Thursday, March 21, 2013
ALIYEPIGWA RISASI JANA KINONDONI SOMA ZAIDI HAPA
Mpaka sasa hivi sijapata maelezo yoyote kutoka kwa Polisi Kinondoni kuhusu kijana alieuwawa kwa risasi akiwa anaendesha gari dogo kwenye foleni Kinondoni Dar es salaam march 20 2013.
Nafasi hii naitumia kumkariri mmoja wa mashuhuda wa hilo tukio akisema “ni kwenye barabara ya kutoka Magomeni kwenda Mkwajuni hii gari ilikua inashuka, kwa sababu sasa hivi kuna foleni upande wa kulia kuna magari upande wa kushoto kuna magari, pikipiki kama kawaida zikawa zinatanua katikati”
“Wakati pikipiki ya muhusika ilipotanua ghafla ilibidi dereva huyu aliyeuwawa amkwepe hivyo akagonga gari lake kwenye kingo za barabara na kupasua tairi, marehemu akatoka kwenye gari na kukutana na jamaa wa pikipiki wenye asili ya kiarabu wakaanza kubishana na kuwaambia amepasua tairi kwa sababu alikua anawakwepa wao kwa hiyo wamlipe tairi lake tu” – Shuhuda
“Wale waarabu walikua na waya flani kama za shoti, yani zinapiga shoti ndio wakawa wanawapiga kama shoti mwilini.. zikatokea purukushani Mwarabu mmoja akamwambia Marehemu nitakuua,
yule Marehemu akasema huna uwezo wa kuniua wewe… ndio mwarabu akampiga risasi ya shingo na kudondoka palepale na kufariki, majirani ndio wakachukua kanga na kumfunika, mpaka naondoka pale Polisi walikua wamefika kwenye eneo la tukio” – Shuhuda
Bado naendelea kuisubiri kauli ya polisi kuhusu hili tukio, pia nina ahadi ya kukutana na mmoja kati ya vijana waliokua pamoja na marehemu kwenye gari wakitokea gereji… nikiipata wakati wowote nitairipoti hivyo kuwa tu karibu na mimi kwenye
ALIYEUA TRAFFIC DSM AZIDI KUBANWA
Elikiza Nko
Kwa ufupi
‘’Juzi usiku tuliwahoji na mmoja wao alitudanganya, tulipomuuliza dereva wa gari hili ni nani akajibu siyo mimi nimeachiwa na mwenyewe amekimbia” alisema Kamanda Mpinga na kuongeza kuwa baada ya kumbana alikiri kuwa ndiye.
Dar es Salaam. Dereva wa gari lililomgonga na kumuua askari wa usalama barabarani, Elikiza Nko (pichani) atafikishwa kortini wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika, ilielezwa jana.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini(trafiki), Mohammed Mpinga alisema hayo jana alipozungumzia tukio hilo ambalo lilisababisha simanzi kwa watu wengi.
Mpinga alisema polisi walifanikiwa kumkamata mhusika kwa mbinu za kipolisi na kwamba kwa jana alikuwa akihojiwa ili kupata ushahidi utakaowezesha kumpeleka kortini.
Alisema dereva huyo ni kati ya wale wawili waliowakamata awali na hatimaye mmoja walimbaini kuwa ni mhusika .
‘’Juzi usiku tuliwahoji na mmoja wao alitudanganya, tulipomuuliza dereva wa gari hili ni nani akajibu siyo mimi nimeachiwa na mwenyewe amekimbia” alisema Kamanda Mpinga na kuongeza kuwa baada ya kumbana alikiri kuwa ndiye.
Kwa mujibu wa Kamanda Mpinga marehemu ameacha mume na watoto watatu. Maziko yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya Mbweni yaliyopo Manispaa ya Kinondoni na yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.
Marehemu alifariki dunia baada ya kugongwa na gari lililokurupuka kuufuata msafara wa Rais Jakaya Kikwete eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita alipokuwa katika ziara ya kutembelea mkoa huo.
mwananchi
Friday, March 15, 2013
MIAKA 35 JELA KWA KUUA BILA KUKUSUDIA NDUGU SABA WA FAMILIA MOJA
NDUGU WA SAMSON DANIEL ALIYOWATEKETEZA KWA MOTO 2010
Mahakama kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 35 Samsoni Daniel Mwang’ombe baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia ndugu wa familia moja wapatao saba.
Akisoma mashtaka mbele ya jaji wa mahakama hiyo Samwel Karua, Mwendesha mashtaka wa Serikali Rhoda Ngole alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 21, 2010 kinyume cha kifungu cha 195 (16) kilichofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.
Ngole aliiambia Mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mwaka huo majira ya 2:00 hadi saa 2:30 usiku ambapo alifika nyumbani kwa baba yake akiwa na sigala mkononi huku akiivuta na baadaye kuidondosha sigala hiyo iliyosababisha moto kuwasha nyumba.
Aliwataja walioathirika na moto uliokuwa umewashwa kutokana na sigala aliyokuwa ameidondosha mtuhumiwa kuwa ni Daniel Mwang’ombe, Anitha Richard, Salome Mwang’ombe,Jane Samson, Diana Samson, Maria George na Cloud Samson.
Kutokana na kosa hilo mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na kwamba aliua bila kukusudia ambapo alikiri kuwa akiwa anavuta sigala alidondosha kipande hicho ambacho kilikuwa bado kinawaka moto.
Aidha Mwendesha huyo aliiambia mahakama hiyo kuwa pamoja na mtuhumiwa kukiri kusababisha vifo bila kukusudia mahakama impe adhabu kali kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo Wakili wa upande wa utetezi Sambwee Shitambala alisema Mahakama inatakiwa kumwonea huruma na kumpunguzia adhabu mshtakiwa kutokana nay eye kuwa miongoni mwa wafiwa.
Alisema mshtakiwa ameondokewa na wazazi, watoto na mke katika ajali hiyo ambapo hakuhudhuria mazishi yao pia amekaa muda mrefu akiwa mahabusu ambapo amekaa kwa miaka mitatu na kuongeza kuwa mtuhumiwa ni kijana ambaye ni nguvu kazi ya taifa hivyo hastahili kufungwa.
Na Venance Matinya, Mbeya.
Sunday, March 10, 2013
JACQUELINE WOLPER ALISEMA HATOPIGA PICHA ZA UCHI MAISHANI MWAKE LAKINI SASA AMEAMUA KUJIACHIA
Hatimaye staa wa filamu za Kibongo mwenye heshima tele, Jacqueline Massawe Wolper amenaswa ‘laivu’ akiwa amepiga picha chafu inayoonesha sehemu kubwa ya nyeti zake.
Kunaswa kwa picha hiyo, kumevunja heshima ya staa huyo aliyekuwa pekee hajapiga picha ya namna hiyo kati ya mastaa wa kike wanaotamba katika tasnia ya fi lamu hapa Bongo.
Wolper alinaswa na mwandishi wetu katika sherehe ya ‘bethidei’ ya msanii mwenzake iliyofanyika hivi karibuni Ubungo jijini Dar.
Siku za nyuma, staa huyo aliwahi kukataa kupiga picha kama hiyo alipotakiwa kufanya hivyo na mwandishi wetu katika ufukwe mmoja jijini Dar.
Siku za nyuma, staa huyo aliwahi kukataa kupiga picha kama hiyo alipotakiwa kufanya hivyo na mwandishi wetu katika ufukwe mmoja jijini Dar.
Wednesday, March 6, 2013
MWENYEKITI JUKWAA LA WAHARIRI ABSALOM KIBANDA AVAMIWA NA MAJAMBAZI AKIINGIA NYUMBANI KWAKE
Mwenyekiti wa Jukwaaa la Wahariri Absalom Kibanda amevamiwa na majambazi akiwa anaingia nyumbani kwake.Amejeruhiwa vibaya ikiwa ni pamoja na kutobolewa jicho na sasa anatibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Taarifa zilizopo hivi sasa katika Taasisi ya Mifupa MOI ni kwamba hali ya Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri ABSALOM KIBANDA bado si nzuri na kwamba Jukwaa la wahariri linafanya utaratibu wa kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi
Taarifa zilizopo hivi sasa katika Taasisi ya Mifupa MOI ni kwamba hali ya Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri ABSALOM KIBANDA bado si nzuri na kwamba Jukwaa la wahariri linafanya utaratibu wa kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi
Thursday, February 21, 2013
FUNDI UMEME TANESCO ALIENASWA NA UMEME AFARIKI DUNIA
WATUHUMIWA MAUAJI YA PADRI MUSHI WAKAMATWA WAKIJARIBU KUTOROKA
*Wadaiwa kusafiri kwa Jahazi kutoka Z’bar hadi Mombasa
*Wanaswa katika usafiri wa gari wakielekea mjini Nairobi
MAKACHERO wa Jeshi la Polisi nchini wamewatia mbaroni vijana watatu wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Padri Everist Mushi (55) wa Kanisa Katoliki mjini Zanzibar.
Watuhumiwa hao wamekamatwa mjini Nairobi, Kenya kutokana na ushirikiano w...a Jeshi la Polisi la Tanzania na Polisi wa Kenya kwa mwamvuli wa Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (Interpol).
Habari za kuaminika kutoka Nairobi, Kenya zimesema kuwa watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa, walitiwa nguvuni juzi mjini humo walipowasili wakitokea Mombasa, mashariki mwa nchi hiyo.
Watuhumiwa hao ambao walikuwa wakiingia katika maficho kukwepa mkono wa dola, wanadaiwa kutumia jahazi kusafiria kutoka Zanzibar hadi Mombasa, Kenya kabla ya kusafiri kwa magari hadi Nairobi ambako walitiwa nguvuni.
Habari na Jamii Forums.
R.I.P
Subscribe to:
Posts (Atom)












