Pages

Wednesday, January 30, 2013

KESI YA TUHUMA ZA KUBAKA NA KUSABABISHA MIMBA YA MCHUNGAJI MWASUMBI MBEYA YAFUFUKA





Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi (57), Jana alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya Gilbert Ndeuluwo akituhumiwa  kumbaka na kumpa Mimba mwanafunzi.

Akisoma mashtaka hayo Mwendesha mashtaka wa Serilkali Archiles Mulisa alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya Mwezi Januari 2008 ambapo alimbaka na kumpa ujauzito Neema Boni (17) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Itende.

Mulisa alidai mahakamani hapo kuwa kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya elimu ya 5 ya gazeti la Serikali namba 265 ya mwaka 2003 na chini ya Sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978 ambapo mshtakiwa anatuhumiwa kutenda makosa mawili ikiwemo kubaka na kusababisha ujauzito.

Aliongeza kuwa kosa la kubaka ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 130(1),(2)(e) na cha 131(1) kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hata hivyo mshtakiwa huyo alikana mashtaka yote ambapo  aliachiwa kwa dhamana ya Shilingi Milioni Mbili na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka taasisi inayotambulika, kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 30 itakapoanza kusikilizwa.

kwa hisani ya Mbeya yetu








Tuesday, January 29, 2013

Na Mercy Mwalusamba
Iringa
Wanawake waendelea kutupa au kutelekeza watoto Nchini
Utupaji wa  watoto hivi sasa umekua kama fasheni kila mahali kumekuwa na kasumba hii ya kutupa watoto mara tu wazaliwapo kana kwamba ni taka ambazo ni kawaida kuzikuta jalalani
Ukatili huo hufanywa mara nyingi na wazazi ambao ama hawana mipango ya kuchukua jukumu la kuwalea watoto hao au kutokana na sababu moja au nyingine, huku wengi wakiokotwa barabarani, kwenye majalala ya taka, vyooni na wengine wakiwa wametelekezwa mahospitalini
Kila binadamu ana haki ya kuishi awe amezaliwa katika hali ya ulemavu wa aina yoyote au awe amezaliwa katika familia duni hivyo  ndivyo Mungu alivyopanga  hivyo yeye kama binadamu ana haki ya kuishi kama binadamu wengine
Wanawake wanaotupa watoto wamekuwa na visingizio lukuki pindi wanapobainika na makosa hayo na kuhojiwa kusingizia maisha magumu au kusingizia kuzaa mtoto mlemavu kukataliwa na wazazi wenzao wanaowapa mimba japo sababu hii inahusiana sana na suala lenyewe lakini si sawa na si haki kutupa kiumbe kilichoumbwa kwa makusudi ya Mungu
Suala la kutupa watoto kila mtu linamuhusu awe mwanamke ambae ndie muhusika mkuu lakini pia linamuhusu mwanaume kwasababu mtoto hutengenezwa na watu hawa wawili hivyo ushirikiano katika hili  unapaswa kuwepo kuanzia kipindi cha ujauzito hadi mtoto anapozaliwa
Japo suala la kukataa kwa mwanaume kua sie muhusika wa mimba ndio limekua limechukua nafasi kubwa lakini sitaki  kuamini kwamba ndio sababu kuu ya kumpelekea mwanamke kutupa mtoto
 Mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe huna haki kisheria huna haki ki imani wala hakuna utamaduni wa kutupa mtoto kwa kabila lolote unapaswa ujue kwamba Mungu anakushangaa na bina damu wanakushangaa kwa ukatili huo
Wanawake wanaosingizia ugumu wa maisha kwamba maisha yake magumu hana uwezo wa  kulea mtoto  uamuzi wa mwisho unaoufikia wakuamua  kwenda  kutupa mtoto  jalalani bado hutendi haki wewe una dhambi tu tena kubwa sana
Kuna baadhi ya wanawake  wanazeeka hajawahi kubeba hata ujauzito ni stori kwake anatamani hata Mungu amjaalie  kupata mtoto taahila  ili mradi tu asionekane mgumba  wengine wamekula hata vinyesi lakini ameshindwa mwingine  lakini wewe unabeba Rambo iliyowekwa mtoto kama taka taka unaenda kutupa jalalani huna tofauti na muuaji
Serikali iangalie adhabu nyingine katika hili ikiwezekana adhabu ibadilishwe na iwe kali zaidi  adhabu iliyopo haiogopwi hata kidogo
kuna njia nyingi za uzazi wa mpango na asilimia kubwa ya wanawake wana elimu hii ya uzazi wa mpango kwanini wasichukue hatua ya kuzitumia ukizingatia hazina gharama yoyote  kuzipata serikali imetoa bure
Ingekua ni vyema kuzuia mapema kama haupo tayari kwa wakati huo kupata mtoto lakini cha ajabu unalea mimba kwa miezi tisa au chini ya hapo ambapo tayari Mungu kafanya uumbaji wake mtoto anazaliwa unatupa
mapema wiki hii mtoto amekutwa ametupwa maeneo ya M.R amekutwa akiwa amekufa ndani ya mfuko wa kusafiria  kabla ya tukio hilo mtoto mwingine aliokotwa karibu na Chuo cha Tumaini University mkoani Iringa  wanawake wanaosifika kwa huruma na kuwa walezi wazuri wa familia wenye mapenzi amebadilika na kua kama mnyama
wengine wamekua wakizaa watoto wazima na kuwanyonga kisha kuwatupa hata hofu ya Mungu haipo kabisa kwao hakuna imani ya dini yoyote inayoruhusu ukatili wa namna hii labda dini ya mashetani
Na hili limekua ni chanzo cha watoto wa mitaani kwasababu baadhi yao akija kugundua ukweli wa maisha yake anashindwa kujikubali  na kuadhirika kisaikolojia na huishia mitaani
imefika wakati sasa wanawake watambue umuhimu na haki ya mtoto ya kuishi kwani wanawake wamekuwa wakibeba ujauzito na kisha kutoa mimba huku wanawake wengine wakitupa watoto wachanga pindi wanapojifungua

Wanawake waepukane na mimba zisizotarajiwa hii itasaidia kupunguza tatizo la watoto wachanga kutupwa au kunyongwa pindi wazaliwapo
Ikishindikana wafuate uzazi wa mpango hospitali inatoa huduma bure na siyo kutupa mtoto ambaye umemlea kwa miezi 9 tumboni leo hii mama anajifungua na kutupa mtoto huo ni ukatili wa hali ya juu kwa mtoto asiye na hata chembe ya hatia
..........................................MWISHO...............................................................

MTOTO ALBINO AKIWA AMETUPWA JALALANI ARUSHA

KICHANGA KILICHOTUPWA PEMBENI MWA MTO KARIBU NA CHUO KIKUU TUMAINI IRINGA


 


Monday, January 28, 2013

HATIMAYE MAHAKAMA IMETANGAZA DHAMANI KWA MWIGIZAJI LULU MICHAEL PAMOJA NA MASHARTI ANAYOTAKIWA KUYAFUATA

Mahakama kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Lulu lakini iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria,

 kutosafiri nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.

Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.

Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.


 Lulu akiwa mahakamani leo


aleshika maji ni mama yake Lulu

Thursday, January 3, 2013

MANENO YA MWISHO YA SAJUKI





Mwigizaji Dinno alikua rafiki mkubwa sana wa Marehemu Sajuki na ndio alikua analala hospitali na Sajuki pale Muhimbili.

Ameongea Exclusive na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutoa maneno ya mwisho ambayo aliyasikia kutoka kwa Sajuki akimzungumzia mke wake ambae ni Wastara.

Kwa haraka haraka mwigizaji Wastara amesifiwa sana na watu mbalimbali kwa moyo wake wa ushujaa wa ukweli wa upendo kwa Sajuki japo walipitia matatizo makubwa na mengi kwenye maisha yao.

Masanja Mkandamizaji na Arnold Kayanda ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopaza sauti zao kupitia mitandao ya kijamii kumsifia Wastara kwa moyo wa upendo.

Tukirudi kwa Dinno, namkariri akisema “tulipokuwa Arusha sisi watatu tu Sajuki alionyesha ishara ya kukata tamaa, siku moja tulikua hotelini usiku kama saa tisa hivi Wastara alikuja kuniamsha kwenye chumba changu nikaenda kwa Sajuki, alikua anaumwa sana akamwambia Wastara naomba mpigie mama niongee nae, Sajuki akamwambia mama yake mzazi kwamba Wastara nampenda sana, kanizalia mtoto mzuri anaitwa Farhini, naomba msimsumbue naomba msimpe shida yoyote amenisaidia sana, naomba mumwachie Farhini amlee amtunze mtamuona, yalikua maneno mazito sana mpaka machozi yakawa yananitoka”

Kwenye mstari mwingine Dinno amesema jambo jingine ambalo Sajuki aliliongea mwishoni ni kuhusu upendo miongoni mwa wasanii wa movie Tanzania, namkariri akisema “alikua ananiambia hebu jitahidi kuwa unakaa na wasanii, unajua sisi hatupendani Dinno ila mimi iko siku nitakuja kuropoka nikae na watu niwazungumzie tuweke upendo pamoja, tukishapendana tutafanya kitu Dinno”

Wednesday, December 26, 2012

PADRI APIGWA RISASI ZANZIBAR


Zanzibar, padri Ambrose Mkenda amepigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akifunguliwa geti aingie nyumbani kwake maeneo ya Kitomondo mjini Zanzibar.

Waliompiga risasi walikuwa kwenye pikipiki na wametokomea kusikojulikana!!!!!!!



Wednesday, December 19, 2012

MSANII WA FILAMU JUMA KILOWOKO AANGUKA JUKWAANI ARUSHA


 Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikwa na wasanii wenzake mara baada ya kuanguka jukwaani juzi ndani ya uwanja wa Sheikh Amri katika tamasha la wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wale wa filamu


Akipewa pole na wenzake waliomdaka baada ya kuanguka

Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikiliwa na wenzake wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka
 alipopewa nafasii ya kuwasalimia mashabiki wake.
 
HALI ya msanii  wa filamu nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha  mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani mara baada ya kuishiwa na nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama.

Tukio hilo lilitokea juzi jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika  ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid  wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.

Mara baada ya msanii huyo kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh” na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake.

Hatahivyo,wasanii hao walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa kupumzika zaidi.

Akihojiwa na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu zaidi.

”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
 Hatahivyo,baadhi ya mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali ya msanii huyo huku wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya wasanii wa filamu nchini walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba wanamtumia ili wapate pesa ilhali mwenzao ni mgonjwa.

Wakihojiwa kwa nyakati tofauti mashabiki hao kwa jazba walisema kwamba msanii huyo alipaswa kupewa muda mwingi wa kupumzika kuliko kuambatana na wenzake mikoani kwani hali hiyo inamchosha zaidi.

“Hawa watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu sana huyu mtu anaumwa sana sisi tunashangaa wanaambatana na mtu mgonjwa mikoani wampe muda apumzike na si kumtumia kwa kupata pesa”alisikika shabiki mmoja akiongea kwa jazba.

Picha na habari kwa hisani ya Full Shangwe Blog
 

 

MTOTO GIFT AUAWA KIKATILI KWA KUCHALANGWA MAPANGA NA BABA YAKE MZAZI

Marehemu Gift Mustafa


Kwenda kuzika


Waombolezaji msibani kwa akina Mustafa


Mama Mzazi wa Gift


Na huyu ndio baba mzazi wa marehemu Gift alieua mtoto wake Bwana Mustafa Mchele


Ni mtoto mdogo lakini alikuwa na uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo ndiyo maana alipowakuta baba na mama yake wanapigana, haraka sana alihoji sababu ya ugomvi wao, akataka waachiane.
Kumbe baba ni katili, eti swali “kwa nini baba unampiga mama”, likamuudhi, hivyo akamcharanga mapanga Gift mpaka akapoteza maisha.

Mtoto Gift, ameuawa kikatili mno, picha za tukio tumeshindwa kuzitumia kutokana na maadili, zinaonesha jinsi muuaji alivyomkatakata usoni na kichwa kizima bila huruma.
Gift, aliuawa Desemba 10, 2012, nyumbani kwao, Yombo Buza, Temeke, Dar es Salaam.

Mama wa marehemu, Zulfa Mustapha na majirani zake, wanamlilia Gift, wakimuelezea alikuwa mtoto mzuri, mwenye akili na uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo licha ya umri mdogo aliokuwa nao.
SIKU YA TUKIO
Jirani aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, Gift alikuwa anatoka madrasa, alipofika nyumbani aliwakuta wazazi wake wanagombana.
“Ni kawaida ya Gift kufuatawa na ama baba yake au mama yake pindi anapokuwa madrasa lakini siku hiyo hakufuatwa, kwa hiyo alifika nyumbani amechelewa kidogo.

“Inaonekana alisubiri kwa muda kabla ya kuamua kurudi mwenyewe. Akakuta wazazi wake wanagombana, hakujua kama amekikaribia kifo chake.
“Mama yake alikuwa analia, kwa hiyo akamuuliza baba yake ni kwa nini alikuwa anampiga mama yake. Hapohapo, baba mtu akachukua panga na kumcharanga.
“Baada ya kumcharanga mtoto, akamgeukia mkewe, akamkata mkononi na kichwani jeraha moja lakini mama mtu yeye alipata upenyo na kukimbia,” alisema jirani huyo.

MAMA ALIPONA
Ripota wetu, walifanikiwa kumuona Zulfa akiwa na majeraha mawili, moja mkononi na lingine kichwani lakini hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.
Hata hivyo, jitihada za maripota wetu kuzungumza na Zulfa ziligonga mwamba kutokana na ndugu zake kuwa wakali.
Wikiendi iliyopita, maripota wetu walifika nyumbani kwake lakini wakaelezwa kwamba ndugu zake wamemhamishia sehemu nyingine.

MTOTO AZIKWA
Gift, alizikwa Desemba 12, mwaka huu kwenye makaburi ya Yombo Buza, Temeke, Dar es Salaam.
Simanzi ilitanda kwa wakazi wa Yombo, husasan majirani wa familia ya Mustafa Mchele, kwani tukio hilo limekuwa na sura ya aina yake
Majirani wamesema kuwa Mustafa hakutegemewa na jamii kutenda mauaji hayo kutokana na asili yake ya upole na ukarimu kwa watu.
Wamesema kuwa pia ni mtu anayemjua Mungu vilivyo, kwani husali swala tano.
“Ni msomi, alikuwa akiishi na familia yake vizuri. Tuliposikia mauaji haya tumeshangaa sana, wengi wamehisi kuna mambo ya uchawi hapa,” alisema jirani huyo na kuongeza:
“Wengi wanaamini akili ya Mustafa imechezewa. Katika siku za hivi karibuni kila alipokuwa akienda kazini alikuwa akiumwa, akirejea nyumbani huwa mzima.

Jirani mwingine ambaye naye aliomba hifadhi ya jina lake, alisema: “Mustafa alikuwa anafanya kazi kwenye kiwanda kimoja kilichopo Barabara ya Nyerere lakini siku za karibuni, alikuwa nyumbani mara nyingi kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
“Kule kiwandani ni kiongozi wa wafanyakazi. Kwa nini aumwe akiwa kazini, akifika nyumbani anapona? Mbona si mtu wa ugomvi, sasa ilikuaje agombane na mkewe kisha amuue mtoto wake kipenzi? Kuna kitu hapa!”
Majirani walisema, Mustafa alikuwa anampenda mno Gift na hata siku ya tukio aliongozana naye mpaka madrasa ambako mtoto huyo alikuwa anasoma