Pages

Saturday, November 17, 2012

WANNE MBARONI KUFUATIA TUKIO LA UVAMIZI PAROKIA YA ISIMANI IRINGA

Na Mercy Mwalusamba

Iringa

Kutokana na sakata la mapadre wa Parokia ya Isimani Jimbo Katoliki la
Iringa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, watu
wanne wametiwa mbaroni wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Hii inakuja siku moja baada ya mapare wawili wa Parokia hiyo kuvamiwa
nyumbani kwao na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimba za mwili kwa
silaha.

Siku moja kabla ya kuvamiwa mapadre hao watu wasiojulikana walivamia
mlinzi wa Kanisa katika Parokia ya Kihesa na kumjeruhi vibaya na kitu
kizito kichwani ndipo walipovunja milango ya Kanisa na kuiba pesa
kadhaa, baadhi ya vyombo vya ibada na kuharibu vibaya mavazi ya ibada,
vitabu na nyaraka mbalimbali kiasi cha kutotamanika tena.

Miongoni mwa vyombo vya ibada vilivyoharibiwa na watu hao ni pamoja na
Kuvunjwa Msalaba, Monstranti, Taberenakulo ndogo pamoja na kumwagwa
ovyo Hostia Takatifu.

Usiku wa kuamkia juzi watu wanaokadiriwa kufikia saba wakiwa na
bunduki, rungu na mapanga walivamia makazi ya mapadri hao majira ya
saa nne za usiku, ambapo walimpiga nne Padre Angelo Burgio ambaye ni
Paroko wa Parokia hiyo na kumjeruhi vibaya msaidizi wake Pd. Helman
Myala fedha zaidi ya shilingi 3.9 milioni na Euro 100.

Watuhumiwa waliokamatwa kuhisiana na tukio hilo wametajwa kuwa ni
Joseph Ngwale (30), Erasto Ngwale (38), Gaitan Kitwange na Anita
Mwinuka wote wakazi wa Isimani.

Taarifa kutoka kwa wananchi mmoja wa kijiji hicho mshiriki wa msako
huo ambaye alitoa taarifa hizi wa masharti ya kutataka jina lake
liandikwe alisema kuwa ,walianza kupata watuhumiwa baada ya kufanya
upekuzi  katika nyumba ya Josepha Ngwale na kupata goroli 37 na gram
100 huku ikipatikana silaha gobore iliyotumika katika ujambazi huo
ambayo kwa usiku huo ililetwa na mwanye Joseph Ngwale ili aifiche.

Tarifa hizo zilithibitishwa na  Diwani wa Kata ya Kihorogota
Costantino Kihwele ambaye alisema watuhumiwa wote wamekwisha
kufikishwa polisi ili hatua za kisheria zifuate.

Hata hivyo watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na tukio la uvamizi wa
Kanisa Kuu la kiaskofu Parokia ya Kihesa.

Kaimu wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Gwanchele Faustine alisema baada ya
kumfanyia upasuaji Pd. Angelo waliweza kutoa risasi 3 sehemu ya
kifuani ambazo zilikuwa zimekwama na kueleza kuwa hali zao zinaendelea
kuimarika.

“Jana tulimfanyia upasuaji Pd. Angelo tukaweza kutoa risasi 3 sehemu
ya kifuani ambazo zilikuwa zimekwama. Hali zao zinaendelea kuimarika
huku tukifanya jitihada za kuwahudumia” alisema Dk. Faustine.

Katika hatua nyingine Dk. Faustine alisema kuwa Mlinzi wa Kanisa la
Kihesa Bathlomeo Nzigilwa aliyejeruhiwa na watu hao bado hali yake ni
mbaya japo kuwa kuna dalili za kuweza hata kufumbua macho.

“Mlinzi wa Kanisa la Kihesa aliyejeruhiwa na kuletwa hapa hospitalini
bado hali yake ni mbaya na tumegundua kuwa alivunjika mfupa wa
kichwani kwa hiyo tunaendelea kufanya utaratibu wa kuutoa. Ila kwa leo
amekuwa na dalili za kufumbua macho kwa hiyo tunafanya jitihada za
kumpa huduma zaidi” alisema Dk. Faustine.

…………………………………….. Mwisho ……………………………

Sunday, November 4, 2012

Toilet paper zenye sura ya Obama zasambaa Florida fire station, Ni baada ya kutoka T-shirt za kumpinga Mitt Romney.

 
 
 
Yakiwa yamebaki masaa machache wananchi wa Marekani waanze kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo kwa awamu nyingine, visa na mikasa ama vituko vimezidi kutawala katika kampeni za uchaguzi huo labda ni mzuka wa kuonesha hisia za watu tofauti tofauti kwa yule wanaemsapoti na kumponda wasiyemsapoti.

Hivi karibuni watu wanaosadikika kuwa ni wapinzani wa rais Obama wametoa toilet paper zenye sura yake na T.P hizo zikasambaa maeneo ya firestation huko Florida.

Ripoti zinasema toilet paper hizo zimetolewa kujibu mashambulizi baada ya mfanyakazi mmoja wa kituo hicho cha zimamoto aliziondoa sticker zote zinazompinga Obama ambazo zilikuwa zimewekwa kwenye maeneo ya umma na sio maeneo ya watu binafsi ama mali binafsi.

Hata hivyo toilet paper hizo nazo zimeondelewa maeneo hayo na kupigwa marufuku maeneo hayo ya Florida firestation kwa sababu ni maeneo ya umma (public place) na sio maeneo binafsi.

Hivi karibuni zilisambaa T-shirt zenye maneno ya kumpinga mpinzani wa Barack Obama katika kinyang’anyiro hicho cha urais wa taifa kubwa duniani Mitt Romney, t-shirt hizo zilizotengenezwa na vizuri kwa ushirikiano wa madesigner watatu John Searles, Aaron Rhodan na Julian Streete zina maandishi yanayosomeka, “That Mitt I Don’t Like.”

Siku ya jumanne November 6, ikiwa na maana kwamba ni masaa machache tu kuanzia sasa raia wa Marekani watapiga kura kumchagua rais wa tiaifa hilo na hapo ndipo maoni ya wengi yatashinda.
 
Ni Romney ama ni Obama tena? Kura ndiyo muamuzi wa mwisho, hizi nyingine za kutoleana T-shirt na kuwekana kwenye toilet paper ni mbwembwe tu na mizuka ya baadhi ya watu ili kushawishi watu wengine kujiunga nao na kufata maoni yao.

Thursday, November 1, 2012

RIHANA NA KARRUECHE WAONA POA KUSHARE PENZI LA CHRISS BROWN!



 
Mkasa wa mapenzi yenye pembe tatu zinazowahusisha warembo wawili Rihanna na Karrueche Tran kwa 'Don’t wake me up' hit maker Chris Brown unazidi kunoga siku hadi siku na imesemekana kuwa warembo hao wako poa tu na maisha yao na ‘baby boy’ wao Chris Breezy.

Mtu mmoja ameiambia Hollywood Life, “he got them both twisted up. He is trying to get as much p-y as he can before he leaves next month.”

Chanzo hicho kiliendelea kufunguka, “Chris anawapenda kweli wote na wanajua hilo na wao wanampenda pia”, akaendelea, “it’s crazy situation. Na inafanya kazi kwao, na ni kama RiRi na K.T wako poa tu na hili, hivo ndivyo ilivyo.”

Lakini stori za mtaa kwa upande mwingine zilisema Rihanna aliogopa pale alihisi kuwa labda Chris angeenda na Karrueche T kwenye party yake kubwa ya Halloween iliyowakutanisha mastaa kibao jumatano ya wiki hii.

Mtu mmoja alisema, “ingawa the 'umbrella' hit maker RiRi alikuwa poa tu kwa kile kinachoendelea kati ya Chris B na K.T lakini hakuwa na uhakika kama Chris ataamua kwenda kwenye party yake na K.T na hii ni kutokanana tetesi ambazo zilikuwa zimetapakaa mitaani na kwenye mitandao kuwa huenda Chris akatokea pale akiwa na K.T kama kawaida. Hapo ndo utaona kweli mapenzi ya watatu hayawezekani hasa inapoonekana kuwa itabidi kukutana kwenye eneo moja.

Chis Brezzy alitangaza kuachana na Karrueche October 4, na kauli yake ilikuwa ,” nimeamua kuwa single ili nifocus kwenye kazi yangu. Nampenda sana Karrueche lakini sitaki kumuona anaoumia kwa sababu ya urafiki wangu na Rihanna. Badala yake inabidi niwe single ili Kurusu kila mmoja wetu kuwa na furaha.”

Siku chache zilizofuata Chris B alitoa video ikiwa na kauli nyingine inayoonesha kweli anawapenda wote Rihanna na Karueche na hajui afanye nini na hajui kama kweli inawezekana kuwapenda watu wawili lakini ndivyo yeye anavyojisikia, lakini mwisho wa siku ikaonekana kabisa ameamua kuhamia rasmi kwa Rihanna wake wa zamani na kumtangaza rasmi japo ndo hivyo tena hawaachani na Karrueche pia. 

Haya ndiyo yanayoitwa Triangular Love, “mapenzi ya pembe tatu”.

ABOOD YAPATA AJALI MBEYA

 
 
GARI LA ABOOD LENYE USAJILI WA NAMBA T 545 AZE LIMEPATA AJALI MAENEO YA SAE SEHEMU MAARUFU  KWA JINA LA KWA MBILINYI LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA TUNDUMA. AJALI HIYO IMETOKEA BAADA YA LORI LA MIZIGO AINA YA SCANIA LIKIWA LIMETOKEA ZAMBIA KUELEKEA DAR WAKATI WA KUTAKA KUPISHANA NA BASI HILO, NA NDIPO GARI AINA YA KENTA IKAJITOKEZA NA KUJICHOMEKA BARABARANI NA KUSABABISHA AJALI HIYO.

Tuesday, October 30, 2012

Professor Jay: Tanzania’s Hip Hop Legend



Tanzanian music has always impressed and lived up to the praise it earns from across the divide of Africa’s entertainment sector.

From the very traditional cord-based Taarab to the modern day American hip hop adaptation; it continues to be a useful source of entertainment to millions of people in and around the East African region.

Joseph Haule, otherwise known as Professor Jay, is one of the Tanzania’s biggest hip hop acts, if not the most popular in East and Central Africa.

In the last decade, Jay, widely referred to as “East and Central Africa’s finest”, has grown to become a force most hip hop acts in Tanzania look up to and respect.

Friday, October 26, 2012

MWALIMU WA CHUO CHA UFUNDI VETA MOROGORO AJINYONGA


Mwalimu wa chuo cha veta marogoro akutwa amejinyonga kataka mwambao wa mto kilakala mjini morogoro asubuhi ya leo,Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mwalimu huyo amejinyonga asubuhi ya leo kwa kutumia mkanda wa suruali.Inasemekana ameonekana subuhi ya leo mtaa wa madizini kilakala kabla tukio hilo halijatokea mchana huu..picha zaidi tembelea

Thursday, October 25, 2012

KATIBU WA BAKWATA MKOA WA ARUSHA ANUSURIKA KIFO BAADA YA YA BOMU LA MKUONO KURUSHWA NYUMBANI KWAKE NA WATU WASIOJULIKANA USIKU WA KUAMKIA LEO




Katibu wa bakwata Mkoa wa Arusha Bw. Abdulkarimu Jonjo akiugulia maumivu katika wodi ya majeruhi ,katika hospitali ya mkoa mount Meru baada ya kulipuliwa na bomu la kutupwa na mkono akiwa amelala usingizini nyumbani kwake na watu wasiofahamika majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo. Picha na Josefu Ngilisho.


KATIBU mkuu wa Bakwata mkoani Arusha,Abdulkarim Jonjo (52) mkazi wa Esso jijini Arusha,amenusulika kufa baada ya kujeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospital ya Mkoa Mount Meru baada ya watu wasiojulikana kumlipua kwa bomu la kurushwa kwa mkono akiwa amelala usingizini nyumbani kwake. 

Akiongea kwa taabu katika wodi ya majeruhi hospitalini hapo,Jonjo alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 6.30 usiku akiwa amelala baada ya kuona mwanga wa cheche dirishani kwake na kufuatiwa na kishindo cha mlipuko. 

Alisema kuwa hali hiyo ilimlazimu kuinuka kitandani