Pages

Monday, December 16, 2013

MANGI AAMUA KUTIA KIBERITI NYUMBA YAKE BAADA YA KUBAINI ANASALITIWA NA MKEWE





Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Dar wakishuhudia nyumba hiyo ikiteketea kwa moto.
Segerea, Dar Es Salaam, Nyumba moja iliyopo Mtaa Ugombolwa Kata ya segerea Jijini Dar imeteketea kwa moto mara baada ya baba wa familia ya nyumba hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Hali hiyo imetokea usiku huu majira ya Saa tano Kasoro usiku katika Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam ambapo inasemekana baba wa familia hiyo alichukua uamuzi huo mara baada ya kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi huo wa kuitia moto nyumba hiyo.
Mmoja wa shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa Wachaga wana matatizo sana Ebu Ona Sasa mwanaume Mzima Anateketeza Nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya Shilingi kisa Mkewe anatembea nje ya ndoa Sasa ona watoto wake wataishi wapi?..watu wengine ni wajinga sana Kama mwanamke anatembea nje ya ndoa si umpe talaka tu" alisikika akiongea Shuhuda huyo.

Hakukuwa na dalili zozote zile zilizokuwa zikichukuliwa kwaajili ya kupambana na moto huo huku ikiwa haijafahamika kama wakati nyumba hiyo ikitiwa kiberiti familia ya huyo baba ilikuwepo ndani ya nyumba au laah huku ikikadiriwa kuwa mali zote zilizomo ndani ya nyumba hiyo zimeteketea kwa moto kwani mpaka tunaondoka hakuna kikosi cha zimamoto kilichofik eneo la tukio wala majirani hawakuonyesha dalili zozote zile za kuuzima mot huo.

Mpaka tunaondoka eneo la tukio hakuna taarifa yoyote ile ya majeruhi wala watu kupoteza maisha katika ajali hiyo ya moto.


Friday, December 13, 2013

MAJAMBAZI WAMVAMIA MWANAJESHI WA JWTZ NA KUMRUSHIA RISASI LIVE ONA HAPA!!

 Polisi Kinondoni anasema ‘December 11 2013 saa nane mchana maeneo ya Maringo roundaboutJaphet Mriga ambae ni Mwanajeshi wa JWTZ Lugalo akiwa na mwenzake ambae ni mfanyabiashara Abdul Zacharia, walikua wanatoka bank ya NMB Mlimani City ambapo Mwanajeshi huyu alichukua shilingi milioni tisa kwa dhumuni la kumpatia Zacharia ili amnunulie gari Zanzibar’

‘Sasa walipofika maeneo ya Maringo walivamiwa na Majambazi watatu wakiwa na pikipiki na walifanikiwa kumpora Mriga fedha na katika purukushani walimjeruhi Mwanajeshi huyu kwa risasi kwenye paja na kiganjani, wakati yote hayo yakiendelea Majambazi hawa walipigana risasi wao kwa wao ambapo jambazi mmoja alipigwa risasi kwenye mbavu upande wa kulia na kufariki papohapo na kupatikana akiwa na bastola moja yenye risasi 6′ – Kamanda
Kwa kumalizia, Kamanda amethibitisha kukamatwa kwa pikipiki moja iliyokua ikitumiwa na Majambazi ambapo msako mkali unaendelea kuwatafuta wale Majambazi wengine waliotoroka wakiwa na silaha nyingine ambayo ndio imemuua Jambazi mwenzao na kumjeruhi Mwanajeshi Mriga ambae alipata matibabu hospitali ya Lugalo na sasa anaendelea vizuri.

 Mwili wa jambazi alieuawa



 Pikipiki ilikua ikitumiwa na jambazi



 Mwanajeshi alejuruhiwa vibaya

Baadhi ya wanchi wa eneo hilo wakishangaa



Tuesday, December 10, 2013

WOSIA WA MANDELA WAZUA MJADALA MZITO....!!


Marehemu Nelson Mandela enzi za uhai wake.
Mwandishi Wetu na Mitandao
WOSIA aliowahi kuuandika hayati Nelson Rolihlahla Mandela ‘Mzee Madiba’ au ‘Tata’ (95) enzi za uhai wake akielezea anavyotaka azikwe, ndiyo tishio kubwa lenye utata kuelekea siku ya mazishi yake, Jumapili ijayo, Ijumaa Wikienda limebaini.
Mtandao mmoja nchini humo umeukumbushia wosia huo huku familia ikianza kuonesha misimamo tofautitofauti, hali inayoashiria kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana.

Gari lililobeba mwili wa Nelson Mandela.
FAMILIA INAVYOTAKA
Habari za ndani zilisema kuwa familia inataka mazishi ya kiongozi huyo maarufu duniani yawe makubwa na ya kisasa kwa vile viongozi wa nchi mbalimbali duniani watahudhuria.
“Mandela ni kingozi mkubwa sana duniani, mazishi yake lazima yawe makubwa pia ya kisasa. Hawezi kuzikwa kama mwananchi wa kawaida,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo. 

Mmoja wa waombolezaji akigusa picha na Mandela.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa wakati familia hasa wajukuu na watoto wake wakishikilia msimamo huo, wapo wanandugu wanaotaka azikwe kama alivyoandika katika wosia wake huo.
SERIKALI YAPANGA MAMBO BILA KUFUATA WOSIA
Habari zaidi zilisema kuwa Serikali ya Afrika Kusini inajitahidi kuupangua wosia huo kwa kuendelea na maandalizi ya mazishi kama haukuwahi kuwepo licha ya kwamba jamii ya watu nchini humo inaheshimu wosia wa marehemu.
WOSIA UNAVYOSEMA
Mzee Madiba alishauandika wosia huo kwenye karatasi moja tu ambapo aliagiza anavyotaka azikwe. Alisema kuwa akifa azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake katika Kijiji cha Qunu, Eastern Cape huko ‘Sauzi’.


Waombolezaji wakiweka maua katika sanamu la Mandela.
ALITAKA MAZISHI YA KAWAIDA SANA
Inadaiwa wosia huo aliuandika Januari, 1996 wakati bado akiwa rais ambao ulijaa maelekezo yote juu ya mazishi yake. Aliagiza kufanyiwa mazishi ya kawaida sana yenye hadhi ya raia wa kawaida nchini humo hivyo kuyafanya kuwa makubwa na ya kifahari ni kukiuka wosia wa mzee.
KABURI ALILOLITAKA MANDELA
Katika wosia wake huo uliotolewa na rafiki yake wa karibu, Mzee Madiba aliandika kuwa akifa azikwe katika eneo la familia lenye makaburi ya ukoo wa Mandela kijijini hapo.
Pia aliagiza kuwa kaburi lake liwekewe jiwe la kawaida kama alama ya mahali lilipo ili lisije kupotea kwa mvua au mabadiliko ya tabia nchi.


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
KABURI LISISAKAFIWE
Katika tafsiri ya maneno hayo, Mzee Madiba alitaka kaburi lake liwe la kawaida sana, akimaanisha lisijengewe kama ilivyokuwa kwa makaburi ya viongozi wengine wa mfano wake barani Afrika kama, Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Kamuzu Banda (aliyekuwa Rais wa Malawi).
WOSIA WAKE ULIKUWA WA UPANDE MMOJA WA KARATASI
Magazeti ya nchini humo, South African Mail na Guardian miezi ya karibuni yaliripoti kumnukuu rafiki huyo wa siku nyingi wa familia ya Mandela akisema: “Madiba hakuwahi kukifanya kifo kuwa jambo kubwa la kufikiriwa, pia hakuwahi kutaka chochote cha fahari wakati wa kumzika.” 
Cha ajabu, wosia huo wa Mandela ulitosha kwenye upande mmoja wa karatasi ya kawaida ya kuandikia licha ya kwamba mauzo ya kitabu chake cha Long Walk to Freedom na michoro yenye jina lake vilimpatia mamilioni ya fedha.


elson Mandela (kulia) akiwa na Mwalimu Julius Nyerere enzi za uhai wao.
FAMILIA YACHUKIZWA NA WOSIA
Wosia huo ulielezwa kuwashangaza watu wengi duniani kwani waliamini angekuwa na vitu vingi vya kuandika kulingana na uwezo wake.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, SABC, suala hilo la sehemu atakayozikwa Mzee Madiba liliiudhi mno familia yake akiwemo yule mjukuu wake ambaye ni chifu, Mandla Mandela aliyewahi kufikishwa kortini kwa kuhamisha makaburi hayo ya ukoo na kuyapeleka sehemu nyingine. Pia ndiye msemaji wa familia ya Mandela.
DUNIA YAMKATALIA
Baadhi ya wanaharakati ulimwenguni kote walisema wosia huo unapingana na matakwa ya dunia nzima, ambapo walitaka maziko ya mzee huyo yawe  makubwa na ya kihistoria ambayo hayajawahi kutokea.Ilifahamika kwamba dunia inataka mazishi hayo yavunje ile rekodi iliyoshikiliwa na mazishi ya Papa John Paul II aliyefariki dunia Aprili 2, 2005.


Mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla Mandela.
SAFARI HII HAKUKIMBIZWA HOSPITALI
Mzee Madiba ambaye alitimiza umri wa miaka 95 Julai 18, mwaka huu, alikuwa hospitalini kwa karibu miezi  mitatu nyuma akitibiwa maambukizi kwenye mapafu huku akipumulia mashine. Baadaye alipata nafuu na kurudishwa nyumbani ambako usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita aliugua ghafla na kufariki dunia.




Thursday, November 28, 2013

WARAKA HALISI WA MKAKATI WA MADILIKO 2013 CHADEMA UTATA 

Utata mkubwa umeibuka kuhusu waraka halisi wa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ uliosababisha Zitto Kabwe kuvuliwa wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika Novemba 20 - 22, mwaka huu.

Baada ya juzi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika kuwaeleza wanahabari kuwa waraka uliochapishwa katika magazeti na mitandao ya kijamii, siyo halisi, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba amejitokeza na kuutetea huku akidai kwamba huo unaodaiwa na uongozi kuwa ndiyo halisi umeghushiwa.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alivuliwa uongozi pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na Mwigamba kutokana na madai ya kuandaa waraka huo ambao Chadema kimesema ulikuwa unaeleza mbinu za uasi za viongozi hao ambazo zingetumika wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho jambo ambalo ni kinyume na katiba, sheria na itifaki zake.

Katika tamko alilotoa jana, Mwigamba alidai kwamba

kuna njama zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa Chadema ili kuubadili waraka halisi wa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ kwa lengo la kupoteza maana yake, huku akisisitiza kuwa waraka halisi hauna tatizo lolote.

Katika madai yake, Mnyika alisema waraka huo unaosambazwa na kuchapishwa, si ule uliowasilishwa na kujadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu na kuahidi kuutoa waraka halisi ambao una mambo makubwa na mengi zaidi.

“Waraka utakaotumika katika mashtaka yao siyo huo. Sisi tutautumia ule ambao uliwasilishwa katika Kamati Kuu ambao una mambo makubwa na mengi zaidi kuliko huo unaochapishwa sehemu mbalimbali, ikibidi tutautoa huo waraka halisi,” alisema.

Hata hivyo, jana Mwigamba alisema waraka halisi ni ule ambao upo katika kompyuta mpakato (Laptop) aliyonyang’anywa na wanachama wa Chadema, Oktoba 25, mwaka huu, katika mkutano mjini Arusha.

“Waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ni sahihi neno kwa neno kama nilivyousoma katika magazeti ya jana (juzi), pamoja na nakala iliyopo katika mtandao wa kijamii wa Jamii Forums.”

Aliongeza: “Ili kuthibitisha kwamba waraka ule ndiyo wenyewe, nawatumieni ‘soft copy’ kutoka kwenye kompyuta yangu kwani waraka huo uliibwa kutoka katika kompyuta hiyo ambayo nilirudishiwa baada ya wao kuikagua na kukuta waraka huo halisi.”

Mwigamba alisema waraka wake unatofautiana kwa kiasi kikubwa na ule ambao Chadema kinasema kuwa ndiyo halisi: “Lissu na wenzake wana mpango wa kuuchakachua waraka huu, lakini wamekwama.”

Alisema kuandaa waraka huo siyo uhaini kama ambavyo imekuwa ikielezwa na viongozi wa Chadema na kusisitiza kuwa ni waraka wa kusaka ushindi katika uchaguzi halali ndani ya chama hicho uliopangwa kufanyika Desemba mwaka huu na baadaye kusogezwa hadi Juni mwakani.

“Wakati wa uchaguzi si ajabu kuwepo kwa wanachama wanaounga mkono wagombea tofauti. Nimekuwa karibu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa miaka mingi, najua hata yeye ana mikakati na wanaoshiriki mkakati wake ni Lissu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema,” alisema.

Alisema anashangazwa kwa kitendo cha Chadema kuusambaza waraka huo, wakati ulikuwa ni mpango wa siri kati yake, Dk Kitila pamoja na mtu mwingine anayetajwa kwa jina la M2.

“Baada ya kugundua madhara ya kusambaza ovyo waraka huo, sasa wameamua kuukana, waraka wangu ni sahihi na unaeleza ukweli. Binafsi nimefanya kazi ofisi ya makao makuu ya chama kama Mhasibu Mkuu ningeweza kuanika mengi lakini sijafanya hivyo kwa masilahi ya chama,” alisema na kuongeza:

“Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia Zitto na tangu siku nyingi walipanga kumfukuza. Nawashauri watafute sababu nzuri za kumfukuza uongozi na hata uanachama. Zitto hahusiki na mkakati huu pamoja na kwamba alikuwa ndiye mhusika mkuu, alikuwa hajui lolote.”

Jumamosi iliyopita, mama yake mzazi Zitto, Shida Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema waraka huo ulikuwa umeongezwa maneno.

“Hata ule waraka uliongezwa maneno baada ya baadhi ya wanachama kumpora Mwigamba `laptop’ yake alipokuwa mkoani Arusha katika kikao cha Chadema,” alisema bila kutaka kufafanua ulibadilishwa vipi, licha ya kuwataja kwa majina waliohusika kuubadili wakiwamo wabunge wawili wa chama hicho na viongozi wa ngazi za juu.

Sitoki Chadema

Kuhusu hatima yake ndani ya Chadema, Mwigamba alisema hana mpango wa kuondoka hata baada ya kuvuliwa uongozi, huku akisisitiza kuwa hakusudii kuomba radhi kutokana na kuandaa waraka huo.

Alisema hakusudii kuhama kwa kuwa ana historia ndefu na Chadema na anaamini kuwa ndicho mkombozi wa Watanzania.

“Nimekuwa kiongozi wa kata, wilaya, mkoa hadi taifa. Nimetumia muda wangu mwingi na hata kuhatarisha maisha yangu kwa ajili ya chama hiki, siwezi kuondoka kutokana na tofauti za kimitazamo na viongozi wangu,” alisema.

Mwigamba, ambaye alikuwa mfanyakazi katika Mahakama ya Kimataifa inayosikiliza Kesi za Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (ICTR) na baadaye kujiondoa ili ajikite kwenye siasa, alisema ana imani yanayotokea sasa katika chama hicho yatapita salama.
Mwananchi 

VIA UDAKU SPECIALLY

BABA KANUMBA ATOA MPYA>>>>>>>>>>>>

KAMA KUNA WANAWAKE WANAO TAKA KUZAA NA MIMI WAJITOKEZE"BABA KANUMBA"

ABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa amefunguka kuwa baada ya kutangaza kuwa wanawake wanaotaka uzao wake wajitokeze azae nao, wamejitokeza kumi lakini akawapa masharti, yakawashinda.

Akizungumza na mwandishi wetu, baba Kanumba aliweka bayana kuwa warembo hao waliojitokeza aliwapa sharti la kwenda kupima Ukimwi lakini ajabu wote waliingia mitini.
“Wamejitokeza vizuri lakini nashangaa wote wamekuwa wazito katika suala la kupima Ukimwi wameingia mitini, kama wapo wengine watakaolimudu sharti hilo, nawakaribisha,” alisema baba Kanumba 



VIA UDAKU SPECIALLY