Pages

Thursday, February 20, 2014

WATOTO WALIO ZALIWA WAMEUNGANA WAREJEA NCHINI BAADA YA KUTENGENISHWA



Watoto pacha, Elikana na Eliud waliokuwa wameungana wamerejea nchini jana wakitokea India walipokuwa kwa ajili ya kutenganishwa, tayari kwa kusherehekea kumbukumbu yao ya kutimiza mwaka mmoja leo.

Waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 10:30 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Oman, wakiwa na mama yao, Grace Joel (20) ambaye muda wote alionekana mwenye furaha.

Elikana na Eliud walizaliwa Februari 20, mwaka jana wilayani Kyela, Mbeya wakiwa wameungana na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambako walipata rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Juni mwaka jana, Serikali iliwapeleka Hospitali ya Chennai, India ambako Desemba 16, mwaka jana walifanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha.

Akizungumza baada ya kutua jana, Grace alisema: “Nina furaha ya ajabu, sijui nimshukuru vipi huyu Mungu wangu, ni mkuu mno. Ninawashukuru sana madaktari wa India, ninawashukuru madaktari wa Muhimbili na sana naishukuru Serikali yangu kwa kunipa msaada huu mkubwa. Siamini kama leo ningekuwa narudi salama na watoto wangu kila mmoja akijitegemea,” alisema Grace.

“Kesho (leo) ni birthday yao, wanatimiza mwaka mmoja, ni furaha ya ajabu niliyo nayo, siwezi kuelezea. Siku nilipoambiwa watoto wangu watafanyiwa upasuaji mkubwa na watapumulia mashine kwa wiki moja, nilichanganyikiwa kwa kweli, sikutamani tena hata hiyo operesheni ifanyike ila sikuwa na jinsi zaidi ya kumwomba Mungu.”

Akizungumza uwanjani hapo, Dk Glory Joseph kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando ambaye aliongozana na watoto hao kurudi nchini alisema: “Watoto wamerejea salama na wanaendelea vizuri ila watakuwa Moi (Hospitali ya Mifupa Muhimbili), kwa uangalizi maalumu mpaka hapo madaktari watakapoona inafaa ndipo watapewa ruhusu ya kurudi nyumbani kwao Mbeya.

“Agosti watarudishwa tena India kwa ajili ya upasuaji katika njia ya mkojo na kufunga sehemu ya utumbo,” alisema.

Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema upasuaji wa watoto hao ulichukua saa 18. Katika muda huo, saa 13 zilitumika kutenganisha viungo vilivyoungana sehemu ya chini ya uti wa mgongo, sehemu ya utumbo mpana, njia ya mkojo, kibofu na sehemu ya uume, wakati saa tano zilitumika kuunganisha sehemu zilizotenganishwa.

Pacha hao walifanyiwa upasuaji na madaktari 20 na wataalamu wengine wa afya ambao walitumia saa 18 kuwatenganisha. Kiasi cha Sh100 milioni kilitumika.

Meneja wa Huduma za Wagonjwa wa Kimataifa wa hospitali hiyo, Senu Sam alizungumza na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen juzi na kusema wamefanya sherehe kwa ajili ya mafanikio ya upasuaji huo.

Sam alisema pacha hao wameonana ana kwa ana kwa mara ya kwanza, wiki tatu baada ya upasuaji... “Imekuwa faraja kuwaona wakitazamana. Eliudi alivishika vidole vya mkono wa Elikana na kuvichezea. Wanaonekana kufurahia

Thursday, February 13, 2014

KESI YA DAUDI MWANGOSI YAANZA KUSIKILIZWA


 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, Frank Leonard ( wa nne kushoto mwenye begi ndogo begani) akiwa nje ya mahakama kuu kanda ya Iringa na wanahabari wengine mara baada ya kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya Daudi Mwangnosi kusikilizwa




Waandishi wakisubiri kupiga picha ya mtuhumiwa bila mafanikio hadi wanaondoka eneo la tukio (mahakamani)

KESI ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Channel Ten Mkoani Iringa, Daudi Mwangosi imeanza kusikilizwa hii leo baada ya kilichoelezwa na upande wa mashtaka kwamba uchunguzi wake umakamilika.

Kama ilivyo ada, makechero wa Polisi wengi wao wakiwa wamavaa kiraia walikuwepo mahakamani hapa huku wakijaribu kuwazuia wanahabari kutekeleza wajibu wao.

Katika mazingira ya kutatanisha, mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo, Frank Leonard ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa alikamatwa na askari wanne waliokuwa wamevaa kiraia kwa kile kilichoelezwa kwamba alikuwa akipiga picha mahakamani wakati kesi ikiendele
Baada ya kukamatwa Leonard, alifikishwa kituo cha Polisi cha Kati mjini Iringa na kuachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi.

Akizungumza na wanahabari baada ya kuachiwa huru, Leonard alisema "wapo baadhi ya askari kwa makusudi wanataka kubomoa mahusiano baina ya wanahabari na jeshi la Polisi ambayo yanaendelea kujengwa na kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi."


Alisema kitendo cha kubambikiziwa tuhuma ndani ya muhimili wa dola unaojitegemea (mahakama) ni kitendo cha uzalilishaji kinachotaka kuaminisha umma kwamba wanahabari ni watu wasiotaka kufuata taratibu za kimahakama.

Alisema akiwa ndani ya chumba cha mahakama hiyo alikamatwa na askari hao bila idhini ya Jaji wa Mahakama Kuu wakati akizima simu yake ya mkononi iliyokuwa katika mtetemo.


"Nilikuwa nazima simu yangu hao askari hao kwasababu wanazojua wao wenyewe waligeuza suala hilo ili lionekane katika sura wanayoitaka na hatimaye wanifungulie mashtaka," alisema.


Alimshukuru Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Iringa, Ngoi kwa kumtendea haki na baada ya kupata ushahidi kufutilia mbali kesi hiyo.

Akizungumza na wanahabari, Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Dunstan Nduguru aliwashangaa Polisi kwa kuingia shughuli za mahakama.

"Hata kama mwandishi huyo angekuwa anapiga picha, haikuwa kazi yao kumkamata mpaka wapewe agizo na Jaji Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo," alisema.

Pamoja na askari hao kuwazuia wanahabari kuchukua picha mara baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani, Nduguru alisema utaratibu wa mahakama unawaruhusu wanahabari kuchukua picha kabla shughuli kabla shughuli za mahakama hazijaanza na baada ya shughuli hizo kwisha.

"Kuwazuia wanahabari kufanya kazi zao kwa utaratibu huo sio sahihi; siku nyingine mkiona kuna dalili ya kupata bugudha kama hiyo naomba mnijulishe ili niondoe mzozo huo," alisema. 

Mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Mary Shangali, Wakili wa upande wa mashtka, Adolph Maganga alisema Adolph Maganda alisema kwa kukusudia mtuhumiwa Pacificius Cleophace Simoni anatuhumiwa kumuua Mwangosi kinyume na kifungu cha sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Alisema katika tukio hilo lililotokea Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa, mshtakiwa alifyatua bunduki yake na kusababisha kifo cha marehemu, papo hapo.

Alisema siku ya tukio marehemu alikuwa Nyororo kwa ajili ya kuripoti na kutoa taarifa kwa umma juu ya mkutano uliokuwa ufanywe na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Alisema mshtakiwa akiwa mmoja wa wafanyakazi wa Polisi, waliwasihi Chadema wasifanye mkutano huo kabla wafuasi wake hawajaanza kurusha mawe kwa Polisi na baadhi yao kupata majeraha.

Kutokana na mzozo huo, wakili huyo wa serikali alisema polisi walipiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi hao kabla mshtakiwa huyo hajamfyatulia bomu marehemu.

Wakili huyo aliwasilisha ramani ya eneo la tukio, ripoti ya mtaalamu wa milipuko na ripoti ya daktari aliyechunguza mwili wa marehemu Mwangosi na gazeti la Mwananchi la Septemba 3, 2012 lililochapisha  picha ya tukio hilo katika ukurasa wa mbele kama vielelezo vinavyohusiana na kesi hiyo.

Wakili wa upande wa utetezi Lwezaula Kaijage alitaja mambo wanayokubaliana katika kesi hiyo kuwa ni jina na anuani ya mshtakiwa na kwamba marehemu Mwangosi alikufa kifo ambacho si cha kawaida.

Na kwamba mshtakiwa Simoni alikamatwa na amefikishwa mahakamani akihusishwa na mauaji hayo.

Wakili Kaijage alisema vielelezo vingine vilivyoletwa na upande wa mashtaka hawakubaliani navyo kwakuwa vinahitaji ushahidi kutoka kwa wahusika.
Jaji Shangali aliahirisha kesi hiyo mpaka kikao kingine cha mahakama kuu kitakapoitwa ili ianze kusikilizwa.

Thursday, January 23, 2014

MAHABUSU AJIPAKA KINYESI KWA LENGO LA KUWATOROKA POLISI MKOANI MWANZA

 




 Mahabusu mmoja aliyekuwa mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la jirani na Mamlaka ya maji safi na Hifadhi ya Mazingira (MWAUWASA) jijini Mwanza alitoa kioja cha mwaka kwa kujaribu kutoroka kwa kujipaka kinyesi ili asiguswe wala kukamatwa.

Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikufahamika alijimwagia kinyesi kilichokuwa kwenye ndoo iliyokuwa ndani ya sero ya Mahakamani hapo na askari alipokwenda kufungua ili kuwapeleka watuhumiwa kwenye chumba cha Mahakama kusomewa kesi yake baada ya kutajwa na karani wa Mahakama ya mwanzo, baada ya kutajwa ndipo mahabusu huyo alipopata mwanya wa kukimbia na kutoa tahadhari kwa atakaye mgusa au kumshika atakumbana na kadhia ya kuchafuliwa kwa kupakwa kinyesi.

Askari mwingine mwenye cheo cha sajenti, ambaye alikuwa akihushughulika na huduma nyingine mahakamani hapo, kwa kuwa alikuwa na uzoefu wa kupambana na mikasa na vioja kama hivyo vya mahabusu wanao kula njama za kutaka kutoroka aliamua kula naye sahani moja kwa kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata.


Baada ya kumkamata na kumrejesha katika chumba cha mahabusu mahakamani hapo, kwanza mtuhumiwa huyo aliamriwa kuzoa mtondoro wa kinyesi cha binadamu alichokuwa amejimwagia na kutapakaa chini na mara baada ya kumaliza kuzoa uchafu huo, alipelekwa kwa hakimu ambapo alisomewa kosa la kula njama za kutoroka na kukumbana na adhabu nyingine ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita (6) jela, huku kesi yake iliyokuwa ikimkabili awali ikiahirishwa.
Via Mzee wa matukio

Tuesday, December 31, 2013

WAFANYABIASHARA MWANZA WAZIGOMEA MASHINE ZA KIELETRONIKI (EFD)

"HATA BURE HATUZITAKI"

Shughuli za biashara ya maduka na huduma mbalimbali za kijamii katika jiji la Mwanza zimesimama kwa siku nzima kufuatia mgomo wa wafanyabiashara wakubwa na wa kati zaidi ya 2000, wanaopinga matumizi ya mashine za kodi za kielektroniki-EFD .

Ni sauti za wafanyabiashara wa jiji la Mwanza, wakiwa wamekusanyika katika kituo kikuu cha zamani cha mabasi cha stendi ya Tanganyika,

 kilichopo katikati ya jiji la Mwanza, huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe unaoelezea namna wanavyonyanyasika kutokana na matumizi ya mashine hizo

Baadhi ya wafanyabiashara wakizungumza kwa jazba, wamesema hawako tayari kufanya biashara kwa kutumia mashine za TRA, hata kama watapewa bure kwa madai kwamba wengi wao bado ni wajasiriamali ambao mitaji yao bado ni midogo, huku wengine wakidai kwamba TRA haijawapa elimu kuhusu matumizi ya mashine hizo zaidi ya kuwapa muda wa kuanza kuzitumia



Mgomo huo, ambao umeathiri maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na kusababisha usumbufu mkubwa kwa baadhi ya wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa, wanaotegemea kununua bidhaa mbalimbali kutoka katika maduka ya jumla yaliyopo jijini Mwanza, umemlazimu meneja wa mamlaka ya mapato ( TRA ) mkoa wa Mwanza Bw. Jeremiah Lusana pamoja na kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Bw. Ndaro Kulwijila kuutolea tamko.


Via ITV

Friday, December 27, 2013

BREAKIN NEWZZZ!!- PICHA ZAKWANZA ZA THIS SUPER STAR MODEL MBONGO KUKAMATWA NA SEMBE MACAO/CHINA

Heroin drug packer arrested in Macao (2013-12-19) 
A woman from Tanzania was arrested on  a charge of drug possession in Macao, Dec 19, 2013. Police officers became suspicious of a female passenger who had flown from Thailand to Monaco on Tuesday (Dec,17,2013). The suspect, a tanzanian National, 28 was allegadly trying to smuggle drugs into Guangzhou. Guangzhou Proivence. After undergoing an X-ray scan, the suspect excreted 66 pellets of heroin, weighting 1.1 kilograms valued 1.1 millionMacao pataca ($137,755)







SUPER STAR DIAMOND PLATZNUM ALIPOMTANGAZA RASMI MCHUMBA WAKE MUPYA JANA LIVE!!


Ilikuwa jana pale Leaders club kwenye show ya Diamond ambapo Wema Sepetu alipanda kwenye stage na kuongea na mashabiki waliofika kwenye show hiyo.
Kwenye hiyo show Diamond aliuliza,”Mnataka kumjua mchumba wangu”?
Show ilivyoendelea Diamond alitaka kuimba wimbo wa ukimwona akasema, “Naskia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani”.
Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.







Friday, December 20, 2013

MKALIMANI WA LUGHA YA ISHARA KATIKA SIKU YA MAZISHI YA MANDELA ALAZWA HOSPITALI YA MAGONJWA YA AKILI


MKALIMANI WA LUGHA YA ISHARA KATIKA SIKU YA MAZISHI YA MANDELA ALAZWA HOSPITALI YA MAGONJWA YA AKILI

Mkalimani huyo anashutumiwa kutoa ishara ambazo hazikuendana na kile kilichokuwa kikiongelewa.
Thamsanqa Jantjie “anaweza kuwa na matatizo”, amekaririwa mke wake Siziwe akisema hayo.
Wataalam wa lugha ya ishara wamemshutumu kwa kutoa tafsiri potofu wakati viongozi mbalimbali wakitoa hotuba zao kwenye mazishi ya kitaifa ya Bwana Nelson Mandela wiki iliyopita.
Bwana Jantjie amesema aliumwa ghafla ugonjwa wa schizophrenia.
Amesisitiza kuwa alikuwa ni mkalimani mwenye ujuzi wa kazi hiyo.
Chama tawala cha African National Congress,ANC, amesema imekuwa ikimtumia Bwana Jantjie kama mkalimani wa lugha ya ishara katika matukio kadha siku za nyuma na hakuwahi kulalamikiwa kuhusiana na huduma yake, kwa upande wa ujuzi au maradhi yoyote.
Bwana Mandela alifariki dunia tarehe 5 Desemba mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95 na kuzikwa Jumapili.

via Kibs 24