Wednesday, November 28, 2012
Tuesday, November 27, 2012
Monday, November 26, 2012
SHARO MILLIONEA AFARIKI KATIKA AJALI
AMAKWELI UDONGO UNAFAIDI
Kuna habari za kusikitisha na uhakika kuwa msanii aliyekuwa maarufu kwa jina la Sharo Millionea, msanii wa muziki na maarufu katika kuwepo kwake katika matangazo kwa style ya aina yake amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari Tanga.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi
Wednesday, November 21, 2012
VIJANA WA UMRI KATI 20 NA 45 KUTOJITOKEZA KUPATA HUDUMA YA TOHARA
Na Mercy Mwalusamba
Iringa
Iringa
Huduma ya tohara inayoendelea kutolewa katika hospitali ya mkoa wa Iringa imekuwa na mafanikio katika kipindi cha mwaka 2010 – 2011 kufuatia kampeni maalumu ya dondosha mkono sweta
Akizungumza na waandishi wa habari jana Muuguzi wa hospitali ya Mkoa katika kitengo cha upasuaji Iluminata Sanga alisema kabla ya mpango wa serikali juu ya huduma ya tohara na uhamasishaji katika kampeni ya dondosha mkono sweta, hali ya wananchi waliopata huduma hiyo ilikua chini kwa asilimia 35
Alisema baada ya mpango mkakati kuanza mwaka 2010 huduma imetolewa kwa mpango maalumu kupitia hospitali ya mkoa pamoja na vituo vya afya vya Ngome manispaa,hospitali ya Tosamaganga Mufindi na Lugoda ambapo jumla ya watu waliopata huduma ni 10,302 hadi sasa
Huduma ya tohara imefanyika kwa kiwango kikubwa vijijini ikilinganishwa na mjini ambapo wengi wao ni watoto kati ya umri 10 hadi 14 na 15 hadi 20 idadi iliyofikia asilimia 65 alisema Sanga
Sanga alisema hali ya usafi kwa mtu aliefanyiwa tohara ndio jambo la msingi kwani bila kua na hali ya usafi katika kidonda husababisha madhara na kidonda kutokupona haraka
“Watu wanaokuja kupata huduma wamekuwa wakipewa elimu ya ushauri nasaha na upimaji wa afya kwakuzingatia vipimo muhimu ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea baada ya tohara” alisema
Aliongeza kuwa kumekuwa na baadhi ya watoto wenye umri chini ya miaka 18 ambao hufika peke yao kupata huduma hii bila wazazi wao au walezi kinyume na utaratibu kwani huduma kwa watoto wa umri huo hutolewa chini ya uangalizi na usimamizi wa wazazi
Alisema kuna haja ya kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na tohara ili kuepukana na changamoto zilizojitokeza kama kufikiri kufanyiwa tohara ni kuruhusu kuendelea kufanya vitendo vya ngono au kupunguza nguvu za kiume
“tohara inamsaidia mtu kuishi katika mazingira salama ya kupunguza uwezekano wa maabukizi ya magonjwa ya ngono”
……………………….MWISHO……………………..
MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI AFIKISHWA MAHAKAMANI TENA
Na mercy Mwalusamba
Iringa
Iringa
MTUHUMIWA wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi alifikishwa mahakamani jana katika ulinzi mkali huku waandishi wa habari wakiendelea kuzuiwa na polisi kupiga picha.
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia wengine waliokuwa na silaha mbalimbali huku wengine wakivaa kiraia waliweka ulinzi mkali kuhakikisha waandishi wa habari hawapati mwanya wa kupiga picha.
Mwendesha mashtaka wa serikali Adolf Maganda aliambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Dyness Lyimo kuwa upelelezia wa kesi hiyo haujakamilia.
Pasificus Cleophace Simon (23) alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tuhuma ya kumuua kwa makusudi mwandishi huyo katika ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa uliofanyika Septemba 2 mwaka huu.
Mtuhumiwa huyo mwenye namba G 2573 alifikishwa mahakamani hapo kwa
gari la polisi lenye namba PT 1404 likiwa na ulinzi mkali akiwa amefichwa uso kiasi cha kutoonekana macho yake.
Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC linalosadikiwa kuwa ni la RCO huku kwa mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani hapo kwa gari namba DFP 2175 pick up akiwa katika ulinzi mkali huku waandishi wa habari wakidhibitiwa na polisi na mmoja wao kunusurika kupigwa jambo lililozusha hisia tofauti miongoni mwa wananchi wengi mkoani hapa.
Kwa mujibu wa wakili huyo, upelelezi haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Desemba 05 mwaka huu itakapotajwa tena.
Unyanyaswaji wa waandishi wa habari wakati wa kupiga picha za mtuhumiwa wa mauaji hayo unaendelea kushika kasi baada ya mwandishi wa gazeti Tanzania daima kupigwa na askari kanzu kwenye chumba cha mahakama alipotaka kupiga picha kabla ya mahakama kuanza jambo ambalo limelaaniwa vikali na waandishi pamoja na wananchi waliokuwepo mahakamani hapo.

Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka huu katika kijiji cha Nyololo yo alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi hayo.
………………………………………………. Mwisho ………………………………………..
Subscribe to:
Posts (Atom)