Pages

Tuesday, June 4, 2013

BREAKING NEWS: Hatimaye Mwili wa Mangwea Wawasili Jione Picha hapa









 Mwili Ukipelekwa kuhifadhiwa Mochwari

 








DIAMOND THE PLATNUMZ BATA KWANZA MSIBANI BAADAE


SUPER MEGA STAR DIAMOND PLATZNUM ATOA MUPYA WAKATI WENZAKE WOTE WAPO AIRPORT KUPOKEA MWILI WA NGWAIR YEYE!!.......!!!

KIFO CHA ALBERT MANGWEA FURAHA KWA DIAMOND, APONDA MARAHA BAHARI YA HINDI WAKATI WASANII WENZAKE WAKISUBRI MWILI WAKE AIPORT



CHAMPAGNE
 akiendesha boti la kifahari katika bahari ya hindi jijini Dar es salaam na rafiki zake.

KULA BATA

JERRY MURO AZIDI KUBANWA NA SERIKALI





MIAKA miwili imepita tangu Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Frank Moshi alipo andika hukumu iliyomwachia huru aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC1), Jerry Murro na wenzake wawili,Edmund Kapama maarufu kama ‘Dokta’ na Deogratius Mugassa.

Katika Hukumu Hakimu Moshi akisema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya washitakiwa bila kuacha mashaka yoyote,hata hivyo upande wa Jamhuri ilikata rufaa Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.

 Rufaa hiyo inatarajiwa kuendelea kuunguruma tena kesho Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya mrufani (Jamhuri) ya kutaka Muro na wenzake warudishwe kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ili kesi yao ianze upya kusikilizwa.

Maombi hayo yalitolewa na Mawakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya na Awamu Mbagwa, Februari 18, mwaka huu, siku ya kwanza ya usikilizwajiwa rufaa hiyo ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Kisutu iliyowaachia huru Muro na wenzake. Hatahivyo Mahakama Kuu katika uamuzi wake ilitupilia maombi hayo ya Jamhuri na badala yake iliamua kuendelea na usikilizwaji wa rufaa hiyo.

Katika rufa hiyo kesho upande wa Jamhuri itaendelea na hoja zake nyingine za kupinga hukumu ya Kisutu, ingawa Wakati wakitupilia mbali maombi hayo ya Jamhuri, Jaji Dk Fauz Twaib hakutoa sababu za kutupilia mbali maombi hayo ya Jamhuri na kudai kwamba atatoa sababu zake kwenye hukumu ya rufaa hiyo.

Katika maombi yake Jamhuri ilidai kuwa mwenendo wa kesi ya msingi una makosa ya kisheria, kwa kuwa Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo (Gabrile Mirumbe), alikosea kuweka kumbukumbu za mwenendo huo.

Wakili Mbagwa alidai kuwa kutokana na kasoro hizo, hata Hakimu (Frank Moshi) aliyeandika hukumu aliegemea katika mwenendo huo ambao haukurekeodiwa vizuri namatokeo yake hata hukumu aliyoitoa si sahihi .

Alifafanua kuwa kuna ushahidi wa baadhi ya mashahidi wa upande wa mashtaka umerekodiwa kwa namna ambayo hauakisi uhalisia wa kile kilichozungumzwa, na kwamba baadhi ya sehemu za ushahidi hazikurekodiwa kabisa.

Hata hivyo Mawakili wa wajibu rufani, Richard Rweyongeza naMajura Magafu walidai kuwa hoja za mrufani (Jamhuri) haziko wazi na kwamba hata kama kasoro zinazolalamikiwa zipo,lakini mrufani hajaonesha yalivyoathiri hukumu.

Wakili Magafu alidai kuwa kitendo cha Jamhuri kuomba kesi hiyo isikilizwe upya ni sawa na biashara ya kuchagua mahakimu kwamba wakishindwa kwa hakimu mmoja wanakwenda kubahatisha kwa hakimu mwingine.

Muro na wenzake, walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama na kuomba rushwa ya Sh10 milioni, kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Karoli Wage. Walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Februari 5, mwaka 2010, na kusomewa mashtaka ya kula njama na kuomba rushwa kutoka kwa Wage.

kwa hisani ya habarimpya































PICHA ZA MSIBA WA MAREHEMU ALBERT MANGWEHA HUKO SOUTH AFRICA




  WATANZANIA WALIOKO SOUTH AFRICA
WAKIWA NA BALOZI WA TZ





Toka huu msiba umetokea kumekua na habari ambazo zinaandikwa au kuripotiwa lakini hazina usahihi, pia habari ya kusafirishwa kwa mwili imeandikwa tofautitofauti kwenye vyombo mbalimbali lakini uhakika ni kwamba mwili wa Marehemu umepelekwa Airport ya Johannesburg June 3 2013 ambapo utasafirishwa june 4 kuelekea Dar es salaam na kufika mchana saa nane.
Hizi picha zimepigwa makusudi ili kutoa ushahidi kwa wale ambao bado walikua hawaamini kama mwili huu umefikia kwenye hatua za kusafirishwa kutokana na kuahirishwa kusafirishwa mara mbili kwa sababu ya taratibu za Serikali ya Afrika Kusini ambazo ilikua ni lazima zifatwe hasa ikizingatiwa kwamba Marehemu ni kutoka nje ya nchi hii na kifo chake ni cha ghafla



George Kalisa, Habib Awes, ambae ni mwakilishi wa Balozi wa Tanzania Afrika Kusini, Kinje Ngombale Mwiru na Mwamvita Makamba wakiwa nje ya Kanisa alipoagwa marehemu Albert Mangweha


Monday, June 3, 2013

AJALI MBAYA YATOKEA MBEYA ENEO LA NANE NANE UYOLE DARAJANI:YAJERUHI WANNE WAHOFIWA KUFA

 GARI LA ABIRIA AINA YA HIACE IKIWA IMEGONGANA USO KWA USO NA GARI AINA YA LAND CRUISER


HIZI NI BAADHI YA MAITI ZILIZO OKOLEWA PUNDE BAADA YA AJALI KUTOKEA 


HIVI NDIVYO DALADALA HII ILIVYO HARIBIKA BAADA YA AJALI HIYO KUTOKEA 

 


DALADALA IKIWA IMEUMIA VIBAYA 

 


BAADHI YA WANANCHI WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI

Saturday, June 1, 2013

J MARTINS AFUNGA NDOA KIMYA KIMYA NA NNEZI TIZAMA PICHA ZOTE HAPA

Msanii na produza maarufu J Martins (Jina lake halisi: Martins Okey Justice) amefunga ndoa ya kisirisiri na mpenzi wake aitwaye Nnezi Mbila baada ya kufunga ndoa ya kimila mwezi januari. ndoa hiyo ilifunga tarehe 30 /5/2013




















Hili ndilo Tamko Rasmi la Push Mobile na Bongo Records Kuhusu Mauzo ya Nyimbo za Mangwear Kwenye Simu