Pages

Tuesday, March 18, 2014

WACHIMBAJI WADOGO WANANE WANADHANIWA KUFA KATIKA MACHIMBO YA NYANGALATA NA KALOLE WILAYANI KAHAMA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI.

  Baadhi ya Wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Kalole wakihangaika kuwatoa wenzao wanane wanao daiwa kufariki dunia kwa kufukiwa na kifusi ndani ya shimo hilo.
 Wachimbaji wakiaangalia sehemu walipofukiwa wenzao wakati wakichimba Dhahabu katika machimbo hayo madogo ya Kalole Wilayani Kahama.

Mjiolojia kutoa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Wilyani Kahama Bw. Amir Chande akitoa maelekezo juu ya kufungwa kwa machimbo hayo baada ya maafa hayo kutokea

 Mmoja wa Wachimbaiji katika Mgodi wa Kalole akiwa katika jitihada za kuwafukuwa wenzao wanaodaiwa kufukiwa katika machimbo hayo juzi

Majeruhi ambaye alisalimika katika tukio hilo akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama akipatiwa Matibabu


via WANG BLOG

BABU SEYA, PAPII MENO NJE WAKILI WAO ANASA USHAHIDI WA KUWATOA GEREZANI




MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ anayetumikia kifungo cha maisha jela na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa kuwanajisi watoto tisa, wana furaha upya baada ya mwanga wa kuweza kurudi uraiani kuchomoza tena, wakili wao, Mabere Nyaucho Marando amezungumza na Uwazi.

KASORO HUKUMU YA MWANZO Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Marando alisema kwamba katika kesi ya Babu Seya na mwanaye iliyosikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar aligundua kuna vielelezo muhimu ambavyo havikuambatanishwa hivyo kuwa vigumu kwake kuviingiza na kuvitetea katika ngazi ya mahakama ya rufaa iliyoshindilia adhabu dhidi ya wawili hao.

Marando alisema mwanga mwingine wa kupitiwa upya wa mashitaka yao umekuja baada ya kuwepo kwa kesi mpya inayofanana na ya akina Babu Seya kwa asilimia mia moja. Alisema kesi hiyo ipo kwenye hatua ya mwisho ambapo ushindi wake utamfanya apate nguvu ya kurudi mahakamani kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa mwaka 2004.

DIRA KWENYE KESI HIYO “Kuna kesi mahakama kuu kanda moja nchini inayotetewa na wakili maarufu (jina tunalo). Hii kesi inafanana sana na ya akina Babu Seya. Uzuri wake ina dalili zote za washtakiwa kuibuka na ushindi wa kishindo. MAHOJIANO Mazungumzo kati ya Marando na Uwazi yalikuwa hivi:

Uwazi: Lakini mheshimiwa kesi ya Babu Seya si ilifika katika rufaa mara tatu na wakashindwa na ulisema hakuna namna tena, sasa itakuwaje kurejeshwa tena huko? Marando: Ni kweli, lakini ni jambo linalowezekana.

Nimesema kama hiyo kesi ninayoitaja watashinda na wanaweza kushinda, basi mimi nitaenda kwa Nguza na kumwambia wazo langu, akikubali nitaiandikia barua mahakama ya rufaa kuomba kupitiwa tena kwa yale mashitaka, nitajenga hoja.

Uwazi: Hiyo kesi unayoingoja hukumu yake inahusu nini? Marando: Inahusu kubaka na kulawiti, ni kama hii ya Babu Seya na wanawe. Hakuna tofauti. Sasa washitakiwa wale wakishinda ndipo hoja inapokuja, kwa nini vipengele vilevile viwatie hatiani akina Babu Seya wengine viwaweke huru, ndivyo inavyokuwa katika kesi. Uwazi: Ukiwaandikia mahakama ya rufaa wakakubali, majaji walewale watasikiliza ombi lako?

Marando: Hilo ni la mahakama lakini idadi inaweza kuongezwa na kufikia majaji sita au saba.Uwazi: Una hakika utashinda na kukubaliwa? Marando: Kama nilivyokueleza, ikipita ile kesi halafu mahakama ya rufaa wakakubali kupitia tena jalada, nina uhakika wa kushinda.

ANALIPWA NA NANI? Wakili huyo maarufu alisema yeye aliwatetea wanamuziki hao bure kwenye kesi yao ikiwa katika ngazi ya mahakama ya rufaa baada ya kusoma jalada lenye kurasa 1,362 ambapo aligundua kuwa kuna nyaraka kadhaa ambazo hazikuambatanishwa katika Mahakama ya Kisutu ambazo zingeweza kuwaokoa na kifungo wateja wake.

“Unajua kesi inapokuwa mahakama ya rufaa, majaji wanachofanya ni kupitia jalada si kusikiliza, hivyo haiwezekani kuambatanisha vielelezo vipya,” alisema Marando ambaye anajipambanua kuwa awali alishinda nusu kwa kuwatoa nje watoto wa Babu Seya, Mbangu na Francis Nguza ambao nao walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa moja na wafungwa hao.

HUKO NYUMA Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Addy Lyamuya aliwatia hatiani kwa ubakaji na ulawiti Babu Seya na wanawe Papii Kocha, Mbangu na Francis. Januari 27, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu hiyo.

Wakili Marando akapeleka suala hilo Mahakama ya Rufaa Tanzania ambako Mbangu na Francis waliachiwa huru na yeye kutangaza kwamba ameshinda nusu. Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka na kulawiti watoto hao kati ya Aprili na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza ya Kwaremmy, Dar es Salaam.
GPL

Thursday, March 6, 2014

KAMPUNI YA STATOIL YAENDELEA KUGUNDUA GESI BAHARI KUU


Meneja wa Statoil Tanzania, Oystein Michelsen


Kampuni ya Statoil na mshirika wake, Exxon Mobil, imetangaza matokeo mazuri ya majaribio ya gesi kwenye kitalu namba mbili katika kina kirefu cha bahari kisima cha Zafarani-2.

Kwa mujibu wa Meneja wa Statoil Tanzania, Oystein Michelsen, majaribio hayo kwenye kisima cha Zafarani-2, kimeonyesha kuwa na uwezo wa kutiririsha futi za ujazo milioni 66 kwa siku.

Alisema takwimu zilizopatikana kwenye majaribio hayo, ni muhimu kwa ajili ya kupunguza shaka inayoweza kuwapo siku za usoni kuhusu gesi iliyoko ya kina kirefu cha bahari na gesi ya kusindikwa hapa nchini.

Alifafanua kuwa majaribio ya uchimbaji yalifanywa katika kisima cha Zafarani-2 urefu wa mita 2,400 ndani ya kina kirefu cha bahari na ikiwa ni umbali wa kilomita 80 kwenda nchi kavu.

Alieleza kuwa baada ya majaribio ya kisima cha Zafarani-2 , kutafuatia uchunguzi wa kiwango cha gesi kwenye kisima cha Zafarani-3, ambacho ndicho cha mwisho kwenye utafiti katika hifadhi ya gesi kwenye kitalu namba mbili.

Alisema kutangazwa kwa matokeo ya majaribio ya kisima cha Zafarani-2 kunafuatia ugunduzi kwenye kisima cha Mronge-1 kulikofanyika Desemba 2013, ambako kunafanya ugunduzi huo kuwa kisima cha tano kwa utafiti unaofanyika kwenye kitalu namba 2.

Alisema ugunduzi huo umefanya jumla ya kiasi cha gesi iliyogundulika kufikia futi za ujazo wa kati ya trilioni 17-20 (Tcf).

Alisema kabla ya ugunduzi uliotokea kwenye kisima cha Mronge-1 kulikuwa na ugunduzi mkubwa gesi wakati wa uchimbaji wa awamu ya kwanza kwenye kisima cha Tangawizi-1, Zafarani-1 na Lavani-1, na ugunduzi mwingine kwenye kisima cha Lavani-2.

Kampuni ya Statoil ina leseni ya kufanya utafiti katika kitalu namba mbili kwa niaba ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), ikiwa na asilimia 65 wakati mbia wake kampuni ya ExxonMobil Exploration and Production Tanzania Ltd ikichukua asilimia 35.

Kampuni ya Statoil imekuwa Tanzania tangu mwaka 2007, ilipopewa leseni na serikali kwa ajili ya kufanya utafiti kwenye kitalu namba 2.


VIA: NIPASHE

Tuesday, March 4, 2014

JAMAA AAMUA KUKATISHA UHAI WAKE KWA KUJICHINJA NA SIME NDANI YA BUS


  UNAWEZA kudhani hii ni hadithi lakini ni kweli yametokea na hili linadhihirisha wazi kazi mbaya za shetani kwa binadamu  kwasababu katika hali ya kawaida hata kama umedhamilia kujiua huwezi kutumia njia hii ya mateso na machungu  katika kukatisha uhai wako

 

Dereva na abiria wa basi la Manchester ambalo namba yake haikujulikana mara moja, lililokua likitoka Lindi kwenda jijini Dar es Salaam walijikuta wakiangua vilio baada ya kumuona mwenzao akijichinja hadi kufa kwa kisu ndani ya gari hilo.
 Ujumbe kabla ya kifo: Kijana aliyejichinja ndani ya basi akiandika ujumbe kabla ya kukata roho. Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa tisa alasiri, Jumatano wiki iliyopita mara basi hilo lilipofika katika hoteli moja ya Nangulukulu kwa ajili ya kupatia chakula.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya abiria walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa  mara walipofika katika hoteli hiyo, kila mmoja alitawanyika kwa lengo la kujipatia chakula na baadhi yao walienda maliwatoni akiwemo marehemu huyo.
 

 Msaada:...Kijana huyo akitolewa kwenye basi baada ya kujichinja kwa sime. Walisema kwamba  marehemu huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, wakati wa kushuka hakuonekana na kisu aina ya sime lakini baadaye abiria wachache waliotangulia kwenye gari, walimshuhudia akiwa ameshika sime hiyo mkono pasipokujua aliipata wapi.
“Hata sisi tulishangaa kumuona akiwa karibu  na usukani wa dereva huku akizamisha sime tumboni kisha kuichomoa  na kujichinja shingoni  hadi pale alipokuwa akivuta koromeo na kuning’inia.

 Damu kila mahali: ...Akiingizwa katika gari lingine huku damu zikiwa zimetapakaa. “Tulichanaganyikiwa kwani ni kitu ambacho hatukukitarajia na wala hatujawahi kushuhudia tukio kama hilo la mtu kujichinja hadharani, tulibakia kutokwa machozi huku akina mama wakipiga yowe, hakuna mtu aliyethubutu kumsogelea kumuokoa kwani kila mmoja alimuogopa.
“Tulishindwa kupanda basi hilo kwani ni tukio la ajabu pia ndani kwa mbele kulikuwa kumetapakaa damu, ghafla alidondoka chini ndani ya gari, aliomba kalamu na karatasi ili kuandika ujumbe.

 Polisi akiwa na sime aliyotumia kujichinja kijana huyo. “Dereva alichukua kalamu na kipande cha karatasi na kumpa, alianza kuandika  huku damu ikimbubujika tumboni na shingoni, ''hatukujua alichokiandika, aliishiwa nguvu taratibu akadondoka''.
“Abiria walimsogelea na kumuinua na walimueleza kuwa atubu kwa Mungu kosa alilolifanya kabla hajafa, alipiga magoti na kuomba,  ghafla alidondoka tena.

 Kijana akisali kabla ya kukata roho. “Kaka yake ambaye alikuwa akisafiri naye kuelekea Dar es Salaam alichanganyikiwa kwani hakutegemea kuwa mdogo wake angejiua, kwani alisema hana historia ya kuugua ugonjwa wa akili. Polisi walipigiwa simu na walifika kumchukua lakini baada ya muda mfupi akawa amefariki dunia.
“Sisi abiria wengine tuliendelea na safari kuelekea Dar es Salaam  ambapo marehemu na kaka yake walibakia huko  mkoani Lindi.


Kifo:...Kijana huyo baada ya kukata roho. “Mara tulipofika Dar es Salaam dereva alitusihi tukae kimya kwa dakika moja na kuomba kutokana na tukio lililotupata, tulifanya hivyo baadaye kila mmoja alitawanyika na kuelekea kwake,” kilisema chanzo kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alipoulizwa mwishoni mwa wiki iliyopita kuhusiana na tukio hilo alikiri kutokea.
“Ni kweli tukio hilo lilitokea lakini kwa sasa sina data kwani nipo njiani nikitokea Nairobi, Kenya kikazi kuelekea Lindi, mara nitakapofika huko ofisini ndipo nitapata tukio zima lilivyokuwa,” alisema Kamanda Mzinga.

Tuesday, February 25, 2014

FAHAMU MADHARA YATOKANAYO NA KINYWAJI KINACHOPENDWA NA VIJANA WENGI RED BULL

 RED BULL Imekua ikiuzwa katika maduka  makubwa (Supermarkets) na maduka madogo (Retail Shops) katika nchi ya Tanzania na watu wazima na watoto wetu wengi wana mazoea ya kunywa kinywaji hiki ambacho kinaweza kusababisha kifo! Kemikali zinazopatikana katika kinywaji cha RED BULL zilitengenezwa maalum katika maabara za kijeshi za Marekani kwa ajili ya kutuliza mzuka wa maaskari wao wakati wakitekeleza mauaji ya kikatili sana dhidi ya wananchi wa Vietnam miaka ya sitini na sabini.
Kemikali hizo zilitumika pia kama dawa ya kuwazindua watu waliozirai (“stress coma”).Hazikukusudiwa kutumiwa kama kinywaji au kilevi cha kawaida! Duniani kinywaji hiki (RED BULL) huuzwa kama kitu chakuleta msismko (Energizer Drink) na matangazo yake yanataja sifa zake kama ifwatavyo.

Ni kinywaji kinachompa mtu nguvu ya kustahimili na umakini. Humpa mtu kasi ya vitendo” ... na kadhalika.RED BULL imesambaa katika nchi 100 kwa mpigo (nchi masikini!). Na matangazo yake kuwalenga vijana na watoto, hasa wanamichezo. Hawa ni rahisi kushabikia kinywaji hiki kibaya na kudhurika kiafya baadaye.



Katika hali yake ya matumizi ya sasa kinywaji hiki kiligunduliwa na Mjerumani Dietrich Mateschitz ambaye alikikuta huko Hong Kong kikiwa ni mojawapo ya madawa yaliyotumika katika kutengeneza dawa ya kupigia mswaki  meno.
Dawa hiyo ilitengenezwa kwa kemikali ambazo zina kafeni na taurini(“caffeine and “taurine). Mjerumani huyo aliona vijana wajinga wa huko wakishabikia unywaji wake akaona mwanya wa kufanya biashara na akafanikiwa kukileta ulaya.

ATHARI ZA KUNYWA RED BULL
Kinywaji kinachotengenezwa na kusambazwa leo hivi kina kemikali mbaya iitwayo “Glucuronolactone”, kemikali hatari ambayo ilitengenezwa na idara ya jeshi la Marekani wakati wa vita na Vietnam kwa ajili ya kutuliza mvurugiko wa mwazo wa maaskari wake uliotokana na mauaji ya kinyama waliokuwa wanafanya huko Vietnam. 
Kwa sababu ya madhara makubwa ya kinywaji hiki nchi za FRANCE na DENMARK zimepiga marufuku kinywaji hiki na kibatiza jina la “MKOROGO WA UMAUTI”. Katika nchi hizi, utafiti uligundua kuwa maaskari wa Marekani waliotumia kinywaji chenye kemikali ya “GLUCURONOLACTONE” waliishia kupata madhara ya maumivu makali ya kichwa, uvimbe wa ubongo na hata ugonjwa wa ini (Migraines, Cerebral tumours and liver diseases). Ni kwa sababu hiyo wamarekani waliacha kuwapa maaskari wao hicho kinywaji katika miaka ya sitini na sabini.

Jambo la kushangaza ni kuwa lebo ya RED BULL inaonyesha wazi kuwa kinywaji hiki kimetengenezwa kwa kemikali hatari ya “GLUCURONOLACTONE”! Ni kwasababu hiyo serikali za Denmark na Ufaransa nazo zikapiga marufuku unywajiwa RED BULL.


Pamoja na wauzaji wa RED BULL kuweka bayana kuwa ndani mwake mna hiyo kemikali hatari, lebo ya RED BULL hailezi madhara makubwa yanayoletwa na kemikali hiyo. Madhara ambayo hayakuwekwa bayana kwa mnywaji ni kama yafuatayo:

Ni hatari kwa mtu ambaye hafanyi kazi au mazoezi mazito sana kukitumia kwani kina tabia ya kuongeza msukumo wa damu na kasi ya mapigo ya moyo kiasi kwamba mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa moyo.
Mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa damu kuvuja ubongoni kwani REDBULL ina kemikali zinazoifanya damu iwe nyembaba ili moyo upate kusukuma damu nyingi bila kutumia nguvu nyingi. Ni hatari kuchanganya RED BULL na pombe ya aina yoyote kwani mchanganyiko wake huwa ni sumu (“Deadly Bomb”) inayoathiri musuli wa ini la mtumiaji na kuiacha katika hali ambayo haitapona kamwe. RED BULL ina vitamini B12 kwa wingi, vitamini ambayo hutumiwa kama dawa ya kuwazindua wagonjwa mahututi. Matumizi ya vitamini hii katika watu wazima ina athari za kuleta shinikizo la damu na humfanya mtu ajisikie kama mlevi. Unywaji wa RED BULL mara kwa mara huvuruga mfumo ya neva za fahamu na husababisha maradhi mithili ya mfadhaiko wa akili usioponyeka.HITIMISHO: :RED BULL ni kinywaji HATARI SANA ambacho hapana budi kipigwe marufuku katika nchi zote zinazoendelea kwani ni dhahiri kimetengenezwa na kusambazwa ili kiathiri afya za wananchi wasiojiweza wa nchi hizi masikini. Kwa kuwa wengi katika nchi hizi hutumia pombe za kila aina ni wazi kuwa kinywaji hiki kina lenga kuwamaliza – kana kwamba ukimwi uliobuniwa na hao wabaya wetu hautoshi! 
credit jamii forums

ATIWA MBALONI KWA KUUZA NYAMA YA BINADAMU



 
Mkazi wa Kijiji cha Kihinga, Kata ya Bugarama wilayani Ngara mkoani Kagera(jina tunalo), anashikiliwa katika kituo kidogo cha polisi cha kata hiyo baada ya kutuhumiwa kuuza kilo moja ya nyama ya binadamu kwa Sh100,000.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kihinga, Hassan Mohamed alisema kuwa jana saa mbili usiku, wananchi walipeleka fedha nyumbani kwake kununua nyama hiyo na alipowaona alikimbia na wananchi hao kwa hasira walimkimbiza ili kumuua na hapo hapo kuunguza nyumba yake.

“Mgambo ndio walimnusuru asiuawe na wananchi wenye hasira kali na alikimbizwa kituo kidogo cha polisi Kata ya Bugarama ili kuokoa maisha yake “.

 Kamanda wa mgambo wa kijiji hicho, Emanuel Kaloli alisema wananchi waliandamana baada ya kusikia taarifa za kuwapo mtu anayeuza nyama ya binadamu na kutaka kuhakikisha ukweli huo.

Alisema baada ya wananchi kufika, walianza kumshambulia na kutaka kumuua, lakini wanamgambo wa kitongoji walifika kisha kumuokoa mtuhumiwa na hatimaye kumfikisha kituo cha polisi kwa ajili ya usalama wake.

“Kijana aliyefahamika kwa jina la Man Balyamwabo mkazi wa Shina la Kalenge katika kitongoji hicho, ndiye aliyeambiwa kuwa angeuziwa nyama hiyo ya binadamu na kuleta taarifa katika uongozi wa kijiji ili uweze kuchukua hatua zaidia”.Alisema Kaloli.

Alisema nyumba aliyounguziwa pamoja na mali iliyokuwamo ndani hasa maharage, mavazi na vitu vinginevyo inakadiriwa kuwa na thamani ya Sh2.6milioni. Pamoja na kuwepo kwa tukio hilo, baadhi ya wananchi walisema mtuhumiwa inasemekana ni raia wa nchi jirani ya Burundi na alianza kuishi katika kitongoji hicho tangu mwaka 1981 kama kibarua wa kilimo kwenye mashamba.

Taarifa zinasema kuwa katika kuishi kwake na ndugu yake aliyefahamika kwa jina la Kahungu walikuwa wakituhumiana kwa uchawi na ilifikia mahala wakatofautiana na kaka yake ambaye alirejea kwao.

Polisi wilayani Ngara imethibitisha kumpokea mtuhumiwa huyo na kwamba linafanya mahojiano ya kina kwa kushirikiana na viongozi wa kijiji ili kubaini ukweli wa tukio hilo.