Tuesday, December 18, 2012
Tuesday, December 11, 2012
KICHANGA CHAKUTWA KIMETUPWA KATIKA DAMPO ENEO LA MAPAMBANO JIJINI MBEYA
Wametupa tena kama taka vile........! kumbe ni binadamu wanawake hebu muogopeni Mungu kumbuka kuna watu wanazeeka hawajawahi hata kunyoshesha wala kushika mimba wanatamani siku Moja Mungu awashushie miujiza yake wapate watoto wamekula kila aina ya vitu lakini wameshindwa ,,,,,,,,kwanini,,,,,,,,,lakini jamani
WALIMU WAIOMBA SERIKALI ITENGE BAJETI KUBORESHA ELIMU ZA AWALI...!!!
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kwagunda, David Kituja
BAADHI ya walimu na wazazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe wameiomba Serikali kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kuboresha elimu ya awali ili madarasa hayo yasiwe mzigo kwa walimu wakuu.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi eneo hilo umebaini licha ya Serikali kusisitiza kila shule ya msingi kuwa na darasa la awali, baadhi ya maeneo haitoi fungu lolote kuendesha madarasa hayo.
Akizungumza hivi karibuni ofisini kwake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kwagunda, David Kituja iliyopo Kijiji cha Kwagunda Korogwe, alisema darasa la awali shuleni hapo hutumia bajeti ile ile ya shule ya msingi, jambo ambalo limekuwa mzigo kwa walimu wakuu hivyo kushauri kuongeza fungu kuboresha darasa hilo.
“Madarasa ya awali kweli ni tatizo, maana inasikitisha Serikali inasisitiza yaanzishwe kwa kila shule lakini hakuna bajeti yoyote iliyotengwa kuyahudumia...mwalimu unalazimika kubana upande wa bajeti ya msingi uitumie kwenye darasa la awali sasa hii ni changamoto kweli kweli,” alisema Kituja.
Kwa upande wake, mmoja wa wazazi, Vedastus Mhilu alisema, changamoto ya kipato kwa wazazi wengi vijijini bado ni tatizo kubwa kwa uchangiaji wa madarasa hayo jambo ambalo husababisha elimu hiyo kuendeshwa kwa kubabaisha.
“...Huku wazazi wengi ni wakulima kwa hiyo ile fedha tunayoipata haitoshelezi kuwapeleka watoto wetu kusoma madarasa ya awali au kuchangia ada na hata michango ya chakula, si kwamba hatupendi watoto wetu wapitie elimu hiyo ya awali tatizo ni kipato,” alisema Mhilu.
Aidha Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kwashemshi, Jonathan Mzava alisema kwa upande wao wameweza kuanzisha madarasa ya awali kwa ushirikiano na Serikali lakini kikwazo ni namna ya kupata walimu wa kudumu kuwafundisha watoto hao muda wote.
“Hapa shuleni ninao wanafunzi kama 100 hivi wa elimu ya awali, madarasa haya yanaendeshwa kwa msaada wa Serikali ila mwakani nafikiria kuwashirikisha wazazi ili tuweze kuiboresha zaidi...nitawaomba wachangie kiasi kidogo ili tuweze kupata walimu ambao muda wote watakuwa wanawafundisha watoto tofauti na sasa ambapo natumia walimu wa shule ya msingi,” alisema Mzava.
Akizungumzia kuhusu elimu ya awali, Kaimu Ofisa Elimu Sekondari, Shaban Shemzighwa alisema hakuna walimu wanaoajiriwa maalumu kama walimu wa madarasa ya awali hadi sasa, hivyo shule zenyewe hujitegemea kimgawanyo wa walimu kuendesha elimu hiyo.
Monday, December 10, 2012
RAY C AKITOA SHUKRANI KWA RAISI IKULU JANA BAADA YA KUPEWA MSAADA WA MATIBABU "basi sawa"
Mama yake RAY C - Bi Margareth Mtweve, Ray C na dada yake RAY C - Sara wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais Ikulu - Dar es salaam mara baada ya familia hiyo kwenda kutoa shukrani kwa msaada wa matibabu ya mwanamuziki huyo yaliyotolewa na
Rais Jakaya Kikwete.
MTOTO WA DARASA LA PILI WA SHULE YA MSINGI MBATA MKOANI MBEYA ALIEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA SHARIFU MWENYE UMRI WA MIAKA 7 AACHIWA MTOTO MCHANGA NA MWANAMKE ASIEFAHAMIKA
Sharifu 7 amesema alipokua anatoka shule mida ya saa nne asubuhi mama mmoja asiemfahamu alimwita mama huyo alikuwa amebeba mtoto mchanga ndipo akamwambia sharifu naomba nisaidie kumbeba mwanangu maramoja kwani nimesahau kuchukua kitu fulani nyumbani
sharifu bila kujua akamchukua mtoto huyo na mama wa mtoto akaondoka na kutokomea kusikojulikana sharifu anasema ilipita muda mrefu sana bila ya kumuona tena huyo mama na baadae kichanga hicho kilianza kulia na sharifu kuona mtoto analia nayeye alianza kulia
Ndipo akatokea mwanafunzi mwenzie na kumuuliza sharifu mbona unalia na mtoto analia? sharifu akamjibu mwanafuzi mwenzake kuwa kuna mama kaniachia mtoto toka saa nne mpaka sasa sijamwona nami nimechoka kumbeba ndipo mwanafunzi huyo akamwambia twende tumpeleke kwa walimu
Hata hivyo Upendo Mwakipunda mwalimu wa shule ya msingi mbata amekiri kutokea kwa tukio hilo shuleni hapo na kwamba ni kweli walimpokea mtoto huyo na kumpeleka kituo cha polisi
Subscribe to:
Posts (Atom)






