyo alikuwa uchi wa mnyama huku ngozi yake ikiwa inatoka baada ya kuchomwa.
Banke Idowu ni mmoja wa watu walionasa video ya mwanamke huyo akiwa anachapwa na umati na kwamba alikuwa amearifiwa na wenzake kuhusu mwanamke huyo alivyobadilika.
Aliambia BBC kuwa "sijawahi kuona jambo kama hili maishani mwangu,lakini nimesikia na kuona tu kwenye filamu kwa hivyo waliponiambia kuwa limetokea , mimi nimeamini. ''
Alisema angedhubutu kumuokoa mwanamke huyo umati huo ungemgeukia na yeye.
Polisi hawajuzungumzia tukio hilo, hususan kabla ya umati huo kukusanyika na kuanza kumchapa mwanamke huyo.
Alifariki mda mfupi baadaye huku mwili wake ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu.
VIA BBC Swahili
Tuesday, September 16, 2014
Thursday, May 22, 2014
HUYU NDIE MTOTO ALIEFUNGIWA NDANI YA BOX KWA MIAKA MINNE NA MAMA YAKE MKUBWA AKIHOFIA KUAMBUKIZWA UKIMWI
Mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa), amedhulumiwa haki yake ya utu
na kuteswa kwa zaidi ya miaka mitatu, kwa kufungiwa ndani ya boksi kama
mnyama, ili asimuambukize mama mlezi virusi vinavyosababisha Ukimwi.
Unyama huo wa kusikitisha, umefanyika muda wote huo kwa mtoto huyo Morogoro mjini katika mtaa wa Azimio bila kuripotiwa popote, huku wakazi na majirani wa nyumba hiyo wakisikia akikohoa na kulia usiku, na baba yake mzazi akiendelea na maisha kwa kumuogopa mkewe.
Wakizungumza na mwandishi jana, majirani hao walidai Mariam alihamia katika nyumba hiyo mwaka 2010, lakini hawakuwahi kumuona akiwa na mtoto.
Hata hivyo majirani hao walikiri kwamba walikuwa wakisikia mtoto akikohoa na kulia hasa nyakati za usiku, lakini walikuwa na wasiwasi kuwa huenda mtuhumiwa alikuwa mshirikina anayefuga watu waliouawa kishirikina au kwa jina lingine misukule.
Hatimaye juzi mateso ya mtoto huyo yalipungua, baada ya msamaria mmoja kupata taarifa sahihi, kwamba ndani ya nyumba hiyo kuna kiumbe asiye na hatia aliye katika mateso na kutoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Dia Zongo.
Zongo akiwa katika kazi za kawaida katika mtaa huo, alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa kuna mwanamke, Mariam Said, amemficha mtoto ndani ya boksi na hamfanyii usafi wala kumtoa nje.
Baada ya kupata taarifa hizo, Zongo alimtafuta mwenyeji wake, Mwenyekiti wa mtaa huo, Tatu Mgagalana na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo ambapo walimkuta mtuhumiwa, Mariam na kuanza kumhoji kuhusu tuhuma hizo.
Kwa mujibu wa Zongo, wakati mtuhumiwa akijibu maswali aliyoulizwa huku akibabaika, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa Mariam kwa nguvu, hatua iliyomuokoa mtoto huyo kutoka katika mateso ya zaidi ya miaka mitatu.
Ofisa huyo na mwenyeji wake walimkuta mtoto huyo ametapakaa uchafu uliotokana na kinyesi na mkojo, kwa kuwa boksi hilo lilikuwa chumba chake cha kulala, meza yake ya chakula na maji na choo kwa ajili ya haja ndogo na kubwa.
Hali ya mtoto huyo ilisababisha mashuhuda waliokuwa wamezunguka nyumba hiyo, kuanza kumshambulia Mariam kwa fimbo na mawe, na kumlazimu Zongo na mwenyeji wake kufanya kazi ya ziada kumnusuru mtuhumiwa kwa kutoa taarifa Polisi, huku wakijaribu kuzuia asidhurike.
Baada ya muda askari Polisi walifika na kumchukua mtuhumiwa na alipofika kituoni, inadaiwa alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa na miezi tisa baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka 2010.
Mtuhumiwa huyo alidai Polisi kuwa kwa mara ya mwisho, alimuogesha mtoto huyo Julai mwaka jana, na alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi hilo.
Mume wa mtuhumiwa huyo, Mtonga Ramadhani ambaye ni mfanyabiashara wa Soko la Mawenzi katika Manispaa ya Morogoro naye alikamatwa na katika mahojiano, alidai hakuona sababu ya kutoa taarifa za kufichwa kwa mtoto huyo kwa sababu hamhusu na wajibu wake ilikuwa kutafuta chakula tu.
Kwa sasa mtuhumiwa huyo yupo Kituo Kikuu cha Polisi mjini Morogoro na mtoto amepelekwa katika Ofisi ya Idara ya Ustawi wa Jamii.
Baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, alidai baada ya mzazi mwenzake kufariki dunia, alishindwa kumchukua mtoto wake kwa sababu tayari alishakuwa na mke.
Alidai kwa kuwa alikuwa ameoa, alikubaliana na upande wa pili wa familia ya marehemu, kuwa mwanawe huyo alelewe na mama yake mkubwa, Mariam.
Akizungumzia ulemavu wa mtoto huyo, Ofisa Ustawi wa Jamii, Oswin Ngungamtitu alisema ulemavu huo huenda umetokana na kuishi kwenye boksi tangu akiwa na miezi tisa hadi sasa bila kutolewa nje, kufanyiwa usafi wala kupewa chanjo mbalimbali ikiwemo ya polio.
Ngungamtitu alisema ulemavu huo pia huenda umetokana na kukosa lishe yakiwemo maziwa ya mama, hewa safi na upendo na kwamba mtoto huyo atakuwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo minyoo, nimonia, utapiamlo na malaria.
Kutokana na hali hiyo, Ngungamtitu alisema ofisi yake imempeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, ili akafanyiwe uchunguzi na kupewa chanjo ya kutibu magonjwa yatakayobainika.
Baada ya hapo kwa mujibu wa Ofisa huyo, mtoto huyo atapelekwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima na ikibidi atakabidhiwa kwa baba yake mzazi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, mwanamke huyo pamoja na mumewe wanashikiliwa Polisi kwa kosa la kumfanyia ukatili mtoto kinyume cha Sheria ya Mtoto ya
VIA HABARI LEO

Thursday, May 15, 2014
MWANDISHI WA HABARI AUWAWA HUKO AFRICA YA KATI
Mwandishi
huyu wa habari ameuwawa huko Africa ya kati na watu ambao hadi sasa
hawajulikani ila Ufarasa imenza Uchunguzi wa makini,
huyu ni muandishi wa 3 kuuliwa africa ya kati muandishi wa kwanza wa kigeni kuuliwa .
MTOTO WA MIAKA MIWILI AFARIKI BAADA YA KUUNGUA NA MOTO AKIWA NDANI YA NYUMBA YAO
Na Mercy
Mwalusamba
Iringa
MTOTO Christian Kipeto
(2) Mkazi wa Mafuruto kata ya Mlandege
manispaa ya Iringa amefariki dunia baada ya kuungua na moto uliosababishwa na
mshumaa
Kamanda wa
polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea majira ya
saa moja na nusu jioni ambapo moto wa
mshumaa uliokua ukiwaka ndani ya nyumba hiyo
ulindondokea
kwenye mito ya makochi na hivyo kuanza kusambaa taratibu na kumuunguza mtoto
huyo kwenye mguu wake wa kushoto na kuepelekea kifo chake.
Katika tukio
lingine wafanyabiashara wawili wilayani Mufindi katika kijiji
cha Sawala tarafa ya Ifwagi mkoani
Iringa wameuawa na wananchi wenye hasira
kali baada ya kuiba msumeno wa kupasulia mbao pamoja na puli yake uliokuwa
unamilikiwa na Joseph Kandege .
Kamanda wa
polisi Mkoani Iringa Ramadhani Mungi amethibitisha kuawa kwa wafanyabiasha hao jana majira ya saa moja usiku ambapo mmoja
alifahamika kwa jina moja la George na mwingine kwa jina Edwin Lyavule wote wakiwa
ni wafabiashara wa Mafinga
Mungi
alisema katika tukio hilo watuhumiwa wengine watano ambao majina yao
yamehifadhiwa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano Zaidi
Mwisho………………….
Monday, May 12, 2014
MAAJABU!!! Je ulijua kama Kondo la Nyuma au 'Placenta' huliwa?
Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa kutoka kwa mama akiwa tumboni.
Baadhi ya wanawake wanaamini kuwa madini yanayopitia kwa mkondo wa Nyuma hadi kwa mtoto ili kumuwezesha mtoto kukuwa huwa bado yanaweza kutumika na kwamba sio vizuri kuitupa.
Njia za kula Kondo la Nyuma
- Husagwa na kuwa majimaji kama Sharbati vile
- Inaweza kukaushwa na kutengezwa kama tembe
- Kupikwa kwa kukaangwa kama vile nyama
'Mama ale Kondo la Nyuma?'
Baadhi ya wanawake husaga kondo hilo na kunywa maji yake saa chache tu baada ya kujifungua, baadhi wanaihifadhi na kutengeza tembe ambazo wanameza na wengine wanaikata vipande vipande kwa kuweka chini ya ndimi zao.
Wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa tembe hizo zinaweza kuwapa nguvu na pia kusaidia maziwa ya mama kuongezeka.
Kampuni moja nchini Uingereza inayotengeza biadhaa mbali mbali kutoka kwa Kondo la Nyuma, hulipisha watu kati ya pauni 150 au dola elfu kumi na saba kwa kila tembe na chini ya dola hamsini kwa maji ya kondo hilo linaposagwa.
Baadhi hutengeza maji ya sharubati kwa kuichanganya na matunda
Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa na madini mengi ambayo hayapaswi kutupwa tu.
Lakini kampuni hiyo inakumbwa na kesi mahakamani ambayo huenda ikaisababisha kufungwa.
Kampuni hiyo ilishitakiwa na wataalamu wanaohofia kuwa bidhaa hizo zinaweza kuwa na Bakteria ambayo inaweza kusababisha athari za kiafya kwa wanaotumia bidhaa zinazotokana na kondo la nyuma.
Charlie Poulter, kutoka mtaa wa Reading, anaamini kuwa alipokunywa maji ya kondo la Nyuma pindi baada ya kujifungua ilimwezesha kupata nguvu.
"nilikunywa harakaharaka, kwa sababu sikutaka kutafakari kuhusu harufu na ladha yake, alisema Charlie''
"nilikuwa nimejifungua na nilihisi kuishiwa na nguvu sana na pia kwa kiasi kidogo nilijidharamau. Kwa hivyo nilihisi kuwa ikiwa nitakunywa maji hayo ingenisaidia kupata nguvu na kupona haraka,'' alisema mama Charlie.
'Kondo la Nyuma ni nini?'
Kiungo hicho hubeba hewa ya Oxygen na madini kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Pia husafirisha uchafu kutoka kwa mtoto hupitia kwa kiungo hicho hadi kwa mama.
Baada ya mtoto kuzaliwa kiungo hicho hutoka mwilini mwa mama anaposukuma mtoto au hutolewa na madaktari mama anapofanyiwa upasuaji.
Binadamu kwa kawaida hajulikani kwa kula sehemu hiyo ya uzazi. Ni kawaida kwa baadhi ya wanyama wa baharini na wanyama wengine wa kufugwa. Lakini kwa mwanmadamu , bila shaka ni jambo geni.
Nchini China baadhi ya madaktari wa kienyeji hutumia sehemu hiyo ya mwili kutengeza dawa za kienyeji lakini utamaduni huu wa watu kula Kondo la Nyuma umeanza tu kusikika katika mataifa ya magharibi.
'Je wanasayansi wanasemaje?'
Hadi leo hakuna utafiti wowote kisayansi kuhusu wanawake wanaokula Kondo la Nyuma.
CHRIS BROWN AENDELEA KUBAKI JELA
Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown ataendelea kutumikia kifungo chake kwa
siku nyingine 131 baada ya kukiri kukiuka amri ya mahakama kuhusu
kifungo cha nje alichokuwa amepewa na mahakama.
Brown amekuwa chini ya aungalizi wa mahakama tangu mwaka 2009 alipokiri kumpiga mwanamuziki mwenzake na ambaye alikuwa mpenzi wake wakati huo, Rihanna.
Mshindi huyo wa tuzo la Grammy amekuwa kizuizini tangu mwezi Machi alipokamatwa kwa kukiuka amri ya mahakama iliyomweka ndani ya kituo cha ushauri nasaha pamoja na jela.
Kifungo alichopata kuongezewa siku kinahusiana na kisa cha ugomvi kilichotokea mjini DC mwaka jana.
Brown anakabiliwa na mashitaka ya kumchapa mwanamume mmoja nje ya hoteli moja mjini Washington
Subscribe to:
Posts (Atom)